Ujenzi wa Mbinu za
Uongozi wa Kifeministi (feminist leadership Styles)
Zipo makala nyingi
zinazozungumzia jinsi wanawake wanavyotumia mbinu tofauti kwenye uongozi.
Inadaiwa kuwa, kutokana na jinsi zao, wanawake huwa na uwezo mkubwa wa
kusikiliza, kupokea ushauri, kushawishi, kushirikisha, kusoma alama za nyakati
na kutumia ubunifu kwenye kutatua migogoro.
Baadhi ya mashirika makubwa ya binafsi
wamegundua vipaji hivi na kuanza kuwateua wanawake kama wakurugenzi wa
makampuni yao, jambo ambalo limewezesha kampuni hizi kuongeza faida kubwa
kwenye uzalisaji wa bidha zao ( Tiffany Harper and Hughey Gorge inapatikana https://womenlovetech.com/7-leadership-skills-ofpsucessful-women) .
Vilevile Utafiti uliofanywa na Rusimbi M,
Meena R na Carolyne I (2018) ulibainisha baadhi ya viwezeshi vinavyosababisha
uongozi mbadala wa wanawake. Baadhi ya viwezeshi ilikuwa ni pamoja na vipaji
binafsi (personal traits) ikiwa ni pamoja na msukumo na hisia za kutaka kuleta
mabadiliko ya mfumo kwa haraka, ubunifu, uwezo wa kusikiliza na kukubali
ushauri, uwezo wa kusoma alama za nyakati na urahisi wa kubadili mbinu bila
kuyumbisha dira na uwezo wa kushirikiana na kuwa na mitandao wezeshi.
Uongozi wa wanawake
unaangalia kwa haraka mahitaji ya watu, au mahitaaji ya msingi ya kijinsia
kuliko yale ya jumla. Wakati mwingine, jamii inachukulia kwamba wanaangalia
masuala madogo madogo sana, ila hayo ndiyo huchangia ufanisi kwa yale makubwa. Mfano,
mahali pa kunyoneshea na kutunzia watoto kwa mfanyakazi anayenyonyesha ili
aweze kukaa kazini kwa masaa mengi na kuongeza ufanisi. Ukilitangalia hili kwa
haraka unaweza kuona kwamba ni jambo la wanaharakati wa haki za wanawake lisilo
na mafanikio.
Swali : Je
Mimi kama kiongozi natumia mbinu zipi za uongozi?Kuna fursa zipi za kuleta
Mabadiliko ya Mbinu za Uongozi? Na Changamoto zipi?
No comments:
Post a Comment