Monday, July 29, 2024

MAELEKEZO 7 YA SERIKALI KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA




Serikali imetoa maelekezo saba yanayaotakiwa kufaanyiwa kazi kwa dharura nchi nzima ili kuzuia vitendo vya Ukatili wa Kijinsia. 

 Maelekezo hayo yametolewa wakati wa  ziara ya Mawaziri wa kisekta kufuatilia uhai wa Kamati za Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia na kwa Watoto, Mtaa kwa Mtaa (MTAKUWWA), iliyofanyika Manispaa ya Temeke, Jijini Dar es salaam, Julai 27, mwaka huu.

maelekezo hayo ni haya yaliyopo hapa chini:-

1. Kamati za MTAKUWWA ngazi zote zikae vikao vya dharura ndani ya wiki 2 kuanzia tarehe 1 Agosti, 2024 zijadili mikakati.

2. Wajumbe wa Kamati watangazwe wajulikane.

3. Viongozi pacha wachaguliwe Ili ikitokea  mwingiliano wa majukumu kazi za kamati ziendelee. 

4. Taarifa ya mipango na mikakati ya kamati imilikiwe na vikao vyote rasmi ngazi zote.

5. Kila tukio linaloripotiwa, Kamati ifanye kikao cha dharura cha tathmini ya kubaini wapi kulikuwa na mianya Ili wadhibiti.

6. Mikakati ya kuamsha uelewa wa watoto kuhusu kujilinda iandaliwe ikiwemo kwa kutumia michezo, hadith, sanaa, sinema nk.

7. Mijadala ya kijamii ifanyike kwa uratibu wa Dawati la Maendeleo ya Jamii.

Friday, July 19, 2024

RC Singida awafunda wanawake viongozi

 RC Singida awafunda wanawake viongozi

Washiriki wa mafunzo kutoka Mikoa ya Simiyu na Singida, wakishangilia wakati wa Kumpokea Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego. 


Na Deogratius Koyanga, Singida

 MKUU  Mkoa wa Singida, Halima Dendego amewataka wanawake viongozi wanaotoka kwenye vikundi vya kijamii vya uzalishaji na wakulima kujitokeza kwenye kugombea uongozi katika ngazi mbalimbali ili kuchangia kuboresha bajeti na mipango ya serikali za mitaa iweze kuzingatia mahitaji ya kijinsia.

 Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya uongozi na ushiriki wa wanawake kwenye nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo kamati na bodi mbalimbali ngazi za vijiji na kata, yaliyoandaliwa na shirika la Helvetas-Tanzania, chini ya mradi wa Wanawake katika uzalishaji wa ukijani, mjini Singida, Dendego amesema kwamba ni lazima wanawake wajitokeze kuomba nafasi za uongozi katika maeneo yote zaidi ya siasa ili waweze kulinda uoto wa asili, mazingira na kuboresha usalama wa chakula.

 







“ Tunapokuwa na wanawake kwenye nafasi za uongozi jamii inakuwa salama, na sio kwamba wanaume wamefanya makosa au hawafanyi kazi vizuri,  wametuongoza siku nyingi tangu uhuru na mambo mazuri yametokea,  lakini sasa wanahitaji tuwasaidie pia ili  tuungane nao katika kujenga taifa hili na kuleta maendeleo ambayo ni shirikishi.”alisema Dendego.

 

Kwa upande wake, Meneja Mradi wa Ukijani, kutoka Shirika la Helvetas- Tanzania, Shoma Nangale, alisema kwamba   mradi unalenga kujenga uelewa wa washiriki, kupata ujuzi na stadi za kuwezesha kujiandaa na kuwania nafasi za maamuzi na uongozi za kuteuliwa, kuchaguliwa ama kugombea ili waweze kusimamia miradi ya maendeleo, na kuhakikisha masuala ya wanawake yanapata kipaumbele  hasa katika sekta ya mazingira, usalama wa chakula na ulinzi wa rasilimali asilia.

 

Mradi wa Ukijani  unatekelezwa katika Halmashauri tatu za Mkoa wa Singida ambazo ni Manyoni, Iramba na Ikungi na kwa Mkoa wa Simiyu ni Halmashauri za Bariadi Mji, Bariadi DC na Meatu ambapo Zaidi ya wanawake 3,000 wananufaika moja kwa moja na mradi huo. 

