UCHAMBUZI:
Takwimu za Kijinsia kwaajili ya maendeleo
shirikishi
Mara kadhaa wachambuzi na wadau wa Haki za wanawake, Usawa
wa Kijinsia na Haki za Binadamu wamekuwa wakisisitiza serikali kutenga bajeti
kwa mrfengo wa Kijinsia ili kukidhi mahitaji ya makundi yote.
Suala kubwa katika usawa wa Kijinsia na Bajeti ni mgawanyo wa rasilimali zote zilizoko katika nchi kwa kuzingatia mahitaji ya watu wote yaani (wanawake, wanaume, watoto wa kike na kiume, wazee, watu wenye ulamavu na watu wanaoishi pembezoni kwa kuokota matunda na kuwinda).
Wakati huu wa zoezi la kuhesabu sense ya watu na makazi, ni muhimu kila mtu kutambua kwamba, ushiriki kamilifu kwenye zoezi hili, kwa kutoa taarifa sahihi za makundi haya kutawasaidia watunga sera, waandaji wa bajeti kupanga kwa kuzingatia idadi ya watu waliopo.
Takwimu za kijinsia ni muhimu katika kuwaongoza waandaaji wa mipango na wafanya maamuzi kufahamu hali halisi ya kijinsia na hivyo kuweza kuandaa majibu sahihi ya changamoto zilizopo.
Takwimu hizi zinapatikana kutoka katika vyanzo mbalimbali na vilevile zimesambaa na hivyo kuwa vigumu kupatikana kwa taarifa kutoka katika vyanzo vyote. Serikali pamoja na Asasi za Kiraia (AZAKI) na wadau wengine hukusanya takwimu zilizochambuliwa kijinsia, zikihusisha idadi ya watu, masuala ya afya, maendeleo ya jamii, kilimo, uchumi, elimu, huduma za jamii, mazingira, na taarifa kuhusu ajira.
Takwimu hizi hukusanywa kupitia sensa ya watu na makazi, tafiti na takwimu za kiutendaji. Nyaraka nyingine nyingi zimebainika kuwa na taarifa muhimu za kijinsia kwa ajili ya uandaaji wa sera na programu.
Aidha, nyaraka nyingine zimeonekana kutokuwa na taarifa toshelevu za kijinsia na hazijumuishi masuala mapya kuhusu hali ya wanawake na usawa wa kijinsia.
Katika muktadha huu, upo umuhimu wa kujenga uelewa wa masuala ya takwimu kwa sekta zote kuanza kukusanya na kuchakata takwimu kwa kuzingatia masuala ya kijinsia kutekeleza mpango wa ufuatiliaji na tathmini wenye mtazamo wa kijinsia.
Serikali yetu ipo kwenye mchakato wa kupitia sera ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya mwaka 2000 ambayo sasa takwimu za sense ya mwaka 2022 zitawezesha sera kukamilika vizuri ikiwa na takwimu sahihi.
Ni jukumu la kutambua kuwa Hii
itasaidia kuhamasisha ufuatiliaji wa mara kwa mara wa sera za kisekta, miradi,
programu na mipango kwa ufanyaji wa maamuzi yenye tija
No comments:
Post a Comment