Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande, akizungumza wakati wa hotuba yake kwenye Kongamano la Miaka 30 ya Beijing, lililoandaliwa na Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uongozi na Uchaguzi |
Na Deogratius Koyanga
Wizara ambazo hazitatenga Bajeti yenye mtazamo wa Kijinsia, zitatakiwa kutopewa fedha hadi zitakapozingatia mahitaji ya msingi ya makundi yote wakiwepo wanawake, wanaume, wazee watoto, wasichana na watu wenye ulemavu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mfuko wa ruzuku kwa wanawake
(WFT-T) Profesa Penina Mlama mbele ya Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande, Wakati wa maadhimisho ya sherehe za Miaka 30
ya Beijing, na siku ya wanawake Duniani, zilizoandaliwa na Mtandao wa wanawake, Katiba,
Uongozi na uchaguzi chini ya uratibu wa WFT-T.
“Mhe. Naibu Waziri, tunaishukuru serikali, wakati tumeenda
Beijing miaka 30 iliyopita, tuliaambatana na viongozi wa serikali, watumishi wa
wizara mbalimbali na wawakilishi wa sekta. Hawa waliwezeshwa na wizara ya
fedha. Masuala ya Beijing ambayo yametekelezwa hapa Tanzania, yametumia bajeti
na fedha za serikali ambazo zinatoka katika wizara yako. Tunaona jinsi wizara
ya fedha imewajibika kusimamia utekelezaji wa maamzimio ya Beijing” alisema
Profesa Mlama na kuongeza:
“Tunakuomba kwa nafasi ya wizara hii, kwa kuzingatia kwamba
bado tunahitaji bado fedha kutekeleza masuala haya 12 ya Beijing, wizara ambayo
haitazingatia Bajeti yenye mtazamo wa
Kijinsia, isipewe fedha”
Mwongozo wa Taifa wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026,
inazitaka wizara, Idara na mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia bajeti yenye
mrengo wa Kijinsia (GRB), katika Bajeti zao ambapo zitatakiwa kuzingatia Haki
na mahitaji ya makundi maalum.
Kwa upande wake , Naibu waziri amesema kwamba, serikali
inazingatia na kuheshimu sana utekelezaji wa masuala yote 12 ya Beijing, na
kuhakikisha kila sekta inatekeleza na
kuweka rasilimali zitakazowezesha kuondoa
mapungufu ya usawa wa Kijinsia nchini.
“sisi zote tumetunzwa na kulelewa na kina mama, tunahitaji
kuwahshimu kwa kuweka miundombinu safi na salama katika kuboresha maisha yao,
hili ni deni kwetu sote, tunatakiwa kuwajibika kufanya hivyo” alisema.
Akizungumza, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
na Kiongozi wa Mkutano wa Beijing, Balozi Getrude Mongela, alisema kwamba
serikali inatakiwa kufuatilia namna ambavyo wanawake wananufaika na bajeti
inayotengwa na serikali ili kuondoa tatizo la mnyororo wa thamani kwa wanawake
wakulima wa Tanzania
“Nakuomba ukafuatilie, fedha za bajeti zinazotengwa zinaishia
wapi?, zinawafikia wanawake? Fedha hizi za bajeti zinazokusanywa na serikali
zinatoka mifukoni mwa wanawake, hii miradi mikubwa ya maendeleo inawanufaisha
wanawake?” alisema Balozi Mongela na kuongeza:
“Nenda hatua kwa hatua ukokotoe bajeti ya kilimo, ambayo wanawake
wengi wamewekeza nguvu zao huko, fedha kiasi gani zinakwenda kuwezesha wanawake
kujenga viwanda vya kuongeza dhamani ya mazao yao? Angalia ni fedha kiasi gani
zimeenda kwenye vikundi vya wanawake?”
“miaka 80 yangu, natamani kuona jembe la mkono limeondoka,
kutumia teknolojia katika kilimo ili kumuondolea mwanamke mzigo wa kazi,
natamani kuona naibu waziri kusimamia bajeti ya kilimo, ikiondoa mzigo kwa
wanawake”aliongeza Balozi Mongela.
Kongamano hili la Kitaifa, lenye
kauli mbiu ya Kusherehekea Miaka 30+
Beijing: Tumetoka wapi, Tulipo, na
Tuendako, pamoja na mengine malengo yake ni pamoja na Kutoa nafasi kwa
wanaharakati wa harakati za wanawake nchini kusherehekea hatua muhimu na
kuheshimu historia ya harakati za ukombozi wa wanawake;
Pia kufikiria upya maisha ya wanawake baada ya Beijing +30, kuchambua
hali ya sasa, changamoto na jinsi changamoto za wanawake zinavyokabiliwa pamoja
na matokeo yake;
Aidha lengo lingine ni kujenga mitandao, kujifunza, kuunda
pamoja taasisi za kimabadiliko, na kuunganisha nguvu kwa mustakabali wa pamoja.
No comments:
Post a Comment