Serikali imetoa maelekezo saba yanayaotakiwa kufaanyiwa kazi kwa dharura nchi nzima ili kuzuia vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.
Maelekezo hayo yametolewa wakati wa ziara ya Mawaziri wa kisekta kufuatilia uhai wa Kamati za Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia na kwa Watoto, Mtaa kwa Mtaa (MTAKUWWA), iliyofanyika Manispaa ya Temeke, Jijini Dar es salaam, Julai 27, mwaka huu.
maelekezo hayo ni haya yaliyopo hapa chini:-
1. Kamati za MTAKUWWA ngazi zote zikae vikao vya dharura ndani ya wiki 2 kuanzia tarehe 1 Agosti, 2024 zijadili mikakati.
2. Wajumbe wa Kamati watangazwe wajulikane.
3. Viongozi pacha wachaguliwe Ili ikitokea mwingiliano wa majukumu kazi za kamati ziendelee.
4. Taarifa ya mipango na mikakati ya kamati imilikiwe na vikao vyote rasmi ngazi zote.
5. Kila tukio linaloripotiwa, Kamati ifanye kikao cha dharura cha tathmini ya kubaini wapi kulikuwa na mianya Ili wadhibiti.
6. Mikakati ya kuamsha uelewa wa watoto kuhusu kujilinda iandaliwe ikiwemo kwa kutumia michezo, hadith, sanaa, sinema nk.
7. Mijadala ya kijamii ifanyike kwa uratibu wa Dawati la Maendeleo ya Jamii.
No comments:
Post a Comment