Kuhusu dhana ya Ufeministi
Ufeministi ni dhana
inayobeba mambo mengi ikiwa ni pamoja na aina nyingi za misimamo, itikadi na
harakati tofauti zinazochangia kwenye azma ya kutetea haki za wanawake dhidi ya
ubaguzi wa jinsia katika nyanja za siasa, uchumi na ustawi wa jamii
Ufeministi kama
itakavyotumika kwenye nyaraka na machapitisho mengi, ni itikadi inayoongozwa na Imani kuhusu usawa
wa wanawake na vitendo vinavyoashiria kutokomeza mifumo inayobagua wanawake
kwenye nyanja zote za uchumi, siasa na hata ustawi wa jamii. Ingawaje kuna
misimamo na mirengo inayotafautiana kwenye ufafanuzi wa dhana hii ya ufeminist,
kuna mambo ya msingi yanayowaunganisha wanaharakati wote watetezi wa haki za
wanawake kimapinduzi.
Dhana ya kifeminist ni kutetea haki na usawa kwa wote bila ubaguzi. kuhakikisha mifumo, miundo na rasilimali zinalenga kujenga jamii yenye usawa bila ubaguzi au unyanyasaji. ufeminia, sio kitu kibaya au sio watu wanaokwenda kinyume na maadili au mila na desturi nzuri isipokuwa Mfeminia hawezi kukubaali kunyamaza akiona mila, desturi, mfumo unamkandamiza mwingine.
No comments:
Post a Comment