Sunday, June 2, 2024

TGNP yaendelea na zoezi la uraghibish Kasulu

 TGNP yaendelea na zoezi la uraghibish Kasulu

Washiriki wa Utafiti Shirikishi wa Kiraghibish (PAR) wakiwasilisha kazi za vikundi ambazo waliibua wenyewe  juu ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia zilizopo kwenye kata ya Kumsenga Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma.


na Deogratius Temba, 

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughuikia Idadi ya Watu (UNFPA), wameendesha zoezi la utafiti shirikishi  wa kijamii (PAR) katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu kuiwezesha jamii kuibua, kuchambua na kuweka mikakati ya kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika jamii. 

Uraghibishi huu unafanyika katika kata za Murusi na Kumsenga zilizopo Halmashairi ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma. Zoezi hili limehusisha wananchi kutoka katika vikundi vya wanawake  na wanaume zaidi ya 30, na washiriki wapatao 50. Uraghibishi huu unatumia mbinu shirikishi ya Uibuaji, Uchambuzi na kuweka mipango ya Utekelezaji (U-3) katika kubaini sababu za tatizo la Ukatili wa kijinsia na kuweka mikakakti ya kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.

Hii ni sehemu ya Utekelezaji  wa Mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa, chini ya UNFPA, wilayani Kasulu, unaolenga pia kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto ili kuwawezesha kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.

Baada ya washiriki kuibua, na kuwasilisha kwa majadiliano, Mwezeshaji aliwaelekeza kupanga changamoto hizo kwenye vipaumbele. ili kusiwepo na udhaifu katika kupanga vipaumbele, washiriki walitakiwa kupigia kura aina za vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ambazo ni kero zaidi na vimeshamiri na wangetaka zifanyiwe kazi kwa haraka. walitumia punje za maharage ya njano kupigia kura.

Mwezeshaji aliwaelekeza washriki kufanya uchambuzi wa kina kwa kutumia mbinu ya "uibuaji, uchambuzi, na utatuzi -(U-3)" kwa kuangalia sababu za wazi (nje), za Kina (ndani-mifumo) na kupenekeza njia za utatuzi. Mti wa Mtatizo (problem Tree) ulitumika kuwawezesha zaidi washiriki kupata uelewa wa mbinu hizi.




aina za Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia zilizoibuliwa kwenye Uraghibish ndani ya Kata ya Kumsenga na washiriki na kuanza kupangwa kwa vipaumbele




No comments:

Post a Comment