Monday, July 1, 2024

Unyago, jando vyachangia utoro shuleni

 Unyago, jando vyachangia utoro shuleni



Na Deogratius Koyanga, Nachingwea

Vitendo vya kupeleka watoto wa kiume na kike kwenye shughuli za jando na unyago vinavyofanywa  na jamii ya Mkoa wa Lindi na viunga vyake vinachangia kwa kiasi kikubwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Hayo yamebainishwa katika mdahalo wa jamii uliowashirikisha wananchi kutoka katika vikundi vya kijamii, wazee wa mila, mangariba na viongozi wa dini katika kata ya Mtuwa, halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi.

Imebainishwa kwamba, vitendo hivyo vinatokana na jamii kutokufuata ratiba ya kufunga na kufungua shule na kuwaingiza watoto wadogo wa shule za msingi kwenye shughuli za kimila za jando na unyago wakati shule zikiendelea na ratiba zake na kupelekea mamia ya wanafunzi kukosa masomo hadi zitakapofanyika sherehe za kuwatoa ndani,

Mdahalo huo, unawashirikisha wananchi  na wadau mbalimbali kama sehemu ya kutekeleza mradi wa uwezeshaji wanawake kushiriki kwenye nafasi za uongozi  na maamuzi na haki ya uchumi, unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili wa Unwomen Tanzania,

Akizungumza wakati wa mjadala huo, mchungaji wa kanisa la wadiventista wasabato, kata ya Mtuwa,Samwel Mang’ati, alisema kwamba wao kama viongozi wa dini wanashauri utaratibu wa kuheshimu ratiba za watoto wa shule ufuatwe ili watoto wote wapate haki ya kupata elimu sambamba na maadili lakini akaonya kuhusu mila hizo kuzingatia maadili na heshima kwa kutumia lugha nzuri zenye staha, kuepuka matusi, kuepuka kufundisha vitu vilivyo nje ya umri wa watoto hao ili kukuza jamii yenye maadili mazuri.

“sisi kama viongozi wa dini tunashauri kuwepo kwa watu maalum, hawa wanaoitwa “warombo” wawe na elimu, wawe ni watu wazima,  walioandaliwa na wawe na elimu maalum ya kufanya kazi hiyo” alisema MchungajI Samwel

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kigango cha Kanisa Katoliki cha Mtuha,Emelius Mkwawa, Alisema kwamba anashauri, utaratibu wa kundesha unyago na jando, uzingatie ratiba za shule ili kutokuwakosesha watoto wa kike na kiume haki ya kupata elimu.

“nashauri, mara tu shule zinapofungwa, hizi shughuli za kimila zianzie hapo hapo, hiyo wiki ya kwanza, shule zinapofunguliwa tuhakikishe hakuna mtoto anabaki kwenye jando au unyago. Wote wawe huru waende shule”alisema na kuongeza:-

“Ninashauri wazazi waache hii tabia kuingia gharama kubwa na kutumia fedha nyingi kwenye sherehe za jando na unyago  lakini kushindwa kuwanunulia watoto hao sare za shule na vifaa vya shule mara shule zinapofunguliwa, unakuta mzazi ananunua nguo za gharama kubwa kwaajili ya shughuli ya unyago au jando, lakini sare za shule hakuna,viatu”

Alisema kwamba, ni vizuri wazazi kuwekeza kwenye elimu, na wanaotoa zawadi kwa watoto wanunue madaftari , kalamu,mabegi ya shule, sare za shule ili kuwafanya watoto walioingia jando kuipenda elimu.

Kwa upande wake Ngariba wa muda mrefu mzee Thomas Ndimbo,  alismea kwamba, taratibu za kutoa vibali vya kuendesha  jando na unyago zinajieleza wazi kwamba, watoto waende jando na unyago wakiwa likizo na wasiwepo kwenye shughuli hizo wakati shule zimefunguliwa na huu ni utaratibu wa mkoa mzima wa Lindi, lakini jamii imekiuka kwa kupanga shughuli hizo wakati mwingine.

“Labda sisi mangariba tukutane, tufanye kikao pamoja na viongozi wa serikali za vijiji vyetu sambamba na jamii ili tukubaliane tena. Asiwepo ngariba anayekubali kupeleka watoto uwanjani, wakati wa shule au wengine akiwa sshuleni” alisema Ndimbo.

