Mchakato wa Mabadiliko Binafsi katika uongozi wa kifeminia
na deogratius Koyanga
Makala ya Valerie Miller na VeneKlasen (2012) Imebainisha kanuni nne za
kuzingatia kwenye mchakato wa mabadiliko binafsi kwa wanaharakati watetezi wa
haki za wanawake. Katika harakati kuna uongozi, uongozi ili uwe na ufanisi na ulete mabadiliko, unahitaji mabadiliko binafsi ya kiongozi. Kiongozi awe na mtazamo chanya, abadilishe mtazamo wake wa awali kabla ya kuwa mwanaharakati, na pia aweke misingi ya kutaka kuona mabadiliko chanya yatakayosababishwa na yeye. kwahiyo hapa ni lazima abadilike. Valerie na veneKlasen, wanandika hizi kanuni ambayo zitatusaidia kubadilika sisi kwanza:
Kanuni
ya Kwanza ni: Ujuzi na Ufahamu muhimu
Waandishi hawa wanadai kwamba elimu na maarifa ya itikadi ya ukombozi
wa mwanamke inaanza kwenye maisha halisia ya mwanamke anayopitia kwenye safari
ya mabadiliko.
Maarifa haya hayapatikani kwenye darasa rasmi, bali yanatokana na
uzoefu unaoanza kwa kujiifunza kuhoji mambo yalivyo “kawaida” Mifano ya maswali
ni kama haya
Mchakato wa kuanza kuhoji ubaguzi na mifumo kandamizi humjengea
mwanamke yoyote ufahamu na hamasa kubwa ya kutamani mabadiliko .
Makala za Valerie Miller na VeneKlasen (2012) zimebainisha viwango vya
ufahamu vinavyochochea wanawake na hasa viongozi kuchukua hatua za kudai na
kufanya mabadilko wanapopata fursa ya kushika usukani wa uongozi.
Kanuni ya 2: Kuhakikisha
na Kujenga Juu ya Ufahamu wa Wwanawake na Roho (Validating and building on women’s
knowledge and spirit)
Katika safari ya kujenga uelewa na ufahamu binafsi, lazima
mwanaharakati afike mahali ambapo anajenga imani na ile ajenda bila wasiwasi au
mashaka. Kwenye ngazi hii kunahitajika wingi wa watetezi wenye uelewa wa muktadha na mifumo kandamizi ili
iimarishe uelewa na ufahamu (knowledge and consciousness raising). mambo ambayo
yanawezesha kuhakikishia misimamo iliyochukuliwa na mielekeo ni pamoja na
kusoma kumbukizi za wapambanaji, mashairi, nyimbo na sanaa zinazoimarisha
uelewa kukuza hamasa na kuhakikisha misimamo ya binafsi na mielekeo.
Kanuni
ya 3. Kuelewa na kutafakari suala la mamlaka (Understanding and navigating
power).
Uwezo wa mwanaharakati kujenga uelewa wa jinsi
mamlaka(nguvu) ndani ya jamii ya mfumo dume inavyofanya kazi ni nyenzo muhimu
ya kumwezesha kuungana na wengine katika kujenga mikakati ya kuvunja hizi nguvu
na kujenga njia mbadala ya kutumia nguvu zilizoko kwenye nafsi zao (power within)
Wachambuzi wa jinsi mamlaka (power) inavyofanya kazi ndani
ya jamii wamebainisha njia mbili. Kwanza kwa njia inayoonekana (visible power), ikiwa ni pamoja na
sheria, sera zinazohalalisha ubaguzi wa jinsia. Mamlaka au nguvu iliyojificha
(invisible power) Wenye mamlaka kama viongozi wa dini, matajiri wa dunia na
taasisi zinazowalinda kama Benki Kuu ya Kimataifa, Shirika la Biashara la
Kmataifa, vina uwezo wa kuumba? au kujenga
ajenda za kisiasa zinazolinda maslahi yao. Kwa mfano sera za kubinafisisha huduma
za jamii, sera za soko huria zote hizi zinalinda maslahi ya mabepari,
zinawakandamiza maskini na mafukara wa dunia na kuwabebesha wanawake mzigo wa
ziada kwenye shughuli za kuendeleza kizazi na nguvu kazi.
Uelewa wa jinsi nguvu hizi zinavyofanya kazi huwezesha
mwanamke mmoja mmoja kuona umuhimu wa kuunganisha nguvu zake kujenga mshikamano
wa kupambana na hizi nguvu kandamizi.
Kanuni
ya 4 - Kujitunza (Moyo, akili-mwili) (Self-care
- Heart-mind-body)
Afya ya kiongozi ni rasilimali kwake, kwa familia, kwa
shirika au asasi anayoongoza na kwa tapo la utetezi wa haki za wanawake
kimapinduzi. Mara nyingi shughuli za uanaharakati ni kazi inayotumia nguvu
nyingi ya kimwili, kiakili, kifikra na
hata kiroho. Shughuli hizi ukiunganisha na shughuli nyingine za uzalishaji (productive)
na za kuendeleza kizazi (reproductive) zinaweza ziwe na athari kubwa kwenye
afya ya hisia (emotional health), afya ya mwili (physical health) na afya ya
akili (mental health).Umuhimu wa kujali afya ni sehemu muhimu za uanaharakati wa mapambano dhidi ya mifumo kandamizi..
Misingi Binafsi inayomwongoza kiongozi wa harakati za utetezi wa
wanawake kimapinduzi
Ø
Hii inamaanisha kwamba, kiongozi wa harakati za
ukombozi wa wanawake kimapinduzi ni yule mwenye kuamini na kuongozwa na misingi ya usawa, na ukombozi wa wanawake kimapinduzi.
Ø
Ni kiongozi anaehamisika na uelewa wa itikadi na
mwenye utayari wa kujiimarisha kwenye uelewa huu ili aweze kujenga mazingira
wezeshi ya kujifunza pamoja (shared learning).
Ø
Mwenye dhamira ya kuweka mifumo mibadala ya
uongozi itakayowezesha ushiriki wa pamoja katika kujenga ajenda ya pamoja,
kujadili, kuendeleza na kutetea ajenda ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi.
Ø
Ni kiongozi mwenye dhamira, nia na uwezo wa kuchambua hali halisi ya muktadha wa siasa na
uchumi kwa kubainisha fursa na changamoto za kuendeleza harakati za utetezi wa
haki za wanawake kimapinduzi.
Ø
Ni kiongozi mwenye uwezo wa kushirikiana na
wenzake kubainisha mafanikio ya pamoja na mwenye utayari wa kuwajibika kutokana
na makosa au mapungufu yatokanayo na maamzi ya pamoja (celebrate collective
achievements and assume individual accountability on behalf of the collective).
Ø
Kiongozi mwenye uwezo na dhamira ya kujenga
mahusiaono mbadala ndani ya shirika yenye kujali utu wa kila mmoja, wenye
kusaidiana wakati wa shida na mwenye kutabiri viashiria vya kugawa nguvu za
pamoja.
Ø
Ni kiongozi mwenye utayari wa kushikamana,
kutandaa na viongozi na mitandao yenye
kuongozwa na misingi ya utetezi wa wanawake kimapinduzi kama mkakati wa ujenzi
wa tapo la kusambaratisha mfumo dume.
Ø
Ni kiongozi mwenye upeo wa kuona mahusiano kati
ya mfumo dume na mifumo mingine kandamizi inayotumia rangi, jinsi, tabaka, hali
ya maumbile na ujinsia wa mtu kukandamiza na kuwabagua wanawake na watu waliko
pembezoni.
Ø
Kiongozi mwenye dhamira na utayari wa
kushirikiana na wengine katika kupambana na mifumo mingine kandamizi bila
kupoteza ajenda ya ukobozi wa mwanamke kimapinduzi.
Ø
Vilevile ni kiongozi mwenye nia na dhamira ya
kushirikiana kwa kugawana majukumu na siyo kushindana.
Ø
Ni kiongozi anachukulia cheo kama dhamana inayompa wajibu na siyo
mamlaka ya kutawala na kumrisha.
Ø
Mwisho na siyo kwa daraja ni kiongozi mwenye
kujali afya yake na ya wale anaowaongoza kama mkakati wa kujenga afya ya
shirika na afya ya tapo.
Ø
Mwezeshaji ajumuishe akizingatia mwongozo wa
Mkataba wa Kanini za Ukombozi wa Wanawake wa Kiafrika Kimapinduzi.
No comments:
Post a Comment