Thursday, August 25, 2022

HATUA NA NYENZO MUHIMU ZA UANDAAJI WA BAJETI YA KIJINSIA

 

HATUA NA NYENZO MUHIMU ZA UANDAAJI WA BAJETI YA KIJINSIA

imendaliwa na Deogratius Temba

Uingizaji wa masuala ya Jinsia siyo Mipango na Bajeti mpya bali ni Mipango na Bajeti jumuishi yenye mtazamo wa Kijinsia (Gender Perspective). Kuna hatua mbalimbali za kuzingatia katika kuingiza masuala tangu ngazi ya uibuai hadi ngazi ya Ufuatiliaji na Tathmini za shughuli. Aidha hatua hizi kama njia ya kufikia usawa wa Kijinsia hutumia pia mikakati mitatu ya kufikia usawa wa Kijinsia ambayo ni Ujumuishi, Mageuzi ya kutoa usawa katika kuthaminisha michango ya wanaume na wanawake na kufanya mabadiliko katika mfumo wa Kijinsia. 

Hatua hizi ni kama zifuatazo:

1.  Uibuaji na Uchambuzi wa Hali halisi/Mazingira

N muhimu sana kutumia mbinu shirikishi katika kuibua na kufanya uchambuzi wa masuala ya kijinsia katika jamii kabla ya kupanga sera, mipango na bajeti katika ngazi husika iwe ya kaya, Halmashauri au ngazi ya Taifa. Mipango Mikakati mingi ya Halmashauri inakosa data zenye mnyambuliko wa kijinsia kutokana na kutozama kwa wananchi na kuibua masuala ya kijinsia kisha kuyafanyia uchambuzi. Hii inahafifisha sana ubora wa bajeti katika ngazi ya Halmashauri.  Katika kuibua na kuchambua masuala ya kijinsia, ni vyema sana kuzingatia vipengele vifuatavyo kulingana na sekta husika (mkazo ni sekta nyeti zinazogusa makundi ya pembezoni). Uibuaji na uchambuzi ni lazima uzingatie 

1.       Uchambuzi wa Masuala ya Kisekta na Mnyambuliko wa Data Kijinsia

Wakati wa kufanya upembuzi yakinifu (baseline survey) ni muhimu kujiuliza maswali yafuatayo 

  • Nani anafanya nini (mgawanyo wa majukumu ya uzalishaji na majukumu ya kaya) 
  • Nani anafikia na kumiliki rasilimali kati ya wanaume na wanawake
  • Nani anafanya maamuzi 
  • Nani ananufaika na rasilimali hizi 

Hatua hii itakuasaidia kupata data zenye mnyambuliko wa kijinsia kwa kila swali na inasaidia sana katika kuandaa sera, mipango na bajeti kwa jicho la kijinsia 


                                    Katuni hii imechorwa na Muhidin Msamba, kwa hisani ya TGNP



2.                                      Kufanya uchambuzi kwa mbinu ya mti wa matatizo 

  • Suala kuu la kijinsia lililoibuliwa 
  • Visababishi 
  • Athari zake 

3.                                      Kufanya uchambuzi wa Wadau na Kubaini vipaumbele 

Ni muhimu baada ya uchakataji wa taarifa za uwandani, kuweka vipaumbele kwa kuzingatia halihalisi kutoakana na majibu ya maswali ya vipengele vya hapo juu

Kwa kila kipengele ni muhimu kubaini waathirika wakuu, wenye ushwishi, watekelezaji wa sera na watunga sera. Hii itasaidia katika uwajibikaji wakati wa kupanga bajeti yaani kila idara itenge bajeti kulingana na halihalisi na waathirika wakuu kijinsia na kimaeneo. 

4.                                      Kufanya uchambuzi wa sera 

Ni muhimu baada ya kutoka uwandani na kubaini masuala na vipaumbele, kufanya uchambuzi wa sera ili kuona ni namna gani sera inashghulikia kadhia hii. Maswali yafiatayo yakuongoze wakati unafanya mapition na uchambuzi wa sera. 

  • Je sera ipo kushughulika kadhia hii?
  • Kama sera ipo, Je sera ina mapungufu gani?
  • Kama haina maoungufu, je inatekelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na suala bainifu kuundiwa mikakati na kungizwa kwenye mipango na bajeti ya Halmashauri? 

5. Kuweka Malengo na kuandaa Mpango wa Utekelezaji (Annual Plans) 

Ni vyema kila sekta iweke malengo kulingana na muda wa utekelezaji ili kushughulikia masuala yaliyoibuliwa kwenye mchakato wa uibuaji na uchambuzi. 

  • Malengo ya muda mfupi (outputs)
  • Malengo ya kati (outcomes)
  • Malengo ya muda mrefu (impact) 

Hata hii itakuasaidia kuandaa mpango kazi kwa mwaka na hata kusaidia katika utoaji wa taarifa. Safu za mpango huu lazima ziwe na vipengele vya suala la kijinsia, visababishi na athari zake, walengwa/waathirika wakuu, shughuli zitakazofanyika, viashiria vya utekelezaji, fungu la fedha lililotengwa, mratibu mkuu na muda wa utekelezaji. 

