MSAMAHA NI NINI?
Msamaha ni uamuzi wa kuachilia hisia
za hasira, chuki, na chuki dhidi ya mtu aliyekuumiza. Ni kuchagua kutokubali
kwamba kosa la mtu huyo litakuwa na nguvu juu ya maisha yako, ni kuchagua
kutokuendelea kutazama nyuma ambako mtu alikutendea uovu au kukwamisha
mafanikio yako.
Msamaha ni kitendo cha kuacha kuudhika, kuachilia mtu aliyekukosea,
na kuamua kutochukua kisasi. Ni uamuzi wa kuachilia maumivu ya moyo na hasira
ambayo yamesababishwa na matendo ya mtu mwingine. Msamaha sio tu unawafungulia
wengine, bali pia unawafungulia yule anayesamehe kutoka katika minyororo ya
chuki na uchungu.
KWANINI TUNALAZIMIKA KUSAMEHE?
Ukibeba glasi au vikombe vya udongo
kwenye kapu au mfuko ni lazima vigongane, kukwaruzana, kusuguana, na vingine
kupasuka. Vikombe vinafanana sana na mfumo wetu wa maisha. Maisha ya binadamu
yamejengwa kwenye harakati za kukutana, kuhusiana na kufanya kazi kwa pamoja,
kufurahi pamoja, kuhuzunika pamoja nk. Katika harakati hizo, ndipo zinatokea
hitilafu na migongano na migogoro ambapo inasabaisha makasiriko, chuki, hasira
na kukoseana. Sasa basi, baada ya kukutana na hali hii, msamaha una maana gani
kwetu?
- Msamaha sio kusahau kwamba mtu alikukosea. Ni kukubali
kwamba tukio hilo limetokea na kuchagua kuachilia maumivu yanayosababishwa
nalo.
- Msamaha hasa unakuhusu wewe. Ni njia ya kuponya na
kusonga mbele.
- Msamaha sio tukio la wakati mmoja. Ni mchakato ambao
unaweza kuchukua muda. Wakati Fulani huchukua miezi, miaka nk.
- Kusamehe haimaanishi kwamba unakubali tabia mbaya ya
mtu mwingine.
- Kusamehe kunaweza kuwa nguvu ya kubadilisha maisha.
Inaweza kukusaidia kupata amani ya akili na uhusiano bora na wengine.
Msamaha ni zawadi unayojipatia
mwenyewe
Ikiwa unakabiliwa na ugumu wa
kusamehe, unaweza kutaka kuzungumza na mshauri,mshauri wa kiroho, mchungaji, padre, Imam /mwalimu wa dini au
mtaalamu wa afya ya akili. Wanaweza kukusaidia katika mchakato wa kupona. Hali
hii inasaidia kukufanya utoke kwenye kifungo cha kubeba mzigo wa watu.
Umuhimu wa Kusamehe Watu
Waliotukosea
Kusamehe ni zawadi kubwa
tunayojipatia wenyewe. Inaweza kuwa vigumu sana, hasa pale tulipojeruhiwa sana.
Lakini faida zake ni nyingi sana na zinaboreshesha maisha yetu kwa njia nyingi.
Unaposamehe unatua mzigo, lakini unajipa furaha na Amani. Unaposamehe unaongeza
fursa za kufanikiwa Zaidi, unapata Baraka kutoka kwa Mungu, “Utusamehe sisi,
kama tulivyowasamehe wengine” ukisamehe unakuwa na afya njema, unapata nguvu za
kuzalisha Zaidi kipato, kipato chako kinaongezeka mara dufu. Ukisamehe unakuwa
na uwezo wa kuwasilisiliana vizuri na wateja wako na kuongeza uwezo wa kuuza na
kununua na kujitengenezea uchumi bora. Msamaha una mafanikio makubw akw
aliyeumizwa na kudsamehe kuliko aliyekosa.
Kwa nini ni muhimu kusamehe?
- Chuki na hasira zinaweza kuleta mzigo mzito moyoni.
Kusamehe ni kama kuondoa mzigo huo na kupata amani ya akili.
- Kusamehe kunaweza kuboresha uhusiano wetu na wengine,
hata na wale waliotutenda mabaya.
- Uchungu wa kutokusamehe unaweza kuathiri afya yetu ya
kimwili na kiakili, ukisababisha matatizo kama vile usingizi mbovu, mkazo,
na hata magonjwa.
- Katika dini nyingi, kusamehe ni sehemu muhimu ya ukuaji
wa kiroho. Inatuunganisha zaidi na Mungu au nguvu ya juu zaidi. Mfano
wakatoliki wanaashwa kusamehe kabla ya kupokea Ekaristi, lakini pia kabla
ya kutoa sadaka yako, nenda kapatane na ndugu yako.
- Tunaposamehe, tunaonyesha wengine jinsi ya
kushughulikia maumivu na kuchagua upendo badala ya chuki. Ukisamehe
unaongeza ufanisi katika shughuli zako za kila siku, uhuru wa akili na
nafsi, unakupa nguvu mpya na ubunifu katika utendaji
Jinsi ya kusamehe:
Kusamehe si jambo rahisi, lakini
kuna hatua unaweza kuchukua:
- Elewa hisia zako na kwa nini umejerahiwa.
- Kushiriki hisia zako na mtu unayemwamini kunaweza
kukusaidia kupata mtazamo mpya.
- Kuandika juu ya hisia zako kunaweza kukusaidia
kuzipanga vizuri.
- Ikiwa unaamini katika Mungu, omba nguvu ya kusamehe.
- Kila mtu hufanya makosa.
Kumbuka: Kusamehe sio sawa na kusahau. Ni juu ya kuchagua kuachilia
maumivu na kusonga mbele.
Maandiko
Matakatifu Yanasemaje Kuhusu Msamaha?
Maandiko Matakatifu, hususan Biblia,
yanasisitiza sana umuhimu wa msamaha. Yesu Kristo, katika mahubiri yake
Mlimani, alisisitiza kwamba tunapaswa kusamehe wale wanaotukosea, kama vile
Baba yetu wa mbinguni anavyotusamehe sisi (Mathayo 6:14-15).
- Mathayo 6:14-15:
“Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni
atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu
hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
- Marko 11:25-26:
“Nanyi kila msimamapo na kusali, sameheni mkiwa na neno juu ya mtu, ili na
Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini
msipowasamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa
yenu.”
No comments:
Post a Comment