Sunday, June 30, 2024

Vijana wataka umri wa unyago,Jando uongezwe

 Vijana wataka umri wa kwenda unyago na Jando uongezwe






Na Deogratius Koyanga, Ruangwa

VIJANA katika kata ya Mandawa, Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi wamependekeza umri wa vijana wa kike na kiume kupelekwa jando na unyago uongezwe kutoka miaka 4 ya sasa iwe  miaka 8 hadi 10 ili kuwa na kundi la vijana waliokomaa wanaoweza kunufaika na mafundisho ya nyango na jando.

Hayo yalisemwa na vijana wakati wa mdahalo wa jamii kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii yaliyoshiriki katika kufanya tathimini ya mafanikio ya midahalo ya nyuma katika mradi wa uwezeshaji wanawake kushiriki kwenye nafasi za uongozi na haki ya uchumi, unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UNwomen).

Unwomen na TGNP, na wadau wengine ikiwepo serikali wanashirikiana katika kujenga uwezo kwa jamii, kubadilisha mila na desturi hasi pamoja na kuboresha mila nzuri zilizopo ili kuwezesha jamii kujikwamua kiuchumi sambamba na  wanawake kushiriki kwenye uongozi na  kufikia usawa wa kijinsia katika Nyanja zote

Akitoa mandekezo ya Vijana kwa niaba ya wengine,Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Mandawa, Zamki Said, alisema kwamba, vijana wanapendekeza kwamba kuwepo na mwongozo unaobainisha umri rasmi wa watoto kwenda jando na unyago, ambao utaanzia angalau miaka 8 hadi 10, ambao watakuwa wameshaanza kukomaa kiakili, na wanaweza kuelewa mafundisho husika na kuyafanyia kazi.

“ …kwa sasa waoto wanaopelekwa jando ni wadogo ,  ni kuanzia miaka mitatu (3) hadi mitano (5) hawa hawawezi hata kuelewa kitu, kila wanachofundishwa kambini wanasahau, wakishatoka kwenye ile sherehe za kutolewa nje, wanakuja kuendelea na maisha huku kijijini, hata hawasalimii tena, utii hakuna, sasa unajiuliza wamejifunza nini? Mbona kijana hana mabadiliko? Jando au unyago imemsaidia nini?, Lakini pia mafundisho baadhi ni ya umri mkubwa lakini wanafundishwa na wakija huku mitaaani wanajaribu yale waliofundishwa ikiwepo ngono katika umri mdogo”alisema

Pia walipendekeza kwamba kuwepo na elimu ya kujitambua, kujitolea , uzalendo, usawa kijinsia, ukatili wa kijinsia ili kuwa na wazazi wazuri wa siku zijazo.

Vijana hao walipendekeza kwamba kuwepo na Makungwi na Manyakanga rasmi wanaotambulika  na watambuliwe na viongozi na serikali ili kuwepo na mfumo mzuri wa elimu inayotolewa na itakayoijenga jamii hasa dhana ya kujitolea kwaajili ya jamii na taifa

Aidha walipendekeza kwamba, kuwepo na  warombo au wasimamizi wa watoto walioko kambinini kwaajili ya unyago na jando ambao watatambuliwa rasmi, na wawe na maadili mazuri  na wasiwe ni watu wanaopatikana kwa utaratibu usio rasmi kwenye jamii.

Akifunga kikao kazi hicho Mtendaji kata wa kata ya Mandawa, halmasahuri ya wilaya ya Ruangwa, Said Ng’itu,  alisema kwamba, uwepo wa TGNP kwenye kata hiyo kumeongeza kwa kiasi kikubwa uelewa wa masuala ya Kijinsia kwani katika kata hiyo  kulianzishwa kituo cha Taarifa na Maarifa ambacho kimeendelea kuchachua masuala ya harakati za usawa wa Kijinsia na kupeleka elimu hiyo katika taasisi mbalimbali ikiwepo kwenye mikutano ya Vijiji.

“ hapa, tulikuwa na changamoto ya Choo cha wasindikizaji wa wazazi wanaojifungua katika Kituo cha Afya, lakini hawa KC waliona hilo kuwa ni tatizo, wameliibua, na wamejitahidi kuhamasisha, sasa choo kinajengwa, ni mafanikio makubwa sisi tumeona nguvu ya jamii wakiamua kuchukua hatua kuboresha mambo yao” alisema  mtendaji.

