UBAKAJI
ELIMIKA NA SMAUJATA🇹🇿💪
Ubakaji ni Tendo la kutumia Nguvu Katika Ngono ambapo mbakaji anatumia Nguvu kutekeleza kitendo hicho. Ama ubakaji ni Ngono isiyo ya hiari.Kama mtu hayupo hiari na analazimishwa kufanya Hivyo hii inahesabiwa kama ubakaji hata kama anaekulazimisha ni rafiki, ndugu, jirani, mume au mtu usiyefahamiana nae.
Ingawa Kwa kawaida ubakaji unafanyika dhidi ya wanawake lakini unatokea pia dhidi ya wanaume mbali ya watoto na watu wenye Ulemavu wa akili wasio elewa kinachoendelea.
Ubakaji unaweza kutumiwa Nguvu ya mwili lakini pia mamlaka,vitisho na nitukio baya kabisa la kikatili Kwa nafsi ya mhanga na pengine Kwa afya yake linaloweza kumuathiri maisha yake yote kama si kusababisha kifo chake hasa likifanywa na watu kadhaa Kwa pamoja.
Matukio ya namna hiyo yanazidi kutokea hata ndani ya ukoo na mengi hayaripotiwi Kwa polisi,yakiwemo yanayotokea Magerezani kati ya watu wa jinsia Ile Ile.
Kwa vyovyote mara nyingi watu wanaobaka ni watu wanaojulikana sana na mhanga.Ubakaji hautokani na tamaa.
Matendo haya hayakubaliki iwe Serikalini,Magereza,Majumbani, kwenye jamii hata vitani,sheria za kimataifa haziruhusu matendo hayo ya kinyama na kikatili Vitani.
SABABU YA UBAKAJI
1.Ushirikina
Mara nyingi ubakaji unafanywa na mtu anaeambiwa na Waganga wa jadi Kwa lengo la Fulani,mfano Kubaka mtoto kama Njia ya kupona ukimwi,Kubaka mtu mwenye Ulemavu Kwa lengo la kupata Mali na Utajiri nk jambo ambalo si kweli na niukatili mkubwa sana.
2.Ulevi
Ulevi kupindukia hupelekea Mwanaume au mwanamke kufanya kitendo Cha ubakaji Kwa mfano baba kumbaka mtoto wake,ama mama kumbaka mtoto wake wakiume, yote hii nikutokana na kunywa pombe kupindukia na kutokujizuia mihemko iliyotokana na ulevi.
3.Mila zisizo faa
Baadhi ya makabila huamini kua mwanamke Hana kauli mbele za wanaume jambo ambalo kumpelekea mwanamke kulazimishwa kufanya kitendo Cha Ngono bila kuridhia kwani pale ambapo mwanaume anamuhitaji kiunyumba Naye bila ya kujiandaa nakujikuta alishaingiliwa pasi na kuridhia.
4.Maadili
Mmomonyoko wa maadili Kwa baadhi ya watoto wa kike na wakiume hupelekea mbakaji kufanya vitendo vya kibakaji ambapo,
Baadhi ya watoto wa kike kuvaa nguo zisizo kua za heshima Kisha kukatiza mbele ya wanaume hupelekea wanaume kupata mihemko na kumfanyia ubakaji binti alovaa vazi ilo lisilo na maadili.Pia wanaume kuvaa Nguo zisizo faa (mlegezo)jambo ambalo hupelekea kufanyiwa ubakaji.hata hivyo uvaaji wa nguo hizo Haina maana ya Moja kwa moja kua ndio chanzo Cha kufanyiwa ubakaji.
5:Wazazi kutosimamia malezi.
Hii huchangia kiasi Kikubwa Cha mtoto kufanyiwa ubakaji kwani wazazi siku izi wamekua wakiacha watoto muda mrefu Kwa madai yakua wanatafuta ridhki bila ya Kujua huku nyuma mtoto anafanyiwa Ukatili wa ubakaji na kupelekea mtoto kupata madhara makubwa sana.
MADHARA YA UBAKAJI
1:Kifo.
Ubakaji humfanya mhanga ajiuwe kwani huathirika kisaikolojia na Kuona Kwamba Hana Tena thamani kutokana na kitendo alicho fanyiwa
2:dharau Kwa wanawake
Mwanamke aliebakwa kudharauriwa na kushushwa uthamani wake hata baadae anapoitaji kuolewa Inapelekea kuonekana kwamba Hana thamani Kwa kubakwa kwake.
3:magonjwa ya zinaa,kama ukimwi,kaswende nk kwani mhanga hupata michubuko kutokana na kuingiliwa bila ridhaa yake Kwa Nguvu.
4:mimba zisizo Tarajiwa,
NINI KIFANYIKE KUKOMESHA UBAKAJI
1:Elimisha kizazi
Iwe Jukumu letu kuhamasisha wanawake wanaotetea haki za wanawake wa siku zijazo.pinga mitindo iliyokaririwa ya Kijinsia na maoni ya vurugu ambayo watoto kupatana nayo kwenye vyombo vya Habari,barabarani na mashuleni, watoto wako wajue kwamba familia yako ni nafasi salaama kwao kujielezea walivyo,sisitiza uamuzi wao uwafundishe umuhimu wa ridhaa ktk umri mdogo.
2:Anzisha mazungumzo na familia yako na marafiki kuhusu jinsi mnavyoweza kufanya kazi pamoja kumaliza utamaduni wa ubakaji Katika jamii zenu.
3:Usifurahie ubakaji
Ubakaji sio jambo la kuchekesha ,utani hivyo Jitahidi kutoharirisha unyanyasaji wa kijinsia hivyo kua ngumu Kwa waathirika kusema wakati idhini Yao inakiukwa.utani unaohalalisha dhuluma ya Kijinsia Haikubaliki kashifu.
4:Ubakaji unaoendelezwa na kutokuwepo au ukosefu wa utekelezaji wa sheria zinazoshughulikia Ukatili dhidi ya wanawake na sheria za kibaguzi ya umiliki Mali,ndoa,talaka na utunzaji wa watoto.
5.Wazazi tutenge muda wa kuwalea watoto wetu kwani Kwa kufanya Ivyo tutakua nao karibu na kuweza kuwapa elimu zaidi kwani mwalimu wakwanza Kwa mtoto nimzazi hivyo tupate muda wa kukaa na watoto wetu
KWA MSAADA ZAIDI YA WAHANGA WA UKATILI
Piga simu namba 116 Bure
Toa taarifa kwa Maafisa Ustawi,Dawati la jinsia, police,ofisi za Serikali ya mtaa,
Toa taarifa kwa Mashujaa wa maendeleo SMAUJATA
Mhanga akimbizwe hospital mara moja kwa ajili ya matibabu na Vipimo.
Imetayarishwa na
Mwamini Samaje
Idara ya Habari mawasiliano na Hamasa SMAUJATA Taifa
KATAA UKATILI WEWE NI SHUJAA💪🇹🇿
No comments:
Post a Comment