Uongozi
na deogratius temba
Uongozi ni dhana inayotumika kuelezea sifa za wenye mamlaka na maamuzi katika nafasi
mbalimbali. Dhana hii inapotumika kueleza sifa
za uongozi uliojikita kwenye misingi ya
mfumo dume, dhana huonesha tabia
ya wenye mamalaka ya kandamizi,
kutawala, kuamirisha na kuhodhi maamuzi ya mwisho.
Uongozi uliojikita
kwenye itikadi ya kifeministi ni dhana
yenye kuonesha sifa na tabia za mtu au watu waliokabidhiwa mamlaka wenye
kuamini katika haki za wanawake na makundi yalioko pembezoni, ni uongozi
ushirikishwaji wa wengi kwenye kupanga,
kutatua matatizo hatimaye uongozi
unabebeshwa wajibu wa kufanya maamuzi na kuwajibika pale kwa matokeo hasi au
chanya.
Ø
Uongozi unahusu matumizi ya mamlaka , ni jinsi gani mamlaka
inatumiwa aidha kukandamiza au kuwezesha
Ø
Uongozi wa Kifeministi unahusu uwezo wa kuchambua na kuelewa
hali halisi, kuwa na maono, na dira ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi. Tafsiri zinazojikita
kwenye tabia ya uongozi zinabainsiha kiongozi bora kama mtu mwenye uwezo wa
kuonyesha njia, kufanya maamuzi, kutafsiri maono na ndoto za shirika, kuhamisisha
wengine kuamini kwenye ndoto na kuweka mikakati ya kutekeleza ndoto na maono ya
shirika/taasisi
Ø
Uongozi unahusu matendo. yenye kuongozwa na dhima ya maadili na
heshima kwa wanawake, watoto na watu wenye changamoto. Tafsiri hii ni ile
inayobainisha mchakato na matendo ya pamoja yenye kuwezesha mabadiliko
yaliyobuniwa pamoja. Tafsiri hii inabainisha uongozi kama mtu au watu wachache
wenye kushirikiana na wengine katika kuleta mabadilko ya mfumo ( transformational leadership)
No comments:
Post a Comment