Friday, June 28, 2024

Jamii yaaswa kuteua ‘mangariba; wanaokubalika wenye maadili

 Jamii yaaswa kuteua ‘mangariba; wanaokubalika wenye maadili





NA Mwandishi wetu, Lindi

Jamii imetakiwa kuteua wataaamu wa kusimamia shughuli za jando na unyago ambao wanaheshimika katika jamii na kukubalika ili kuweka mazingira salama na kutoa elimu nzuri ya makuzi kwa jamii

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Kata ya Mchinga,Wiliam Mwang’onda, katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, wakati akitoa mrejesho kwa viongozi wa dini, mila, viongozi wa vikundi vya kijamii juu ya manafinikio yaliyopatikana kutokana na elimu iliyotolewa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwenye utekelezaji wa Mradi wa Uwezeshaji wanawake kushiriki kwenye uongozi na Maamuzi  na Haki ya uchumi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UNwomen).

Akizungumza kwenye mdahalo wa jamii, uliowashirikisha wananchi kutoka makundi tofauti, kama sehemu ya mwendelezo wa midahalo ya makundi hayo, alisema kwamba, mradi huo umesaidiea kujenga uelwa kwa jamii juu ya kubadilisha mitazamo hasi, mila na desturi hasi, juu ya uwezo wa wananwake kuwa viongozi na pia kumiliki uchumi hasa ardhi na mazao yanayotokana na kilimo.

“tunaendelea kusisitiza na kutoa elimu ili jamii ibadilike. Tunaomba wanaotoa elimu ya jando na unyago wawe ni watu wanaokubalika na jamii, wenye maadili, na ambao wanataswira nzuri ili waweze kuwafundisha vijana wetu mambo mazuri ya makuzi yatakayowawezesha kuwa wazazi wazuri wa kesho kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla na watakaoweza kuzuia na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika jamii” alisema Mwang’onda.

Kwa upande wake mchungaji wa kanisa la wa adiventista Wasabato, Mchinga, Yohana Mwihechi, alisema kwamba wao kama viongozi wa dini, ni washauri wa jamii kuhusu suala la maadili, na wataendeea kutoa elimu katika taasisi zao za dini ili kuwa na jamii inayojali usawa wa Kijinsia na kuheshimu haki na utu wa wengine.

“sisi ni sehemu ya wasimamizi wa madili mema na washauri wa jamii, tutaendelea kusaidiana na serikali katika kutoa elumu kwa jamii juu ya kuacha mila potofu, zinazochangia ukatili wa kijinsia na udhalilishaji, lakini zinazosababisha wanawake kutokumiliki rasilimali kama ardhi”alisema Mchungaji Yohane.

Awali akiwasilisha mafanikio ya mradi huo, mwezeshaji ngazi ya kata ambaye ni afisa Ugani Kata, Abduliazii Ngimbwa, Alisema kwamba baada ya kupatiwa mafunzo na TGNP kuhusu usawa wa Kijinsia, Bajeti yenye mtazamo wa Kijinsia na urasimishaji wa masuala ya KIjinsia kwenye jamii  kwa kushirikiana na maafisa wengine wa Halmashauri wamewezea kutoa elimu hiyo kwenye shule za msingi na sekondari, vikundi vya wanaume na wanawake na kufanikiwa kufikia Zaidi ya watu 3000, katika kata hiyo. 










Monday, June 10, 2024

TGNP,UNFPA wajipanga kutokomeza Ukatili wa Kijinsia Kasulu

 TGNP,UNFPA wajipanga kutokomeza Ukatili wa Kijinsia Kasulu



Na Deogratius Koyanga, Kasulu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirkiana na shirikal la Umoja wa matifa la Idadi ya watu (UNFPA), wameiwezesha jamii inayoishi katika kata za Kumsenga na Murusi katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu, kuanzisha Vituo vya taarifa na Maarifa katika kata zao, ili kuendeleza harakati za kupambana na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika eneo hilo.

