TGNP yawapiga msasa wadau na viongozi wanawake Dodoma
Na Mwandishi
Wetu, Kondoa
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Imewajengea
uwezo wadau mbalimbali kutoka kwenye mashirika, asasi na vikundi vya kijamii kuhusu
namna ya kuongeza Ushiriki wa Wanawake ngazi za uongozi na maamuzi Halmashauri
ya Wilaya Kondoa Mkoani Dodoma
Mafunzo haya yanatolewa katika
Halmashauri za Wilaya ya Kondoa,Morogoro na Mtwara, kama sehemu ya utekelezaji
wa Mradi wa ‘’Mwanamke Ongoza-She Leads’’ unaotekelezwa na TGNP kwa ufadhili wa
Agakhan Foundation na Serikali ya Watu wa Canada unaolenga kuwezesha wanawake viongozi
walioko madarakani kutekeleza majukumu yao vizuri ya kiuongozi na kuongeza
ushiriki Zaidi wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi.
Mafunzo hayo yamewanufaisha jumla ya washiriki
30 ambao ni viongozi wa vikundi vya Bodaboda, Dini, vikundi vya kijamii, asasi
za kiraia, watu maarufu wenye ushawishi, ambao baada ya mafunzo hayo wataenda
kutoa elimu kwenye vikundi vyao na kushawishi wanawake kushiriki kikamilifu
kwenye nafasi za maamu.
Mwezeshaji mwenza kutoka TGNP, Ester
Wiliam alisema kwamba warsha hiyo inalenga kuongeza uelewa wa dhana za jinsia na
uongozi,ubainishaji wa fursa zilizopo katika mifumo ya vyama na kwenye jamii
ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi,
Ameongeza kwamba washiriki hao,
wamejengewa uwezo kubainisha na kuchambua mifumo kandamizi inayomzuia mwanamke kushiriki
katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi.
“Mafunzo haya yanaenda kuongeza nguvu
kwenye Tapo, kwasababu hawa tuliowajengea uwezo wanatoka kwenye makundi mengi,
taasisi ndogondogo zinazofanya kazi katika kata ya Haubi, ambapo wakienda
kupeleka ujumbe tutakuwa tumewafikia watu wengi sana” alisema Esther
Kwa upande wake Anna Ambrose, Katibu
wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Haubi, amesema kwamba, mafunzo hayo yanaenda
kubadilisha mitazamo ya jamii katika uwezo wa wanawake kuwa viongozi, lakini
pia kubadilisha baadhi ya mila na desturi zinazokwamisha wanawake kuwa viongozi
katika jamii hiyo.
No comments:
Post a Comment