WAZAZI WASIO WAJALI NA KULINDA WATOTO KUCHUKULIWA HATUA- WAZIRI
GWAJIMA
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imetangaza kuwachukulia hatua kali za kisheria
wazazi na walezi watakaoshidnwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kuwalea na
kuwalinda watoto na kusababisha kufanyiwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia
kutokana na kuzurura hovyo mitaani na kufanya shughuli mbalimbali za ajira
kinyume na sheria.
ameahidi
kuwachukulia hatua kali
za kisheria wazazi
na walezi wote
watakaobainika kuwaachia watoto
kuondoka nyumbani na
kuingia mitaani na kufanya shughuli
mbalimbali .
hayo yamesemwa na, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi
maalum Dkt . Doroth Gwajima,
jijini Dar es Salaam, wakati
akifungua mkutano wa
siku mbili uliuowakutanisha wadau
wa huduma za Ustawi
wa Jamii nchini.
Katika mkutano huo
Dkt. Gwajima amesema
serikali ya awamu
ya Sita kupitia
wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wanawake
na Makundi Maalum
kwa kuungana na
wadau wote wa
ustawi wa jamii
wanakuja na mpango
maalum utakaofanikisha kuondoa
mtandao mzima unaofanikisha kuzagaa
kwa watoto mitaani
katika miji mbali mbali
hapa nchini .
Aidha waziri huyo
pia amesema wizara
yake imeona kuna
umuhimu wa kutungwa
kwa sheria maalum
itakayo komesha vitendo
vya baadhi ya
watu wenye ulemavu
wanaotuimia viti vyenye
magurudumu kutumia ulemavu
wao kwa kuomba omba
kitendo alichosema kinaongeza kundi
la Ombaomba mitaani.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam
Amos Makalla akizungumza katika
mkutano huo amesema
kwa kushirikiana na
wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, wanawake na
Makundi Maalum tayari
wanampango kazi la kuwajengea
mazingira mazuri ya
kuwatambua watoto wa mitaani
na omba omba kwa
kuangalia mahala watakapopelekwa mara baada ya
kuondolewa mitaani.
Mkutano huo wa
wadau wa huduma za Ustawi
wa Jamii umekwenda sambamba na
uzinduzi wa vitabu
viwili ikiwemo kitabu
cha Kanuni za
Maadili ya kufanya
kazi na watoto pamoja na uzinduzi wa kitabu
cha kiongozi cha
penzi kitakachosaidia kutoa
muongozo katika vituo vya
kulelea watoto mchana .
Kwa mujibu wa sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, ni wajibu wa
mzazi kuhakikisha mtoto anapata ulinzi, anakuwa salama, anatunzwa na kulelewa
katika mazingira salama na asifanyiwe kitendo cha Ukatili au udhalilishwaji
hadi atakapotmiza umri unaoatakiwa kisheria kuwa sasa amekuwa mkubwa. Kuhsindwa
kutimiza wajibu ho na mengine yaliyoainishwa kwenye sheria hiyo ni kosa.
No comments:
Post a Comment