TWCC yawataka wanawake kujitokeza uchaguzi serikali za Mitaa
Na Deogratius Temba; Chamwino
WANAWAKE wametakiwa kujiimarisha
kiuchumi kwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa na kushiriki kwenye nafasi za
uongozi na maamuzi katika ngazi mbalimbali ili kubadili mfumo itakayoweka mazingira
wezeshi kwa wanawake kufanya biashara
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Mwajuma Hamza, wakati
wa kufunga mafunzo ya wanawake viongozi yanayolenga kuongeza kasi ya kuwezesha
wanawake vijiji ni, na kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi
wa serikali za Mitaa mwaka huu 2024, yanayofanyika katika Halmashauri ya Wilaya
ya Chamwino , Mkoani Dodoma.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mradi
wa kuongeza kasi ya uwezeshaji wanawake vijijini, unaofadhiliwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (Unwomen) unaotekelezwa
katika wilaya ya Chamwino.
“wilaya ina kata 36, madiwani
wanaume ni 35 na mwanamke Diwani wa kata ni mmoja pekee, vijiji 107 lakini mwanamke
mwenyekiti ni mmoja pekee. Hii sio sawa, hakuna usawa wa Kijinsia katika
uongozi, tunahitaji mabadiliko makubwa katika eneo hili. Tuongeze wanawake
viongozi tafadhali” alisema Mwajuma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Bodi ya TWCC, Mercy Silla, alisema kwamba, wanawake wanatakiwa kumiliki uchumu
wa viwanda vikubwa na miradi mingine mikubwa ili kujikwamua kiuchumi,
kubadilisha kaya zao kiuchumi na kujiwezesha kiuchumi ili waweze kugombea
nafasi za uongozi
“Tunataka wanawake wamiliki
miradi mikubwa yenye fedha. Kugombea uongozi unahitaji fedha na unahitaji kuwa
vizuri kiuchumi, familia za viongozi ni lazima ziwe na ustawi, ndio maana TWCC
tunasisitiza, wanawake wafanyabiasha kuboresha biashara zao, na kuhakikisha
wanajitokeza kugombea nafasi za uongozi sambamba na kuingia kwenye nafasi za
maamuzi ili wakabadilishe sera ambazo haziwapi nafasi wanawake kuwa wawekezaji
au wafanyabsiahara wakubwa”alisema Sila.
Lakini pia amesema kwamba,
wanawake watakapokuwa kwenye uongozi watapata nafasi ya kutoa elimu na
kubadilisha mitazamo hasi, mila na desturi kandamizi zilizoko kwenye jamii juu ya uwezo wa wanawake
viongozi
Mafunzo hayo yamewezeshwa na
Deogratius Temba, ambaye ni mtaalam na mkufunzi wa masuala ya Jinsia na uongozi,
na kuwajumuisha viongozi wanawake kutoka katika ngazi ya Kitongoji, ujumbe wa
serikali za Mitaa, kamati na bodi mbalimbali na madiwani wanawake kutka kata 18
za mradi huo.
No comments:
Post a Comment