6.  Kutenga Rasilimali kwa kuzingatia Jinsia (Gender Sensitive Resource Allocations) 

Kama utazingatia vyema na kwa weledi na uadilifu hatua zote hapo juu ni rahisi sana kutenga bajeti kijinsia kwani itakua imebeba mahitaji na vipaumbele vya makundi yote ya jamii 

7.       Kufuatilia kujifunza na kutathmini Utekelezaji

1.       UFUATILIAJI 

Ufuatiliaji na tathnini wa kisera, mipango, mikakati na bajeti vinapaswa kuwa na mwitikio wa kijinsia na viashiria mahususi vya jisia. Ufuatiliaji na tathmini wenye mwelekeo wa kijinsia unapaswa kuwa na vigezo vifuatavyo:-  

a.                                      Kuwa na malengo na viashiria vya ufuatiliaji vyenye mrengo wa kijinsia

b.                                      Kuzingatia ukusanyaji wa  data zenye mnyambuliko wa kijinsia.

c.                                      Kujumuisha viashiria mahususi kwa ajili ya uingizaji wa maswala ya kijinsia

d.                                      Kufuatilia maendeleo kuelekea kukidhi mahitaji mahususi ya wanaume na wanawake

e.                                      Kuhakikisha kwamba wanaume na wanawake wana ushiriki sawa na wanahudumiwa sawa wakichukuliwa kwamba ni watoa maamuzi, watekelezaji na washiriki.

f.                                       Kupima matokeo kwa wanaume na wanawake kutoka hatua ya utekelezaji wa sera/ mpango/mradi.

g.                                      Kuhakikisha kuwa rasilimali na unufaikaji vinagawanywa kwa uwiano kwa wanaume na wanawake.

h.                                      Kufuatilia endapo mpango au shughuli za  mradi zinapunguza tofauti za kijinsia au zinaongeza tofauti za kijinsia.

i.                                        Kuhakiki maeneo ambapo shughuli zinaongeza tofauti za kijinsia.

j.                                        Kuhakikisha kwamba wale walioshiriki kwenye utekelezaji wa sera/mipango/mradi wana motisha wa kuendeleza mwaswala ya kijinsia.

k.                                      Kufuatilia viashiria vya upimaji wa mabadiliko ya wanawake na wanaume katika mapokeo na uwezo wa kupokea mabadiliko.

l.                                        Kuweka kumbukumbu ya mifano bora na vipingamizi vinavyojitokeza kutoka kwenye hatua utekelezaji ambavyo vitashughulikiwa baadae.

8.       Tathmini

Tathmini muhimu kubainisha ni kwa jinsi gani shughuli zenye mrengo wa kijinsia zimeathiri mapokea na uwezo wa wanaume na wanawake.  Ili kuhakikisha kwamba tathmini inafikia kwa usahihi matokeo ya kundi husika la wadau/wanufaika, ni muhimu tathmini ikaandaliwa katika mfumo ulio kwenye mwitikio wa kijinsia. Kwahiyo kwa tathmini ya shughuli zinazohusiana na sera,mikakati, mipango na bajeti zinapaswa kuwa:-

a.                                      Kutathmini endapo rasilimali na vinginevyo vimegawanywa kwa kuzingatia uwiano kati ya wananwake na wanaume.

b.                                      Kupima endapo mpango wa malengo ya kijinsia uliowekwa umefikiwa.

c.                                      Kutathmini ni kwa kiwango gani malengo ya maendeleo yamefikiwa.

d.                                      Kutathmini ni kwa jinsi gani matokeo juu ya uingizwaji wa maswala ya kijinsia yanavyotokea.

e.                                      Kutathmini kama kulikuwa na matokeo ya kijinsia yasiyotarajiwa au yasiyokusudiwa.

f.                                       Kutoa maoni juu ya mambo ya kuzingatia wakati wa utekelezaji wa mpango ama mradi ujao.

9.       Muundo wa kitaasisi wa ufuatiliaji na Tathmini 

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ina jukumu la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli zenye mrengo wa kijinsia kwa Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa hivyo inao wajibu wa kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mpango huu katika ngazi ya kitaifa na ngazi ya serikali za mitaa. Katikakutekeleza majukumu yake kama mratibu wa jumla wa mpango huu, itafanya kazi kwa karibu na Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Wizara. Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pia itafanya kazi na Wizara za ki sekta na wadau wengine wa maendeleo wa kijinsia ili kupata taarifa ambazo zitahusishwa kwenye mfumo wa ufuatiliaji na utoaji wa taarifa wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

10.   Kujifunza

Kujifunza ni hatua ya kupata ufahamu au ujuzi kwa kujifunza, kutenda, kufundishwa,au kupata uzoefu wa jambo Fulani. Kujifunza ni muhimu katika kupata mambo ambayo yanahitaji shughuli za kuboresha mbinu, vigezo vya kiutendaji, mpango wa utekelezaji na tathimini.

Kujifunza kuna unganishwa na ufahamu na mawasiliano ya shughuli kwa jinsi zinavyokusudiwa kuzalishwa, kupatikana, pamoja na kutoa elimu na kuhakikisha kwamba elimu inayopatikana inatumika katika kujifunza kwa lengo la:-

i.Kupata na kuchangia elimu iliyopatikana wakati wa kuandaa na utekelezaji wa OR-TAMISEMI, Serikali za Mitaa, wadau wa maendeleo, Mpango/mradi na kutolea taarifa kwa ajili ya utoaji wa maamuzi ili kuongoza na kuboresha shughuli zikiwemo uandaaji wa mipango kwa matokeo sahihi na halisi.

ii.Kutambua mapungufu ambayo yanahitaji utafiti wakati wa mtiririko wa matukio ya mradi.

iii.Kuwezesha ushirikishanaji wa shuhuda ambazo zitawezesha shughuli za mradi kupokea na kutumia mifano ya mbinu bora.

iv.Kuwezesha utambuzi wa mapungufu pamoja na fursa za kujifunza

v.Kushirikishana uelewa na wengine ili kujenga fursa pana kwa ajili ya shughuli za mradi nchini

No comments:

Post a Comment