Vitendo vya Ubakaji, ulawiti kero Kasulu
Na Deogratius
Koyanga, Kasulu
Wananchi wa kata ya
Murusi, Halmashuri ya Mji wa Kasulu, mkoani Kigoma, wamesikitishwa na kushamiri
kwa vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto.
Sababu zilizoibuliwa na wananchi hao, wakati wa zoezi la
uraghibish shirikishi (Participatory
Action Research –PAR) ulioendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa
kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu
(UNFPA), ni pamoja na Imani za
kishirikina ambao hupelekea vitendo vya ulawiti kwa wanaume na ubakaji kwa
wanawake na wasichana unaosababishwa na tamaa ya mali.
Aidha, sababu nyingine iliyoibuliwa ni unywaji wa pombe
kupita kiasi kwa wazazi na kupelekea watoto kukulia vilabuni, na hivyo kukosa
malezi stahiki. Pia unywaji pombe kupitiliza husababisha watu kubakwa au
kubaka.
“hapa kwentu kuna tatizo la watu kudanyangwa na waganga wa
kienyeji kuwa ili wapate utajiri wabake watoto wao. Mfano baba kubaka binti ili
apate utajiri, na wanafamilia wengine kukaa kimya/kuyamaliza kifamilia”
wamesema washiriki hao
Pia imeonekana kwamba, kuna vitendo vya Ubakaji kwa watu wanaoishi
na ulemavu – mfano wagonjwa wa akili hadi kupewa mimba.
No comments:
Post a Comment