Wakiwasilisha mrejesho wa utafiti uliofanywa na wananchi hao kw akuwezeshwa na TGNP na UNFPA, wananchi hao mbele ya Menejimenti ya halmashauri ya Mji wa Kasulu, walisema kwamba:

“… baada ya utafiti huu, na kwa kuongozwa na TGNP, tumeunda kikundi cha kijamii kinachoitwa Kituo cha Taarifa na Maarifa kwenye kila Kata, yaani Kituo cha Taarifa na Maarifa Kumsenga na Kituo cha Taarifa na Maarifa Murusi. Vituo hivi ni mahali ambapo wanajamii wote wa Kata zetu watapata fursa ya kupashana habari na kupeana taarifa mbali mbali juu ya masuala yanayohusu jamii zetu ndani ya mitaa na Kata, na taifa kwa ujumla. Tutashirikiana na viongozi wetu, na jamii nzima kutatua changamoto zinazotukabili, ikiwa ni pamoja na kupambana na ukatili wa kijinsia. Tunaamini kuwa jamii yenye usawa wa kijinsia ni jamii inayojitambua na yenye maendeleo.”

Katika risala hiyo, wameeleza kwamba kwenye mradi huo wa kupambana na ukatili wa kijinsia, TGNP itaendelea kushirikiana na viongozi na wananchi wa Kata ya Kumsenga na Murusi kupitia Vituo hivi vya Taarifa na Maarifa, pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Kasulu Mji.

“..Ndugu Mkurugenzi, sisi kama wazazi na jamii ambayo pia ni sehemu ya waliochangia uwepo wa changamoto tulizozitaja hapo juu, tumeamua kubadilika na kuwa sehemu ya kukemea na kutoa taarifa za wale wanaoendeleza changamoto hizo na hususani ukatili wa kijinsia. Kama jamii tunatakiwa kuacha tabia ya kumaliza mambo hayo kwa siri nyumbani. Tunaomba Polisi na watendaji wa serikali ngazi ya mitaa, kata na wilaya watusaidie kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kupata hukumu stahiki, nasi tutatoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha hilo.

“…., tunatoa shukurani za dhati kwa asasi hii ya TGNP kwa elimu hii; kwani wametufumbua macho na sasa tuko tayari kushirikiana na viongozi wetu katika kuhakikisha jamii yetu inashiriki vema katika kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili. Aidha, tunaahidi kujenga jamii inayothamini utu wa kila mtu.” Walisema washiriki hao ambao ni waanzilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa hivyo vipya.

Baada ya kunzishwa kwa Vituo hivyo, TGNP sasa inakuwa na Vituo vya Taarifa na Maarifa tisa (7) katika halmasahuri hivyi vikiwemo , Nyansha, Murufiti, Kigondo, Muganza, Kigondo, Ruhita na Kumsenga.






 

TGNP na UNFPA wanzisha Vituo vya Taarifa na Maarifa Kasulu

 TGNP  na UNFPA wanzisha Vituo vya Taarifa na Maarifa Kasulu






Na Deogratius Koyanga,Kasulu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana  na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA), wameunda Vituo vya taarifa na Maarifa kwenye Kata mbili za Kumsenga na Murusi, katika halmashairi ya Mji wa Kasulu

Kuunadwa kwa vituo  vya taarifa na Maarifa (KCs) katika Halmashauri hiyo kumefuatiwa na zoezi la utafiti shirikishi wa kiraghibish (PAR), ambao ulifanywa na TGNP kama sehemu ya Utekelezaaji unaotekelezwa na UNFPA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Kasulu na TGNP kwa lengo la kutokomeza Ukatili wa Kijinsia katika jamii ya Kasulu.

Kituo cha Taarifa na Maarifa kinachoundwa na TGNP ni sehemu ya kujenga na kuimarisha ujenzi wa nguu ya pamoja katika kusimamia harakati za kutokomeza vitnedo vya Ukatili wa Kijinsia. Katika jamii na kusimamia utekelezaji wa mipango kazi iliyoibuliwa wakati wa zoezi la uraghibish.

Tangu mwaka 2018, TGNP imekuwa ikifanya kazi katika halmasahguri hiyo na kuanzisha Vituo hivyo ambavyo vimeweza kufanya kazi kubwa ya uhamasishaji kwa wananchi kushiriki shughuli za maendeleo na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.

