Mambo muhimu kwa vyombo vya habari kukabiliana na Ukatili
Na Mwandishi Wetu.
SERA ya Jinsia ya vyomvo vya habari ya mwaka 2019, inavitaka
vyombo vyote vya habari kuzingatia yafuatayo ili kuepuka kuwa sababu au chanzo
cha ukatili wa kijinsia. Vyombo vya
habari vitaepuka kuunga mkono chuki au kushadidia ukatili wa kijinsia. Vitapaswa
kuepuka mambo yafuatayo:
Kutangaza au
kuchapisha kwa kinagaubaga habari za ubakaji au ukatili wa kingono kwa namna
ambayo itafanya waathirika watambulike;
Kushadidia picha chafu na za ukatili dhidi ya wanawake na
watoto;
Kuwadunisha wanawake kwa kuwabainisha kama viumbe dhalili
wanaostahili kufanyiwa ukatili, labda tu pale ambapo ukatili ni sehemu ya
habari inayosimuliwa;
Kuwadunisha ama kuwatumia vibaya wanawake kwa kuwaonyesha
kama viumbe dhalili wasio na uwezo wa kufanya lolote mbele ya ukatili na
unyanyasaji;
Kuwadunisha au kuwatumia vibaya wanawake na kuhujumu nafasi
chanya waliyo nayo, na umuhimu wao katika jamii;
Kushadidia unyanyasaji wa mawazo[1]mgando
juu ya jinsia, na
Kuchapisha habari ambazo zinaweza kuibua vurugu na chuki
kutokana na uwasilishaji mbaya wa masuala ya jinsia au kutukuza ukatili dhidi
ya wanawake
No comments:
Post a Comment