TAMASHA LA JINSIA KUWATUNANISHA ZAIDI YA 500 SAME.
Mtandao wa Jinsia Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaotetea haki za wanawake na usawa wa jinsia, wanaharakati binafsi kwa ufadhili wa Ubalozi wa Watu wa Canada, Sweeden, Coady Institute Canada, Seedchange, wameandaa tamasha hilo ambalo linatarajiwa kutoa fursa ya kutafakari na kutathmini changamoto zilizopo kwenye jamii na namnana kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi wakati akizungumza na waandishi wa Habari, Wilayani Same juu ya ujui wa tamasha la jinsia ambalo litafanyika kuanzia October 5-7, katika uwanja wa kwasa kwasa, huku likibebwa na dhima isemayo Haki ya Uchumi, Rasilimali ziwanufaishe wananchi Walioko Pembezoni.
“Tamasha hili la Jinsia Kanda ya Kaskazini linatarajiwa kuwaleta washiriki zaidi ya 500 kutoka pande mbalimbali za nchi kusherekea mafaniko, kujadili namna bora ya kutumia fursa za zilizopo na zinazoibuka za kiuchumi ili kuongeza ajira zenye staha na kuleta maisha endelevu”Alieleza taarifa ya Mkurugenzi Liundi.
Tamasha la jinsia kanda ya kaskazini ambalo linafanyika Wilayani Same kwa mara ya kwanza litafunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, ambalo litatua fursa ya kutafakari na kutathmini changamoto zilizopo na namnana kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Edward Mpogolo amelipongeza TGNP kwa kuandaa tamasha hilo,na kusema ujio wa tamasha hilo litakuwa sehemu ya mkombozi kwa mwanamke, ambapo kuna matarajio makubwa ya kusaidia kuleta mabadiliko kwenye jamii hususani masuala ya usawa wa kijnsia.
“Kihistoria hatujawahi kupata watu 500 kwa wakati mmoja,tunajua tgnp mngeweza kuamua mkanda sehemu nyingine lakini mkaamua kuja kufanya Same,Imani yetu ni kwamba ile dhamira ya tamasha ya kumkomboa mwanamke kiuchumi hasa wa pembezoni ni sahihi na, litatoa fursa ya kuwafumbua macho wanawake kutambua fursa zilizopo na kuzitumia”Alisema Mpogolo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment