Wananchi Kasulu, wataja maeneo hatarishi kwa Ukatili wa Kijinsia
Na Deogratius Koyanga,
Kasulu
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), kwa kushirikiana
na Shirika la Umoja wa Maataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), wamewawezesha
wananchi kutoka kata mbili za Kumsenga na Murusi, katika Halmashauri ya Mji wa
Kasulu, kutambua, kuibua na kuainisha maeneo hatarishi ambapo vitendo vya
Ukatili wa Kijinsia vinafanyika na kusababisha kutokea kwa mimba za utotoni.
Hayo yameibuliwa wkaati wa mrejesho wa zoezi la
utafiti shirikishi (PAR) liliofanyika katika Halmashauri hiyo, kama sehemu ya
utekelezaji wa mradi wa TGNP na UNFPA unaolenga kutokomeza vitendo vya Ukatili
wa Kijinsia katika wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma.
Maeneo yaliyotajwa kuwa yanasababisha uwepo wa mimba
za utotoni ni pamoja na; Masoko ya usiku ambayo husababisha ngono zembe bila
kuangalia rika. Mfano, Soko la CCM
lililoko mtaa wa Omar, Soko Kuu lililoko mtaa wa Ikulu mjini na soko la kwa
Shayo lililopo kata ya Murusi, Masoko
haya yanaanza saa kumi jioni na kumalizika kati ya saa nne hadi sita usiku.
“Wazazi kwenda kulima mashamba ya mbali na kuwaacha
watoto peke yao majumbani, hali hii hupelekea watoto wakubwa kwenye familia
hizi kuhemea kwa ajili ya wadogo zao, hivyo kulazimika kushiriki ngono ili
kukidhi mahitaji ya familia zao” imeeleza sehemu ya risala ya wananchi
iliyossomwa kwa Mkurugenzi wa Halmasahuri ya mji wa Kasulu.






No comments:
Post a Comment