Mapengo ya Kijinsia
hutokea pale ambapo tafsiri za jamii kuhusu haki, wajibu na majukumu inaashiria
kujenga tabaka au mapengo kati ya mwanamke na mwanaume katika ngazi mbalimbali.
Mapengo haya ya kijinsia hupelekea kuwepo kwa tofauti ya ufikiaji wa rasilimali
kama vile umiliki wa ardhi, nyumba, biashara, tofauti za mishahara, ufikiaji wa
huduma za msingi kama elimu, bima ya afya, nk. Vilevile mapengo ya jinsia
huonekana kwenye mgao wa uzito wa kazi, haki na ule wa mapato. Kwa ufupi,
mapengo ya kijinsia hutokea pale ambapo kumekosekana haki (social justice) kati
ya mwanamke na mwanaume na hivyo kusababisha ubaguzi wa jinsia na uwiano usio
sawia kati ya mwanamke na mwanaumme kwenye nyanja zote za maisha.
No comments:
Post a Comment