HATUA NA
NYENZO MUHIMU ZA UANDAAJI WA BAJETI YA KIJINSIA
imendaliwa na Deogratius Temba
Uingizaji wa masuala ya Jinsia siyo
Mipango na Bajeti mpya bali ni Mipango na Bajeti jumuishi yenye mtazamo wa
Kijinsia (Gender Perspective). Kuna hatua mbalimbali za kuzingatia katika
kuingiza masuala tangu ngazi ya uibuai hadi ngazi ya Ufuatiliaji na Tathmini za
shughuli. Aidha hatua hizi kama njia ya kufikia usawa wa Kijinsia hutumia pia
mikakati mitatu ya kufikia usawa wa Kijinsia ambayo ni Ujumuishi, Mageuzi ya
kutoa usawa katika kuthaminisha michango ya wanaume na wanawake na kufanya
mabadiliko katika mfumo wa Kijinsia.
Hatua hizi ni kama zifuatazo:
1. Uibuaji
na Uchambuzi wa Hali halisi/Mazingira
N muhimu sana kutumia mbinu
shirikishi katika kuibua na kufanya uchambuzi wa masuala ya kijinsia katika
jamii kabla ya kupanga sera, mipango na bajeti katika ngazi husika iwe ya kaya,
Halmashauri au ngazi ya Taifa. Mipango Mikakati mingi ya Halmashauri inakosa
data zenye mnyambuliko wa kijinsia kutokana na kutozama kwa wananchi na kuibua
masuala ya kijinsia kisha kuyafanyia uchambuzi. Hii inahafifisha sana ubora wa
bajeti katika ngazi ya Halmashauri. Katika kuibua na kuchambua masuala ya
kijinsia, ni vyema sana kuzingatia vipengele vifuatavyo kulingana na sekta
husika (mkazo ni sekta nyeti zinazogusa makundi ya pembezoni). Uibuaji na
uchambuzi ni lazima uzingatie
1. Uchambuzi
wa Masuala ya Kisekta na Mnyambuliko wa Data Kijinsia
Wakati wa kufanya upembuzi yakinifu
(baseline survey) ni muhimu kujiuliza maswali yafuatayo
- Nani
anafanya nini (mgawanyo wa majukumu ya uzalishaji na majukumu ya
kaya)
- Nani
anafikia na kumiliki rasilimali kati ya wanaume na wanawake
- Nani
anafanya maamuzi
- Nani
ananufaika na rasilimali hizi
Hatua hii itakuasaidia kupata data
zenye mnyambuliko wa kijinsia kwa kila swali na inasaidia sana katika kuandaa
sera, mipango na bajeti kwa jicho la kijinsia
Katuni hii imechorwa na Muhidin Msamba, kwa hisani ya TGNP
2.
Kufanya uchambuzi kwa mbinu ya mti wa
matatizo
- Suala
kuu la kijinsia lililoibuliwa
- Visababishi
- Athari
zake
3.
Kufanya uchambuzi wa Wadau na Kubaini
vipaumbele
Ni muhimu baada ya uchakataji wa
taarifa za uwandani, kuweka vipaumbele kwa kuzingatia halihalisi kutoakana na
majibu ya maswali ya vipengele vya hapo juu
Kwa kila kipengele ni muhimu
kubaini waathirika wakuu, wenye ushwishi, watekelezaji wa sera na watunga sera.
Hii itasaidia katika uwajibikaji wakati wa kupanga bajeti yaani kila idara
itenge bajeti kulingana na halihalisi na waathirika wakuu kijinsia na
kimaeneo.
4.
Kufanya uchambuzi wa sera
Ni muhimu baada ya kutoka uwandani
na kubaini masuala na vipaumbele, kufanya uchambuzi wa sera ili kuona ni namna
gani sera inashghulikia kadhia hii. Maswali yafiatayo yakuongoze wakati
unafanya mapition na uchambuzi wa sera.
- Je
sera ipo kushughulika kadhia hii?
- Kama
sera ipo, Je sera ina mapungufu gani?
- Kama
haina maoungufu, je inatekelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na suala bainifu
kuundiwa mikakati na kungizwa kwenye mipango na bajeti ya
Halmashauri?
5. Kuweka Malengo na kuandaa
Mpango wa Utekelezaji (Annual Plans)
Ni vyema kila sekta iweke malengo
kulingana na muda wa utekelezaji ili kushughulikia masuala yaliyoibuliwa kwenye
mchakato wa uibuaji na uchambuzi.
- Malengo
ya muda mfupi (outputs)
- Malengo
ya kati (outcomes)
- Malengo
ya muda mrefu (impact)
Hata hii itakuasaidia kuandaa
mpango kazi kwa mwaka na hata kusaidia katika utoaji wa taarifa. Safu za mpango
huu lazima ziwe na vipengele vya suala la kijinsia, visababishi na athari zake,
walengwa/waathirika wakuu, shughuli zitakazofanyika, viashiria vya utekelezaji,
fungu la fedha lililotengwa, mratibu mkuu na muda wa utekelezaji.
6. Kutenga
Rasilimali kwa kuzingatia Jinsia (Gender Sensitive Resource Allocations)
Kama utazingatia vyema na kwa
weledi na uadilifu hatua zote hapo juu ni rahisi sana kutenga bajeti kijinsia
kwani itakua imebeba mahitaji na vipaumbele vya makundi yote ya jamii
7.
