Friday, June 7, 2024

TGNP na UNFPA wawezesha jamii kuibua vitendo vya Ukatili wa Kijinsia Kasulu

 TGNP na UNFPA wawezesha jamii  kuibua vitendo vya Ukatili wa Kijinsia  Kasulu


Washiriki katika hafla ya kutoa mrejesho wa Utafiti Shirikishi (Participatory Action Research) kutoka kata za Kumsenga na Murusi, Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Kigoma, Utafiti huo umewezeshwa na TGNP na UNFPA ili kutokomeza Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia 



Na Deogratius Koyanga, Kasulu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  wamefanya mrejesho wa Utafiti raghibishi (Participatory Action Research [PAR]) uliofanyika katika kata ya Mrusi na Kumesenga, Halmasahuri ya Kasulu Mji.

Utafiri shirikishi huo ni sehemu ya mradi wa kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia unaotekelezwa na TGNP na Shirikla la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA), unaotekelezwa katika wilaya ya Kasulu chini ya program ya Pamoja ya Mashirika ya Umoja wa Kimataifa

Katika wasilisho lao, washiriki wa PAR katika Halimashauri ya Kasulu Mji, walisema kwamba kupitia mchakato wa PAR uliowezeshwa na TGNP kwa kutumia mbinu za U-3 za Uibuaji, Uchambuzi na Utekelezaji, wameweza kuibua sababu za kina za kushamiri kwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto katika eneo hilo na kubaini njia za utatuzi wake ambazo kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi za serikali za mitaa na wilaya watashirkiana na kuhakikisha vinakoma.

“Tumeona jinsi ambavyo kata zetu hizo, mbili zimeadhirika na vitendo vya ubakaii, ulawiti na mimba za utotoni, hatutaki hali hii iendelee, tutahakikisha sasa kwa kushirkiana na viongozi wetu tunazuia kabisa kwa kushirikiana na viongozi wetu.”alisema Beatrice Christopha msomaji wa risala mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri.

“Tumejifunza pia kuwahusisha viongozi wetu kama madiwani na watendaji wote wa serikali tulio nao katika ngazi ya mitaa, kata na wilaya ili kupata ufumbuzi wa changamoto zilizo nje ya uwezo wetu sisi kama wananchi. Katika mchakato huu wa siku sita, tulijadili kwa kina, tulichambua kwa kina na tuliweza kuibua changamoto mbalimbali ndani ya Kata zetu” alisema  Beatrice

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mabena Paschalina, alisema kwamba kazi iliyofanywa na TGNP ni kubwa kuwajengea uwezo wananchi hao uwezo na kujitambua na kuamua kuchukua hatua za changamoto za kukidhiri kwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia.

“Nyie mliojengewa uwezo na TGNP ni wazazi lakini pia mnaishi miongoni mwa jamii, ambako vitendo vya Ukatili vinatokea, ninawataka sasa tuchukue hatua, tupite kwenye mikutano, vikao, majukwaa, kwenye taasisi za dini, shuleni nk. Kuhakikisha ujumbe unawafikia watu wazima lakini pia na watoto” alisema

Kaimu Mkurugenzi amesema kwamba, Halmasahuri itaendelea kutoa ushirkiano kwa wadau kama TGNP na UNFPA katika kutekeleza afua za usawa wa Kijinsia, sambamba na kuhakikisha kwamba jamii inabadilika kimtazamo na kitabia kwa kusimamia vizuri sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kuwepo na haki na usawa.

Ameongeza kwamba, halmashauri kwa kushirikiana na vyombo vingine, itahakikisha  kwamba wananchi wote wanakuwa salama, hawafanyiwi vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ili waweze kunufaika na fursa zilizopo na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya Tanzania kuwezesha wananchi kiuchumi. 

Kikao hicho cha mrejesho kilihudhuriwa pia na wakuu wa idara na Vitengo wa Halmasahuri pamoja na Mkuu wa dawati la Jinsia -Polisi Kasulu, ambao walipata nafasi ya kujibu baadhi ya masuala yaliyoibuliwa ambayo yapo chini ya maeneo yao ya kiutendaji.

wengine waliohudhuria ni watendaji kata mbili za Kumsenga na Murusi, Madiwani wa kata  na viti maalum na Maafisa Maendeleo ya jamii wa kata husika.
















