TGNP na UNFPA wawezesha jamii kuibua vitendo vya Ukatili wa Kijinsia Kasulu
Na Deogratius Koyanga, Kasulu
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wamefanya mrejesho wa Utafiti raghibishi (Participatory
Action Research [PAR]) uliofanyika katika kata ya Mrusi na Kumesenga,
Halmasahuri ya Kasulu Mji.
Utafiri shirikishi huo ni sehemu
ya mradi wa kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia unaotekelezwa na TGNP na
Shirikla la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA),
unaotekelezwa katika wilaya ya Kasulu chini ya program ya Pamoja ya Mashirika
ya Umoja wa Kimataifa
Katika wasilisho lao, washiriki
wa PAR katika Halimashauri ya Kasulu Mji, walisema kwamba kupitia mchakato wa
PAR uliowezeshwa na TGNP kwa kutumia mbinu za U-3 za Uibuaji, Uchambuzi na
Utekelezaji, wameweza kuibua sababu za kina za kushamiri kwa vitendo vya
Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto katika eneo hilo na kubaini njia za
utatuzi wake ambazo kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi za serikali za mitaa
na wilaya watashirkiana na kuhakikisha vinakoma.
“Tumeona jinsi ambavyo kata zetu
hizo, mbili zimeadhirika na vitendo vya ubakaii, ulawiti na mimba za utotoni,
hatutaki hali hii iendelee, tutahakikisha sasa kwa kushirkiana na viongozi wetu
tunazuia kabisa kwa kushirikiana na viongozi wetu.”alisema Beatrice Christopha msomaji
wa risala mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri.
“Tumejifunza
pia kuwahusisha viongozi wetu kama madiwani na watendaji wote wa serikali tulio
nao katika ngazi ya mitaa, kata na wilaya ili kupata ufumbuzi wa changamoto
zilizo nje ya uwezo wetu sisi kama wananchi. Katika mchakato huu wa siku sita,
tulijadili kwa kina, tulichambua kwa kina na tuliweza kuibua changamoto
mbalimbali ndani ya Kata zetu” alisema Beatrice
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mabena Paschalina, alisema
kwamba kazi iliyofanywa na TGNP ni kubwa kuwajengea uwezo wananchi hao uwezo na
kujitambua na kuamua kuchukua hatua za changamoto za kukidhiri kwa vitendo vya
ukatili wa Kijinsia.
“Nyie
mliojengewa uwezo na TGNP ni wazazi lakini pia mnaishi miongoni mwa jamii,
ambako vitendo vya Ukatili vinatokea, ninawataka sasa tuchukue hatua, tupite
kwenye mikutano, vikao, majukwaa, kwenye taasisi za dini, shuleni nk. Kuhakikisha
ujumbe unawafikia watu wazima lakini pia na watoto” alisema
Kaimu
Mkurugenzi amesema kwamba, Halmasahuri itaendelea kutoa ushirkiano kwa wadau
kama TGNP na UNFPA katika kutekeleza afua za usawa wa Kijinsia, sambamba na kuhakikisha
kwamba jamii inabadilika kimtazamo na kitabia kwa kusimamia vizuri sheria,
kanuni na taratibu za nchi ili kuwepo na haki na usawa.
Ameongeza
kwamba, halmashauri kwa kushirikiana na vyombo vingine, itahakikisha kwamba wananchi wote wanakuwa salama,
hawafanyiwi vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ili waweze kunufaika na fursa
zilizopo na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya Tanzania kuwezesha wananchi
kiuchumi.
Kikao hicho cha mrejesho kilihudhuriwa pia na wakuu wa idara na Vitengo wa Halmasahuri pamoja na Mkuu wa dawati la Jinsia -Polisi Kasulu, ambao walipata nafasi ya kujibu baadhi ya masuala yaliyoibuliwa ambayo yapo chini ya maeneo yao ya kiutendaji.
wengine waliohudhuria ni watendaji kata mbili za Kumsenga na Murusi, Madiwani wa kata na viti maalum na Maafisa Maendeleo ya jamii wa kata husika.















No comments:
Post a Comment