Kufuatilia kujifunza na kutathmini
Utekelezaji
1. UFUATILIAJI
Ufuatiliaji na tathnini wa kisera, mipango,
mikakati na bajeti vinapaswa kuwa na mwitikio wa kijinsia na viashiria mahususi
vya jisia. Ufuatiliaji na tathmini wenye mwelekeo wa kijinsia unapaswa kuwa na
vigezo vifuatavyo:-
a.
Kuwa na malengo na viashiria vya ufuatiliaji
vyenye mrengo wa kijinsia
b.
Kuzingatia ukusanyaji wa data zenye
mnyambuliko wa kijinsia.
c.
Kujumuisha viashiria mahususi kwa ajili ya
uingizaji wa maswala ya kijinsia
d.
Kufuatilia maendeleo kuelekea kukidhi mahitaji
mahususi ya wanaume na wanawake
e.
Kuhakikisha kwamba wanaume na wanawake wana
ushiriki sawa na wanahudumiwa sawa wakichukuliwa kwamba ni watoa maamuzi,
watekelezaji na washiriki.
f.
Kupima matokeo kwa wanaume na wanawake kutoka
hatua ya utekelezaji wa sera/ mpango/mradi.
g.
Kuhakikisha kuwa rasilimali na unufaikaji
vinagawanywa kwa uwiano kwa wanaume na wanawake.
h.
Kufuatilia endapo mpango au shughuli za
mradi zinapunguza tofauti za kijinsia au zinaongeza tofauti za kijinsia.
i.
Kuhakiki maeneo ambapo shughuli zinaongeza
tofauti za kijinsia.
j.
Kuhakikisha kwamba wale walioshiriki kwenye
utekelezaji wa sera/mipango/mradi wana motisha wa kuendeleza mwaswala ya
kijinsia.
k.
Kufuatilia viashiria vya upimaji wa mabadiliko
ya wanawake na wanaume katika mapokeo na uwezo wa kupokea mabadiliko.
l.
Kuweka kumbukumbu ya mifano bora na vipingamizi vinavyojitokeza
kutoka kwenye hatua utekelezaji ambavyo vitashughulikiwa baadae.
8.
Tathmini
Tathmini muhimu kubainisha ni kwa
jinsi gani shughuli zenye mrengo wa kijinsia zimeathiri mapokea na uwezo wa
wanaume na wanawake. Ili kuhakikisha kwamba tathmini inafikia kwa usahihi
matokeo ya kundi husika la wadau/wanufaika, ni muhimu tathmini ikaandaliwa
katika mfumo ulio kwenye mwitikio wa kijinsia. Kwahiyo kwa tathmini ya shughuli
zinazohusiana na sera,mikakati, mipango na bajeti zinapaswa kuwa:-
a.
Kutathmini endapo rasilimali na vinginevyo
vimegawanywa kwa kuzingatia uwiano kati ya wananwake na wanaume.
b.
Kupima endapo mpango wa malengo ya kijinsia
uliowekwa umefikiwa.
c.
Kutathmini ni kwa kiwango gani malengo ya
maendeleo yamefikiwa.
d.
Kutathmini ni kwa jinsi gani matokeo juu ya
uingizwaji wa maswala ya kijinsia yanavyotokea.
e.
Kutathmini kama kulikuwa na matokeo ya kijinsia
yasiyotarajiwa au yasiyokusudiwa.
f.
Kutoa maoni juu ya mambo ya kuzingatia wakati wa
utekelezaji wa mpango ama mradi ujao.
9.
Muundo wa kitaasisi wa ufuatiliaji na
Tathmini
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa ina jukumu la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli
zenye mrengo wa kijinsia kwa Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa hivyo inao
wajibu wa kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mpango huu katika ngazi ya
kitaifa na ngazi ya serikali za mitaa. Katikakutekeleza majukumu yake kama
mratibu wa jumla wa mpango huu, itafanya kazi kwa karibu na Ofisi za Wakuu wa
Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Wizara. Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa pia itafanya kazi na Wizara za ki sekta na wadau
wengine wa maendeleo wa kijinsia ili kupata taarifa ambazo zitahusishwa kwenye
mfumo wa ufuatiliaji na utoaji wa taarifa wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
10.
Kujifunza
Kujifunza ni hatua ya kupata
ufahamu au ujuzi kwa kujifunza, kutenda, kufundishwa,au kupata uzoefu wa jambo
Fulani. Kujifunza ni muhimu katika kupata mambo ambayo yanahitaji shughuli za
kuboresha mbinu, vigezo vya kiutendaji, mpango wa utekelezaji na tathimini.
Kujifunza kuna unganishwa na
ufahamu na mawasiliano ya shughuli kwa jinsi zinavyokusudiwa kuzalishwa,
kupatikana, pamoja na kutoa elimu na kuhakikisha kwamba elimu inayopatikana
inatumika katika kujifunza kwa lengo la:-
i.Kupata na kuchangia elimu
iliyopatikana wakati wa kuandaa na utekelezaji wa OR-TAMISEMI, Serikali za
Mitaa, wadau wa maendeleo, Mpango/mradi na kutolea taarifa kwa ajili ya utoaji
wa maamuzi ili kuongoza na kuboresha shughuli zikiwemo uandaaji wa mipango kwa
matokeo sahihi na halisi.
ii.Kutambua mapungufu ambayo
yanahitaji utafiti wakati wa mtiririko wa matukio ya mradi.
iii.Kuwezesha ushirikishanaji
wa shuhuda ambazo zitawezesha shughuli za mradi kupokea na kutumia mifano ya
mbinu bora.
iv.Kuwezesha utambuzi wa
mapungufu pamoja na fursa za kujifunza
v.Kushirikishana uelewa na
wengine ili kujenga fursa pana kwa ajili ya shughuli za mradi nchini