Wednesday, June 5, 2024

Vitendo vya Ubakaji, ulawiti kero Kasulu

 Vitendo vya Ubakaji, ulawiti kero Kasulu


Washiriki wa Utafiti shirikishi wa Kiraghibish (participatory Action Research-PAR) kutoka kata ya Murusi, Kasulu Mjini, walijadiliana, kuchambua na kubaini sababu za kushamiri kwa vitendo vya Ubakaji katika eneo hilo. PAR ni shughuli inayotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA katika Halmashauri hiyo.


 Na Deogratius  Koyanga, Kasulu

Wananchi wa kata ya Murusi, Halmashuri ya Mji wa Kasulu, mkoani Kigoma, wamesikitishwa na kushamiri kwa vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto.

Sababu zilizoibuliwa na wananchi hao, wakati wa zoezi la uraghibish  shirikishi (Participatory Action Research –PAR) ulioendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA),  ni pamoja na Imani za kishirikina ambao hupelekea vitendo vya ulawiti kwa wanaume na ubakaji kwa wanawake na wasichana unaosababishwa na tamaa ya mali.

Aidha, sababu nyingine iliyoibuliwa ni unywaji wa pombe kupita kiasi kwa wazazi na kupelekea watoto kukulia vilabuni, na hivyo kukosa malezi stahiki. Pia unywaji pombe kupitiliza husababisha watu kubakwa au kubaka.

“hapa kwentu kuna tatizo la watu kudanyangwa na waganga wa kienyeji kuwa ili wapate utajiri wabake watoto wao. Mfano baba kubaka binti ili apate utajiri, na wanafamilia wengine kukaa kimya/kuyamaliza kifamilia” wamesema washiriki hao

Pia imeonekana kwamba, kuna vitendo vya Ubakaji kwa watu wanaoishi na ulemavu – mfano wagonjwa wa akili hadi kupewa mimba.





Sunday, June 2, 2024

TGNP yaendelea na zoezi la uraghibish Kasulu

 TGNP yaendelea na zoezi la uraghibish Kasulu

Washiriki wa Utafiti Shirikishi wa Kiraghibish (PAR) wakiwasilisha kazi za vikundi ambazo waliibua wenyewe  juu ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia zilizopo kwenye kata ya Kumsenga Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma.


na Deogratius Temba, 

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughuikia Idadi ya Watu (UNFPA), wameendesha zoezi la utafiti shirikishi  wa kijamii (PAR) katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu kuiwezesha jamii kuibua, kuchambua na kuweka mikakati ya kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika jamii. 

Uraghibishi huu unafanyika katika kata za Murusi na Kumsenga zilizopo Halmashairi ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma. Zoezi hili limehusisha wananchi kutoka katika vikundi vya wanawake  na wanaume zaidi ya 30, na washiriki wapatao 50. Uraghibishi huu unatumia mbinu shirikishi ya Uibuaji, Uchambuzi na kuweka mipango ya Utekelezaji (U-3) katika kubaini sababu za tatizo la Ukatili wa kijinsia na kuweka mikakakti ya kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.

Hii ni sehemu ya Utekelezaji  wa Mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa, chini ya UNFPA, wilayani Kasulu, unaolenga pia kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto ili kuwawezesha kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.

Baada ya washiriki kuibua, na kuwasilisha kwa majadiliano, Mwezeshaji aliwaelekeza kupanga changamoto hizo kwenye vipaumbele. ili kusiwepo na udhaifu katika kupanga vipaumbele, washiriki walitakiwa kupigia kura aina za vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ambazo ni kero zaidi na vimeshamiri na wangetaka zifanyiwe kazi kwa haraka. walitumia punje za maharage ya njano kupigia kura.

Mwezeshaji aliwaelekeza washriki kufanya uchambuzi wa kina kwa kutumia mbinu ya "uibuaji, uchambuzi, na utatuzi -(U-3)" kwa kuangalia sababu za wazi (nje), za Kina (ndani-mifumo) na kupenekeza njia za utatuzi. Mti wa Mtatizo (problem Tree) ulitumika kuwawezesha zaidi washiriki kupata uelewa wa mbinu hizi.




aina za Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia zilizoibuliwa kwenye Uraghibish ndani ya Kata ya Kumsenga na washiriki na kuanza kupangwa kwa vipaumbele




Wednesday, May 29, 2024

TWCC yawataka wanawake kujitokeza uchaguzi serikali za Mitaa

TWCC yawataka wanawake kujitokeza uchaguzi serikali za Mitaa

Na Deogratius Temba; Chamwino

Mkurugenzi Mtendaji, TWCC, Ms. Mwajuma Hamza, akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Uongozi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Chamwino, Mkoani dodoma, yaliyowahusisha wanawake kutoka kata 18 za Wilaya hiyo.


WANAWAKE wametakiwa kujiimarisha kiuchumi kwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa na kushiriki kwenye nafasi za uongozi na maamuzi katika ngazi mbalimbali ili kubadili mfumo itakayoweka mazingira wezeshi kwa wanawake kufanya biashara

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Mwajuma Hamza, wakati wa kufunga mafunzo ya wanawake viongozi yanayolenga kuongeza kasi ya kuwezesha wanawake vijiji ni, na kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi wa serikali za Mitaa mwaka huu 2024, yanayofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino , Mkoani Dodoma.

Mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa kuongeza kasi ya uwezeshaji wanawake vijijini, unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (Unwomen) unaotekelezwa katika wilaya ya Chamwino.

“wilaya ina kata 36, madiwani wanaume ni 35 na mwanamke Diwani wa kata ni mmoja pekee, vijiji 107 lakini mwanamke mwenyekiti ni mmoja pekee. Hii sio sawa, hakuna usawa wa Kijinsia katika uongozi, tunahitaji mabadiliko makubwa katika eneo hili. Tuongeze wanawake viongozi tafadhali” alisema Mwajuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TWCC, Mercy Silla, alisema kwamba, wanawake wanatakiwa kumiliki uchumu wa viwanda vikubwa na miradi mingine mikubwa ili kujikwamua kiuchumi, kubadilisha kaya zao kiuchumi na kujiwezesha kiuchumi ili waweze kugombea nafasi za uongozi

“Tunataka wanawake wamiliki miradi mikubwa yenye fedha. Kugombea uongozi unahitaji fedha na unahitaji kuwa vizuri kiuchumi, familia za viongozi ni lazima ziwe na ustawi, ndio maana TWCC tunasisitiza, wanawake wafanyabiasha kuboresha biashara zao, na kuhakikisha wanajitokeza kugombea nafasi za uongozi sambamba na kuingia kwenye nafasi za maamuzi ili wakabadilishe sera ambazo haziwapi nafasi wanawake kuwa wawekezaji au wafanyabsiahara wakubwa”alisema Sila.

Lakini pia amesema kwamba, wanawake watakapokuwa kwenye uongozi watapata nafasi ya kutoa elimu na kubadilisha mitazamo hasi, mila na desturi kandamizi  zilizoko kwenye jamii juu ya uwezo wa wanawake viongozi

Mafunzo hayo yamewezeshwa na Deogratius Temba, ambaye ni mtaalam na mkufunzi wa masuala ya Jinsia na uongozi, na kuwajumuisha viongozi wanawake kutoka katika ngazi ya Kitongoji, ujumbe wa serikali za Mitaa, kamati na bodi mbalimbali na madiwani wanawake kutka kata 18 za mradi huo.









Saturday, March 9, 2024

TGNP yawapiga msasa viongozi wanawake Kondoa

 TGNP yawapiga msasa viongozi wanawake Kondoa


Na Mwandishi wetu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wamefanyamafunzo ya kujenga uwezo wa uongozi na kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafsi za uongozi na maamuzi

Mafunzo hayo ambyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Mwanamke Ongoza  unaotekelezwa na  TGNP kwa kushirikiana na Taasisi ya Aga Khan Foundation na Serikali ya watu wa Canada, unaolenga kujenga uwezo kwa viongozi wanawake walioko madarakani ili kuboresha utendaji wao kwa manufaa ya jamii na kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi.

Pia mradi huu, unataka kuondoa vikwzo vinavyo wafanya wanawake waliopewa dhamana ya uongozi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kiuongozi ipasavyo, ambavyo ni pamoja na shughuli za huduma na matunzo kama vile utafutaji wa maji, shughuli za nyumbani, kuhudumia wagonjwa na utunzaji wa watoto ambazo zinaweza kufanywa na mtu mwingine kwenye familia, ikiwa ni sambamba na kubalisha mitazamo, mila na desturi na tamaduni zilizopitwa na wakati ambazo zinakwamisha wanawake kushiriki kwenye uongozi.

Kwa upande wake, Diwani wa Viti maalum Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Madina Fentu, alisema kwamba, mradi huu umemsaidia kwa kiasi kikubwa kupata uelewa wa mambo mengi lakini pia mume wake ameweza kushiriki moja ya semina ambazo alinufaika nazo.

“kwa kweli, ile warsha wa wenza wa viongozi wanawake imetusaidia sana, wenza wetu waliposhiriki, tumeona mabadiliko, pamoja na kwamba mimi mume wangu alikuwa akinisaidia awali, lakini aliongeza sana kunisaidia, hasa pale ninapokuwa na majukumu mengi ya kiuongozi na kushindwa kuhudumia familia” alisema Madina

Mapendekezo yaliyotoka kwenye warsha hiyo ni pamoja na Halmashauri zianzishe kanuni ya utaratibu wa kuwatangaza wanawake viongozi wa mfano wa kuigwa  na jamii na wapewe nafasi ya kuonekana ili kubadilisha mitazamo hasi kwa jamii kwamba wanawake hawezi kuwa viongozi wazuri.

Kutoa elimu ya kubadilisha mitazamo hasi kwa viongozi wa dini zote, wazee wa mila, wazee maarufu ili wawe mstari wa mbele katika kubadilisha mitazamo hasi, Kuweka kanuni kali za kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, Udhalilishaji wa kijinsia wakati wa chaguzi, sambamba na kuendelea kuwaelimisha wanaume ili kuwasaidia wenza wao ambao ni viongozi wa kisiasa katika majukumu ya kifamilia ili waweze kuhsiriki vizuri kwenye majukumu yao.

Viongozi wanawake walioshiriki mafunzo hayo ni Madiwani  wa Kata, madiwani wa viti maalum, Wenyeviti wa Vitongoji, wajumbe wa serikali za Vijiji, viongozi wa vyama vya siasa, na viongozi wataalamu ngazi ya jamii.  

 


















Tuesday, March 5, 2024

TGNP yawapiga msasa wadau na viongozi wanawake Dodoma

 TGNP yawapiga msasa wadau na viongozi wanawake Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Kondoa

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Imewajengea uwezo wadau mbalimbali kutoka kwenye mashirika, asasi na vikundi vya kijamii kuhusu namna ya kuongeza Ushiriki wa Wanawake ngazi za uongozi na maamuzi Halmashauri ya Wilaya Kondoa Mkoani Dodoma

Mafunzo haya yanatolewa katika Halmashauri za Wilaya ya Kondoa,Morogoro na Mtwara, kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa ‘’Mwanamke Ongoza-She Leads’’ unaotekelezwa na TGNP kwa ufadhili wa Agakhan Foundation na Serikali ya Watu wa Canada unaolenga kuwezesha wanawake viongozi walioko madarakani kutekeleza majukumu yao vizuri ya kiuongozi na kuongeza ushiriki Zaidi wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi.



Mafunzo hayo yamewanufaisha jumla ya washiriki 30 ambao ni viongozi wa vikundi vya Bodaboda, Dini, vikundi vya kijamii, asasi za kiraia, watu maarufu wenye ushawishi, ambao baada ya mafunzo hayo wataenda kutoa elimu kwenye vikundi vyao na kushawishi wanawake kushiriki kikamilifu kwenye nafasi za maamu.

Mwezeshaji mwenza kutoka TGNP, Ester Wiliam alisema kwamba warsha hiyo inalenga  kuongeza uelewa wa dhana za jinsia na uongozi,ubainishaji wa fursa zilizopo katika mifumo ya vyama na kwenye jamii ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi,

Ameongeza kwamba washiriki hao, wamejengewa uwezo kubainisha na kuchambua  mifumo kandamizi inayomzuia mwanamke kushiriki katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi. 

“Mafunzo haya yanaenda kuongeza nguvu kwenye Tapo, kwasababu hawa tuliowajengea uwezo wanatoka kwenye makundi mengi, taasisi ndogondogo zinazofanya kazi katika kata ya Haubi, ambapo wakienda kupeleka ujumbe tutakuwa tumewafikia watu wengi sana” alisema Esther

Kwa upande wake Anna Ambrose, Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Haubi, amesema kwamba, mafunzo hayo yanaenda kubadilisha mitazamo ya jamii katika uwezo wa wanawake kuwa viongozi, lakini pia kubadilisha baadhi ya mila na desturi zinazokwamisha wanawake kuwa viongozi katika jamii hiyo.