TGNP na UNFPA wanzisha Vituo vya Taarifa na Maarifa Kasulu
Na Deogratius
Koyanga,Kasulu
Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA), wameunda
Vituo vya taarifa na Maarifa kwenye Kata mbili za Kumsenga na Murusi, katika
halmashairi ya Mji wa Kasulu
Kuunadwa kwa
vituo vya taarifa na Maarifa (KCs)
katika Halmashauri hiyo kumefuatiwa na zoezi la utafiti shirikishi wa kiraghibish
(PAR), ambao ulifanywa na TGNP kama sehemu ya Utekelezaaji unaotekelezwa na
UNFPA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Kasulu na TGNP kwa lengo la
kutokomeza Ukatili wa Kijinsia katika jamii ya Kasulu.
Kituo cha Taarifa na
Maarifa kinachoundwa na TGNP ni sehemu ya kujenga na kuimarisha ujenzi wa nguu
ya pamoja katika kusimamia harakati za kutokomeza vitnedo vya Ukatili wa
Kijinsia. Katika jamii na kusimamia utekelezaji wa mipango kazi iliyoibuliwa
wakati wa zoezi la uraghibish.
Tangu mwaka 2018,
TGNP imekuwa ikifanya kazi katika halmasahguri hiyo na kuanzisha Vituo hivyo
ambavyo vimeweza kufanya kazi kubwa ya uhamasishaji kwa wananchi kushiriki
shughuli za maendeleo na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.
Vituo vya Taarifa na
Maarifa vlivyoanzishwa mwishoni mwa wiki katika kata hizi mbili vinaenda
kuunganisha nguvu na vingine ambavyo TGNP ilishaanzisha katika halmashauri
hiyo, ambavyo ni Kata za Kigondo, Murufiti, Nyansha, Mganza.




No comments:
Post a Comment