Thursday, October 27, 2022

Fahamu ukweli kuhusu Ukeketaji na Mathara yake

 **FAHAMU UKWELI KUHUSU UKEKETAJI*

📌👨‍👩‍👧‍👦ELIMIKA NA SMAUJATA🇹🇿


Ukeketaji ni kitendo Cha uondoaji wa Sehemu au sehemu yote ya Siri ya nje ya mwanamke au kuweka jeraha lingine Kwa viungo vya uzazi vya mwanamke Kwa Sababu ZISIZO za kitabibu.


Ukeketaji hauna faida Kwa wasichana na wanawake kwani hutokwa na damu nyingi na matatizo ya kukojoa na baadae uvimbe maambukizo,pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.

Zaidi wa wasichana Milioni 200 waliohai Leo wamefanyiwa ukeketaji ktk nchi 36 za Afrika Mashariki na Asia ambapo ukeketaji unafanyika Kwa kiwango Cha juu.Ukeketaji mara nyingi hufanywa Kwa watoto wadogo wa umri kati ya miaka ya uchanga na miaka 15, ukeketaji ni ukiukwaji wa haki za binaadam na Ukatili Wa wasichana na wanawake, ukeketaji hauna faida kwa wasichana na Jamii na unapingwa na Jamii na shirika la afya Duniani.


*AINA ZA UKEKETAJI*

1.Uondoaji wa Sehemu ya kinembe chote (sehemu ya nje na Inayoonekana ya kisimi,ambayo nisehemu nyeti ya sehemu ya Siri ya mwanamke)au mlango wa ngozi unaozunguka sehemu ya Siri ya mwanamke.

2.Uondoaji wa Sehemu ya kisimi au chote na labia ndogo(mkunjo ya ndani ya uke)pamoja na bila kuondolewa labia kubwa(sehemu ya nja ya ngozi ya uke)

3.Kupunguza Kwa mwanya wa Sehemu ya uke Kupitia utengenezaji wa muhuri wa kufunika sehemu hiyo(infibulation)muhuri huundwa Kwa kukata na kuweka upya labia ndogo au kubwa wakati mwingine Kwa kushona au bila kuondolewa kisimi/kinembe .

4.Inajumlisha Taratibu zingine zote zenye madhara Kwa sehemu za Siri ya mwanamke Kwa madhumuni yasiyo ya matibabu kama kutoboa,kuvuta,kuchanja,kukwarua na kuchoka sehemu za Siri.

Hauna faida yoyote Bali husababisha madhila,unadharirisha wasichana na wanawake Kwa njia nyingi.Unaharibu uke wa mwanamke na huingilia utendakazi wa asili wa MIILI ya wasichana na wanawake.huhusishwa na ongezeko la hatari ya matatizo ya kiafya hatari ni kubwa zaidi ya kutokana na aina Kali zaidi ya Ukeketaji.


*ATHARI ZA UKEKETAJI*

1.Maumivu makali.

2.kutokwa damu nyingi(kuvuja damu nyingi)

3.uvimbe wa tishu za viungo vya uzazi

4.homa Kali

5.Maambukizi ya magonjwa kama pepopunda,

6.Matatizo ya mkojo

7.Matatizo ya uponyaji wa jeraha

8.Kupata mshituko

9.kifo


*MATATIZO YA MUDA MREFU NI KAMA*

. Matatizo wakati wa haja ndogo(kukojoa Kwa uchungu na Maumivu makali,maabukizu ya magonjwa ya Njia ya mkojo)

.Magonjwa wa Sehemu za Siri kama usaha,kuwashwa,magonjwa yatokanayo na backteria,na maambukzi mengine)

.matatizo ya hedhi

.kuweka jeraha la maisha

. Matatizo ya Kushiriki Ngono(Maumivu wakati wa kujamiiana,kutokufurahia Tendo la kujamiiana,na kutokuridhika au kufika kileleni)

. Matatizo wakati wa kujifungua,kutokwa damu nyingi,kuhitaji upasuaji,kujifungua mtoto mfu na vifo vya watoto wachanga.