Vituo vya Taarifa na Maarifa vlivyoanzishwa mwishoni mwa wiki katika kata hizi mbili vinaenda kuunganisha nguvu na vingine ambavyo TGNP ilishaanzisha katika halmashauri hiyo, ambavyo ni Kata za Kigondo, Murufiti, Nyansha, Mganza. 

Saturday, June 8, 2024

Wananchi Kasulu, wataja maeneo hatarishi kwa Ukatili wa Kijinsia

 Wananchi Kasulu, wataja  maeneo hatarishi kwa Ukatili wa Kijinsia


Mwananchi wa Kata ya Kumsenga, akipanga mawe kama sehemu ya kubainisha sehemu hatarishi ambako kuna vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika Kata hiyo. Zoezi hili ni mbinu moja wapo ambayo hutumika wakati wa Utafiti shirikishi (Participatory Action Research).washiriki huwezeshwa kutumia mbinu za U-3 [Uibuaji, uchambuzi na Utatuzi]


Na Deogratius Koyanga, Kasulu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Maataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), wamewawezesha wananchi kutoka kata mbili za Kumsenga na Murusi, katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu, kutambua, kuibua na kuainisha maeneo hatarishi ambapo vitendo vya Ukatili wa Kijinsia vinafanyika na kusababisha kutokea kwa mimba za utotoni.

Hayo yameibuliwa wkaati wa mrejesho wa zoezi la utafiti shirikishi (PAR) liliofanyika katika Halmashauri hiyo, kama sehemu ya utekelezaji wa mradi wa TGNP na UNFPA unaolenga kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma.

Maeneo yaliyotajwa kuwa yanasababisha uwepo wa mimba za utotoni ni pamoja na; Masoko ya usiku ambayo husababisha ngono zembe bila kuangalia rika. Mfano,  Soko la CCM lililoko mtaa wa Omar, Soko Kuu lililoko mtaa wa Ikulu mjini na soko la kwa Shayo lililopo kata ya Murusi,  Masoko haya yanaanza saa kumi jioni na kumalizika kati ya saa nne hadi sita usiku.

“Wazazi kwenda kulima mashamba ya mbali na kuwaacha watoto peke yao majumbani, hali hii hupelekea watoto wakubwa kwenye familia hizi kuhemea kwa ajili ya wadogo zao, hivyo kulazimika kushiriki ngono ili kukidhi mahitaji ya familia zao” imeeleza sehemu ya risala ya wananchi iliyossomwa kwa Mkurugenzi wa Halmasahuri ya mji wa Kasulu.







Friday, June 7, 2024

TGNP na UNFPA wawezesha jamii kuibua vitendo vya Ukatili wa Kijinsia Kasulu

 TGNP na UNFPA wawezesha jamii  kuibua vitendo vya Ukatili wa Kijinsia  Kasulu


Washiriki katika hafla ya kutoa mrejesho wa Utafiti Shirikishi (Participatory Action Research) kutoka kata za Kumsenga na Murusi, Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Kigoma, Utafiti huo umewezeshwa na TGNP na UNFPA ili kutokomeza Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia 



Na Deogratius Koyanga, Kasulu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  wamefanya mrejesho wa Utafiti raghibishi (Participatory Action Research [PAR]) uliofanyika katika kata ya Mrusi na Kumesenga, Halmasahuri ya Kasulu Mji.

Utafiri shirikishi huo ni sehemu ya mradi wa kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia unaotekelezwa na TGNP na Shirikla la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA), unaotekelezwa katika wilaya ya Kasulu chini ya program ya Pamoja ya Mashirika ya Umoja wa Kimataifa

Katika wasilisho lao, washiriki wa PAR katika Halimashauri ya Kasulu Mji, walisema kwamba kupitia mchakato wa PAR uliowezeshwa na TGNP kwa kutumia mbinu za U-3 za Uibuaji, Uchambuzi na Utekelezaji, wameweza kuibua sababu za kina za kushamiri kwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto katika eneo hilo na kubaini njia za utatuzi wake ambazo kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi za serikali za mitaa na wilaya watashirkiana na kuhakikisha vinakoma.

“Tumeona jinsi ambavyo kata zetu hizo, mbili zimeadhirika na vitendo vya ubakaii, ulawiti na mimba za utotoni, hatutaki hali hii iendelee, tutahakikisha sasa kwa kushirkiana na viongozi wetu tunazuia kabisa kwa kushirikiana na viongozi wetu.”alisema Beatrice Christopha msomaji wa risala mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri.

