Na Mwandishi wetu, Unguja
Chama cha wananci (CUF) kimeanza mchakato wa kuandaa sera ya
Jinsia ya Chama itakayotumika kurasimisha masuala ya kujinsia ndani ya chama
kwa kipindi chote
Mchakato huu ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Mkutano
wa Baraza la Vyama vya siasa nchini lilolomwagiza Msajili wa Vyama vya Siasa
kushirikiana na wadau ili kuviwezesha vyama vya siasa kuwa na sera ya Jinsia
ili kuzingatia usawa wa kijinsia na kuongeza ushiriki wa wanawake, vijana, watu
wenye ulemavu katika nafasi za uongozi na maamuzi ndani ya chama.
Mchakato huu unawezesha na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)
na shirika la Wanawake, Sheria katika Maendeleo Afrika (WilDAF), kwa kutoa
wataalamu ambao wanajenga uwezo kwa watendaji wa CUF kuandaa rasimu ya sera
hiyo.
Akizungumza wakati wa maandalizi ya rasimu hiyo, Naibu
Katibu Mkuu Zanzibar Mbarouk Seif Salim, wakati wa kukaribisha wajumbe wa kikao
kazi hicho kuanza kazi, alisema kwamba,
chama kimefurahi kwamba kimekuwa miongoni mwa vyama vya awali ambavyo vitatengeneza
sera hiyo, na ana matumaini kuwa kazi hiyo itamalizika kwa wakati na kuleta
tija ndani ya chama.
“sisi CUF ni chama cha siasa ambacho tumekuwa tukizingatia usawa wa kijinsia, kwenye ushiriki wa wanawake
tumejitahidi, bado hatujafikia 50:50 lakini tuna matumaini kuwa tutafanya vizuri
sana baada ya sera hii kukamilika” alisema Naibu Katibu Mkuu.
Aidha Katibu wa Kikosi kazi, Ally Juma Khamis, alisema
kwamba kwa niaba ya kikosi kazi hiyo, wameamua kujituma, kuhakikisha kazi hiyo
ya kuandaa sera inakamilika kwa wakati na inawasilishwa kwenye vikao vya juu
kwaajili ya kupata baraka na kuanza kutekelezwa.
“sisi tunashukuru Chama kwa kutuamini, kututeua tuwe sehemu
ya maandalizi ya sera hii. Tumeaminiwa kuwawakilisha wenzetu, hatuta wangusha,
tutahakikisha tunatoka na sera nzuri ya Kijinsia ambayo italeta mabadiliko
makubwa ya usawa wa kijinsia ndani ya chama chetu” amesema Ally.
Upande wake, Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba,
alisema kwamba yeye amefkia CUF kwaajili
ya kuwezesha watendaji wa chama kutengeneza sera hiyo, na kwamba mchakato huu
unafanywa na chama chenyewe sio TGNP au WiLDAF.
“Sisi hapa ni wawezeshaji tu, kazi hii inafanywa na chama
chenyewe, tunawawezesha kutambua masuala ya Kujinsia na namna ya kuyaweka ili
yaeleweke, tunawawezesha pia kuwa na uwezo wa jicho la kijinsia , baadaye
wanayaweka kwenye sera, hapa mimi nimekuwa nikijibu maswali yao zaidi,
ninaamini hiki kikosi kazi kitamaliza kazi kwa wakati na kuanza utekelezaji wa
sera hii”alisema Temba
Mchakato huu umehusisha kupitia nyaraka za chama zikiwemo
Ilani, Katiba, Kanuni, sera, program na nyaraka nyingine za kiuendeshaji ili
kuangali kwa namna zilivyozingatia usawa wa Kijinsia.
washiriki wa kikosi kazi cha kuandaa sera ya Jinsia ya CUF wakiwa katika Picha ya Pamoja
washiriki wa kikosi kazi cha kuandaa sera ya Jinsia ya CUF wakiwa katika Picha ya Pamoja
washiriki wa kikosi kazi cha kuandaa sera ya Jinsia ya CUF wakiwa katika Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment