Sunday, August 14, 2022

Dhana za Jinsia: JINSI na JINSIA (SEX AND GENDER)

 

Dhana ya 1:  Jinsi na Jinsia

Jinsi: Kwa kawaida, binadamu huzaliwa na jinsi ya kike au kiume. Jinsi hizi ni tofauti za   kibaologia tu. Tofauti hizi za kibaologia hazina tabaka na hazihusiana na nani kati ya mwanamke au mwanaume ni wa hali ya juu zaidi ya mwenzake. Hali ya kuzaliwa ke au me (biologia) haibadiliki. Hali hii ina majukumu yake (kama mfano, mwanamke hubeba mimba na kunyonyesha na mwanamume hutunga mimba)

 

Jinsia: Ni dhana ambayo hutumika katika kuelezea mahusiano ya kijamii yaliyojengeka kati ya mwanaume na mwanamke. Dhana hii hutumika kuelezea tafsiri ya kijamii kuhusu maana ya kuwa mwanamke au mwanaume, ikiwa inatoa utofauti katika thamani ya utu wao, stahiki na haki zao pamoja na nafasi zao kama vile: wajibu au kazi, madaraka, maamuzi, umiliki wa rasilimali n.k. Hivyo basi, dhana hii mara nyingi hutumika katika kutoa tafsiri ambayo inaelezea mahusiano yanayooundwa na jamii, na ambayo huwa nje ya tofauti za kibaolojia kati yao. Tafsri hii ya kijamii ambayo mara nyingi huimarishwa na mifumo ya kidini, kielimu na kisera/bajeti, inaashiria kumbebesha mwanamke wajibu mkubwa katika kuzalisha na kuendeleza kizazi na nguvu kazi ya jamii husika na kumnyima haki sawa na hasa usawa wa kufikia na kumiliki huduma za kijamii, raslimali za nchi, kufaidi matunda ya jasho lao pamoja na ushiriki ulio imara katika maamuzi yanayogusa maisha ya jamii kutoka ngazi ya familia, kitaifa na kimataifa. Vilevile   wakati mwingine kuondoa utu na thamani ya maisha yao kwa njia ya kuhalalisha au kuendeleza vitendo vya ukatili na udhalilishaji dhidi yao. Kwa kuwa mahusiano haya yamesababisha pengo la kijinsia yamejengwa na wanajamii (wa kiume na wa kike) yanaweza kubadilishwa na kuleta usawa wa kijinsia yenye tija katika jamii (WFT: Kitita cha Mafunzo ya Rushwa ya Ngono).



No comments:

Post a Comment