Monday, June 10, 2024

TGNP,UNFPA wajipanga kutokomeza Ukatili wa Kijinsia Kasulu

 TGNP,UNFPA wajipanga kutokomeza Ukatili wa Kijinsia Kasulu



Na Deogratius Koyanga, Kasulu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirkiana na shirikal la Umoja wa matifa la Idadi ya watu (UNFPA), wameiwezesha jamii inayoishi katika kata za Kumsenga na Murusi katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu, kuanzisha Vituo vya taarifa na Maarifa katika kata zao, ili kuendeleza harakati za kupambana na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika eneo hilo.

Wakiwasilisha mrejesho wa utafiti uliofanywa na wananchi hao kw akuwezeshwa na TGNP na UNFPA, wananchi hao mbele ya Menejimenti ya halmashauri ya Mji wa Kasulu, walisema kwamba:

“… baada ya utafiti huu, na kwa kuongozwa na TGNP, tumeunda kikundi cha kijamii kinachoitwa Kituo cha Taarifa na Maarifa kwenye kila Kata, yaani Kituo cha Taarifa na Maarifa Kumsenga na Kituo cha Taarifa na Maarifa Murusi. Vituo hivi ni mahali ambapo wanajamii wote wa Kata zetu watapata fursa ya kupashana habari na kupeana taarifa mbali mbali juu ya masuala yanayohusu jamii zetu ndani ya mitaa na Kata, na taifa kwa ujumla. Tutashirikiana na viongozi wetu, na jamii nzima kutatua changamoto zinazotukabili, ikiwa ni pamoja na kupambana na ukatili wa kijinsia. Tunaamini kuwa jamii yenye usawa wa kijinsia ni jamii inayojitambua na yenye maendeleo.”

Katika risala hiyo, wameeleza kwamba kwenye mradi huo wa kupambana na ukatili wa kijinsia, TGNP itaendelea kushirikiana na viongozi na wananchi wa Kata ya Kumsenga na Murusi kupitia Vituo hivi vya Taarifa na Maarifa, pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Kasulu Mji.

“..Ndugu Mkurugenzi, sisi kama wazazi na jamii ambayo pia ni sehemu ya waliochangia uwepo wa changamoto tulizozitaja hapo juu, tumeamua kubadilika na kuwa sehemu ya kukemea na kutoa taarifa za wale wanaoendeleza changamoto hizo na hususani ukatili wa kijinsia. Kama jamii tunatakiwa kuacha tabia ya kumaliza mambo hayo kwa siri nyumbani. Tunaomba Polisi na watendaji wa serikali ngazi ya mitaa, kata na wilaya watusaidie kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kupata hukumu stahiki, nasi tutatoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha hilo.

“…., tunatoa shukurani za dhati kwa asasi hii ya TGNP kwa elimu hii; kwani wametufumbua macho na sasa tuko tayari kushirikiana na viongozi wetu katika kuhakikisha jamii yetu inashiriki vema katika kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili. Aidha, tunaahidi kujenga jamii inayothamini utu wa kila mtu.” Walisema washiriki hao ambao ni waanzilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa hivyo vipya.

Baada ya kunzishwa kwa Vituo hivyo, TGNP sasa inakuwa na Vituo vya Taarifa na Maarifa tisa (7) katika halmasahuri hivyi vikiwemo , Nyansha, Murufiti, Kigondo, Muganza, Kigondo, Ruhita na Kumsenga.






 

No comments:

Post a Comment