“Tumejifunza pia kuwahusisha viongozi wetu kama madiwani na watendaji wote wa serikali tulio nao katika ngazi ya mitaa, kata na wilaya ili kupata ufumbuzi wa changamoto zilizo nje ya uwezo wetu sisi kama wananchi. Katika mchakato huu wa siku sita, tulijadili kwa kina, tulichambua kwa kina na tuliweza kuibua changamoto mbalimbali ndani ya Kata zetu” alisema  Beatrice

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mabena Paschalina, alisema kwamba kazi iliyofanywa na TGNP ni kubwa kuwajengea uwezo wananchi hao uwezo na kujitambua na kuamua kuchukua hatua za changamoto za kukidhiri kwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia.

“Nyie mliojengewa uwezo na TGNP ni wazazi lakini pia mnaishi miongoni mwa jamii, ambako vitendo vya Ukatili vinatokea, ninawataka sasa tuchukue hatua, tupite kwenye mikutano, vikao, majukwaa, kwenye taasisi za dini, shuleni nk. Kuhakikisha ujumbe unawafikia watu wazima lakini pia na watoto” alisema

Kaimu Mkurugenzi amesema kwamba, Halmasahuri itaendelea kutoa ushirkiano kwa wadau kama TGNP na UNFPA katika kutekeleza afua za usawa wa Kijinsia, sambamba na kuhakikisha kwamba jamii inabadilika kimtazamo na kitabia kwa kusimamia vizuri sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kuwepo na haki na usawa.

Ameongeza kwamba, halmashauri kwa kushirikiana na vyombo vingine, itahakikisha  kwamba wananchi wote wanakuwa salama, hawafanyiwi vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ili waweze kunufaika na fursa zilizopo na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya Tanzania kuwezesha wananchi kiuchumi. 

Kikao hicho cha mrejesho kilihudhuriwa pia na wakuu wa idara na Vitengo wa Halmasahuri pamoja na Mkuu wa dawati la Jinsia -Polisi Kasulu, ambao walipata nafasi ya kujibu baadhi ya masuala yaliyoibuliwa ambayo yapo chini ya maeneo yao ya kiutendaji.

wengine waliohudhuria ni watendaji kata mbili za Kumsenga na Murusi, Madiwani wa kata  na viti maalum na Maafisa Maendeleo ya jamii wa kata husika.
















Wednesday, June 5, 2024

Vitendo vya Ubakaji, ulawiti kero Kasulu

 Vitendo vya Ubakaji, ulawiti kero Kasulu


Washiriki wa Utafiti shirikishi wa Kiraghibish (participatory Action Research-PAR) kutoka kata ya Murusi, Kasulu Mjini, walijadiliana, kuchambua na kubaini sababu za kushamiri kwa vitendo vya Ubakaji katika eneo hilo. PAR ni shughuli inayotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA katika Halmashauri hiyo.


 Na Deogratius  Koyanga, Kasulu

Wananchi wa kata ya Murusi, Halmashuri ya Mji wa Kasulu, mkoani Kigoma, wamesikitishwa na kushamiri kwa vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto.

Sababu zilizoibuliwa na wananchi hao, wakati wa zoezi la uraghibish  shirikishi (Participatory Action Research –PAR) ulioendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA),  ni pamoja na Imani za kishirikina ambao hupelekea vitendo vya ulawiti kwa wanaume na ubakaji kwa wanawake na wasichana unaosababishwa na tamaa ya mali.

Aidha, sababu nyingine iliyoibuliwa ni unywaji wa pombe kupita kiasi kwa wazazi na kupelekea watoto kukulia vilabuni, na hivyo kukosa malezi stahiki. Pia unywaji pombe kupitiliza husababisha watu kubakwa au kubaka.

“hapa kwentu kuna tatizo la watu kudanyangwa na waganga wa kienyeji kuwa ili wapate utajiri wabake watoto wao. Mfano baba kubaka binti ili apate utajiri, na wanafamilia wengine kukaa kimya/kuyamaliza kifamilia” wamesema washiriki hao

Pia imeonekana kwamba, kuna vitendo vya Ubakaji kwa watu wanaoishi na ulemavu – mfano wagonjwa wa akili hadi kupewa mimba.