Na Deogratius Temba
Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umewasilisha mapendekezo
ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge, jijini
Dodoma.
Mapendekezo hayo ambayo yanalenga kuishawishi serikali
kuingiza masuala ya Kijinsia kwenye sekta ya Elimu ili kuongeza ubora wa elimu
unaowanufaisha wanafunzi wa kike, kiume na wenye ulemavu yamewasilishwa kwa
kwmaati ya Kudumu ya Bunge wakati ambapo mchakato wa bajeti kwa mwaka wa fedha
2023/2024 unaendelea.
Miongoni mwa mapendekezo yaliyowasilishwa kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ni pamoja na:
Utengwaji wa bajeti kwa ajili ya kutoa pedi bure kwa
wanafunzi; ambapo TEN/MET ilishauri kwamba serikali iondoe kodi ya VAT kwenye bidhaa za hedhi salama. Na pia serikali itenge fedha kwenye Bajeti
zake za elimu kwa ajili ya kuwezesha wasichana kupatiwa taulo za kike bure shuleni.
Kutokana na kuendelea kuwepo kwa mdondoko wa wanafunzi wa
kike na wa kiume kwenye mfumo wa elimu ya msingi na sekondari. TEN/MET ilipendekeza, kuweka mkazo kwenye
ujenzi wa mabweni katika shule za kata na kuhakikisha watoto wanapata chakula
shuleni
Pia TEN/MET ilipendekeza kwamba serikali iangalie namba ya kuongeza bajeti ya
Miundombinu mfano idadi toshelezi ya vyoo
vyenye mfumo wa maji tiririka kwenye shule za msingi na sekondari. “Tunapendekeza,
bajeti kwaajili ya SWASH program isimamiwe kikamilifu kuondoa changamoto hii.
Halmashauri ambazo hazipo kwenye miradi ya SWASH zielekezwe kutenga fedha kupitia
mapato ya ndani ili vyoo vinavyojengwa viweze kuwa na miundombinu yenye kukidhi
mahitaji ya hedhi salama, hii itasaidia wasichana wanaoingia hedhi kushiriki
masomo kwa siku zote bila kukosa” alisema sehemu ya mapendekezo hayo
iliyowasilishwa na Deogratius Temba, mchambuzi na mkufunzi wa Bajeti yenye
mrengo wa Kijinsia.
Pia ilielezwa kwamba wasichana
walio acha masomo kwa ujauzito
wanakumbana na changamoto mbalimbali wakati wa kurejea shuleni katika mfumo
rasmi na usio rasmi. Na kupendekeza
kwamba serikali imarishe vituo vya kutolea elimu ili viwe rafiki kwa wanafunzi
hao
Awali akitoa utangulizi kwa mbele ya Kamati, Meneja Programu wa TEN/MET, Bi.
Martha Makala, alisema kwamba TEN/MET ni Mtandao mpana unaoundwa na mashirika Zaidi
ya 180 ambayo yanafanya kazi nchi nzima yakiwa ynajishughulisha na afua
mbalimbali za elimu hasa utetezi kwenye usawa wa Kijinsia katika elimu.
Alisema kwamba, pamoja na kufanya afua za kutoa elimu,
mashirika wanachama wa TEN/MET waliosambaa kila kona ya nchi wamechangia kwa
kiasi kikubwa ujenzi wa miundombinu ya kutolea elimu chini kwa kushirikiana na
halmashauri za wilaya.
No comments:
Post a Comment