.Kuhitaji kufanya upasuaju baadae mfano kuziba au kupunguza uwazi wa uke

.Matatizo ya kisaikolojia msongo wa mawazo wasiwasi,kupata kiwewe baada ya kujifungua,kuweka kisasi,kutokujiamini


*NANI YUPO HATARINI*

.Wasichana wadogo kati ya umri wa utoto na ujana na mara kwa mara kwa wanawake watu wazima


*SABABU ZA KITAMADUNI NA KIJAMII*

WHO inasema Sababu zinazofanya ukeketaji ufanywe hutofautiana kutoka eneo Moja Hadi jingine na vile vile baada ya muda na ni pamoja na  Mchanganyiko wa mambo ya KITAMADUNI ktk jamii na Jamii

1.Pale ambapo ukeketaji ni utaratibu wa kijamii(kadia ya jamii)shinikizo la kijamii lakufuata kile ambacho wengine wanafanya na wamekua wakifanya pamoja na haja ya kukubalika kijamii na hofu ya kukataliwa na Jamii ni motisha kubwa ya Kuendeleza Mila hiyo.

2.mara nyingi huchuliwa kama sehemu muhimu Kulea wasichana na njia ya kumtayarisha kwa utu uzima na ndoa.Ukeketaji mara nyingi huchochewa na Imani kuhusu kile kinachochukuliwa kuwa tabia ya kujamiiana inayolenga Kuhakikisha ubikra kabla ya ndoa na uaminifu wa Ndoa.

3.Pale ambapo huaminika ukeketaji huongeza fursa ya ndoa Kuna uwezekano mkubwa wa kufanya vitendo hivyo.

4.Ukeketaji unahusisha na MAADILI ya kitamaduni,ya uke na adabu ambayo ni pamoja na Dhana kwamba wasichana ni safi na warembo baada ya kuondolewa Kwa sehemu ya mwili zinazochukuliwa kua najisi ZISIZO za kike au kiume

5.ktk.jamii nyingi ambazo ukeketaji unafanywa inachukuliwa kua ni Mila ya kitamaduni ambayo mara nyingi hutumiwa kama Hoja ya Kuendeleza Ukatili huo 


*HATUA MUHIMU*

Kwa kuzingatia kazi ya miongo iliyopita mwaka 1997 WHO ilitoa tamko la pamoja dhidi ya Mila ya Ukeketaji Kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la umoja wa mataifa la Idadi ya ary UNFPA tangu 1997 juhudi kubwa zimefanywa kukabiliana na ukeketaji Kupitia utafiti,kufanya kazi ndani ya jamii na mabadiliko ktk sera za umma.

Mwaka huu wa 2022 WHO itazindua mwongozo wa mafunzo juu ya mawasiliano yanayomuhusu mtu binafsi PCC mbinu ya Ushauri ambayo inawahimiza watoa huduma ya Afya kupinga mitazamo Yao inayohusiana na ukeketaji na kujenga ujuzi wao wa mawasiliano Ili kutoa Ushauri nasaha wa kuzuia ukeketaji

Kuwapatia elimu watoto juu ya madhara ya Ukeketaji ktk jamii na wanawake Ili kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuzijua haki zao za msingi na kupinga Ukatili wa namna hiyo unaoendelezwa kwenye jamii ya Kiafrika.


Imeandaliwa na Mwamini Samaje

Makamu mwenyekiti idara ya Habari na mawasiliano SMAUJATA Taifa


💪🏾SMAUJATA #👨‍👩‍👧‍👦 

*KATAA UKATILI* *WEWE* *NI* *SHUJAA* *💪💪💪🇹🇿🇹🇿🇹🇿

No comments:

Post a Comment