Na Mwandishi Wetu
KUTOKANA na kuongezeka kwa
vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika Jamii, hasa kwa watoto wanapokuwa nje ya
shule, Jamii imeashwa kuwalinda watoto wa kike na kiume wanaotarajiwa kuahitimu
darasa la saba mapema mwezi Oktoba mwaka huu.
Pia wazazi wameaswa kuhakikisha wakati wahitimu wa darasa la saba wakisubiria kuijunga na kidato cha kwanza mwakani, wanawaandalia watoto sehemu salama ya kuendelea kujifunza na kuongeza maarifa ya kitaaluma au kuboresha vipawa na vipaji vyao Zaidi.
Akizungumza wakati wa mahafali ya
nane ya shule ya awali na msingi ya NABA iliyopo Kata ya Saranga, manispaa ya
Ubungo, jijini Dar es salaam, Diwani wa kata ya Saranga Edward Laizer ambaye
alikuwa mgeni rasmi, alisema kwamba, wanafunziz wanaohitimu wamekuwa salama na
kufikia kuhitimu darasa la saba akwa sababu waalimu walikuwa makini, na walishirikiana vizuri na wazazi.
“Nina waasa sasa kuendeela kuwa
karibu na hawa watoto, bado hawajawa watu wazima, wanatakiwa kuendelea kulelewa
kimaadili, wanahitakiwa kuwa chini ya uangalizi, kuhitimu kwao leo tusiwache
waka anza kuzurura mitaani, wakajiunga na vikundi vya uhalifu”.alisema Laizer
katika hotuba yake.
Aliongeza kwamba, Vijana wakikosa uangalizi,
ndio tunapata changamoto ya watoto wa mitaani, panya road na makundi mengine
ambayo yanaibuka katika jamii.
“Tunawasihi sana miezi hii ya
kusubiria matokeo, tuwatafutie hawa vijana sehemu ya kukaa, vitu vya kufanya,
kujifunza, ili wawe bize badala ya kuzurura mitaani. Zipo fursa za kujifunza
computer, ufundi wa muda mfupi, kujifunza stadi za maisha, ambavyo pia
vitawafanya watambue vipaji vyao” aliongeza
Laizer aliongeza kwamba, Watoto wa kike wengi wanapata
ujauzito wakati wa kusbiria matokeo ya shule, au hata wengine kuolewa kabla ya
kujiunga na kidato cha kwanza, wakati ni
kosa la jinai, kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 pamoja na
kanuni zake.
Pia alipongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuifanya kata ya
Saranga kupaa kielimu kutokana na Shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma, katika
mitihani ya Kitaifa, kimkoa na kiwilaya.
Awali akisoma taarifa ya maendeleo ya shule hiyo, Mwalimu
Mkuu, Mariam Mbaya, alisema kwamba, shule imewekaza kwenye kumjenga mtoto kukua
kinidhamu, kitaaluma na kujitambua.
“Mheshimiwa Mgeni rasmi, kama unavyowaona watoto hawa , wamejengwa kwenye
misingi ya nidhamu, kujiamini, na kujitambua. Wanafunzi waliohitimu NABA
wanajiamini, wanauwezo mkubwa wa kujieleza, na wanafaulu vizuri. Matokeo yetu
kitaaluma ni mazuri sana. Na tunaendelea kujitahidi kufanya vizuri Zaidi”
alisema Mwalimu Mkuu.
Shule ya awali na msingi NABA ipo katika manispaa ya Ubungo,
kata ya Saranga.
No comments:
Post a Comment