Jamii yaaswa kuteua ‘mangariba; wanaokubalika wenye maadili
NA Mwandishi wetu, Lindi
Jamii imetakiwa kuteua wataaamu
wa kusimamia shughuli za jando na unyago ambao wanaheshimika katika jamii na
kukubalika ili kuweka mazingira salama na kutoa elimu nzuri ya makuzi kwa jamii
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji
Kata ya Mchinga,Wiliam Mwang’onda, katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,
wakati akitoa mrejesho kwa viongozi wa dini, mila, viongozi wa vikundi vya
kijamii juu ya manafinikio yaliyopatikana kutokana na elimu iliyotolewa na
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwenye utekelezaji wa Mradi wa Uwezeshaji
wanawake kushiriki kwenye uongozi na Maamuzi
na Haki ya uchumi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
masuala ya wanawake (UNwomen).
Akizungumza kwenye mdahalo wa
jamii, uliowashirikisha wananchi kutoka makundi tofauti, kama sehemu ya mwendelezo
wa midahalo ya makundi hayo, alisema kwamba, mradi huo umesaidiea kujenga uelwa
kwa jamii juu ya kubadilisha mitazamo hasi, mila na desturi hasi, juu ya uwezo
wa wananwake kuwa viongozi na pia kumiliki uchumi hasa ardhi na mazao
yanayotokana na kilimo.
“tunaendelea kusisitiza na kutoa
elimu ili jamii ibadilike. Tunaomba wanaotoa elimu ya jando na unyago wawe ni
watu wanaokubalika na jamii, wenye maadili, na ambao wanataswira nzuri ili
waweze kuwafundisha vijana wetu mambo mazuri ya makuzi yatakayowawezesha kuwa
wazazi wazuri wa kesho kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla na watakaoweza
kuzuia na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika jamii” alisema Mwang’onda.
Kwa upande wake mchungaji wa kanisa
la wa adiventista Wasabato, Mchinga, Yohana Mwihechi, alisema kwamba wao kama
viongozi wa dini, ni washauri wa jamii kuhusu suala la maadili, na wataendeea
kutoa elimu katika taasisi zao za dini ili kuwa na jamii inayojali usawa wa
Kijinsia na kuheshimu haki na utu wa wengine.
“sisi ni sehemu ya wasimamizi wa
madili mema na washauri wa jamii, tutaendelea kusaidiana na serikali katika
kutoa elumu kwa jamii juu ya kuacha mila potofu, zinazochangia ukatili wa
kijinsia na udhalilishaji, lakini zinazosababisha wanawake kutokumiliki
rasilimali kama ardhi”alisema Mchungaji Yohane.
Awali akiwasilisha mafanikio ya
mradi huo, mwezeshaji ngazi ya kata ambaye ni afisa Ugani Kata, Abduliazii
Ngimbwa, Alisema kwamba baada ya kupatiwa mafunzo na TGNP kuhusu usawa wa
Kijinsia, Bajeti yenye mtazamo wa Kijinsia na urasimishaji wa masuala ya
KIjinsia kwenye jamii kwa kushirikiana
na maafisa wengine wa Halmashauri wamewezea kutoa elimu hiyo kwenye shule za
msingi na sekondari, vikundi vya wanaume na wanawake na kufanikiwa kufikia Zaidi
ya watu 3000, katika kata hiyo.









No comments:
Post a Comment