Tuesday, November 1, 2022

Global Peace Foundation waendelea kutoa elimu ya Amani Mikoa ya Kusini

 Global Peace Foundation waendelea kutoa elimu ya Amani Mikoa ya Kusini

Na Mwandishi Wetu

Shirika la Global Peace Foundation Tanzania Kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu -kazi vijana na Ajira, Chama cha Skauti Tanzania, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, GRCF na Vijana Wa Umoja wa mataifa (YUNA), kupitia program ya Vijana na amani255 inatoa mafunzo ya Amani Wilaya ya Nyasa yenye lengo la kuhamasisha ushiriki na ushirikishwaji wa Vijana katika Ujenzi wa Amani kwenye jamii.

Kaimu Mkuu wa wilaya ya Nyasa, Aziza Mangosongo, akitoa hotuba ya ufunguzi

Mafunzo haya yanatolewa katika Ukumbi wa Bay live mjini Mbamba bay Kwa Vijana, viongozi wa dini, Viongozi wa Utamaduni,wazazi walezi, Viongozi wa Serikali na Vijana.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh Aziza Mangosongo amewataka vijana na wananchi Kwa ujumla kuwa wazalendo na kudumisha Amani Kwa kufanya kazi Kwa juhudi, na kuilinda Amani Kwa kuwa Haina mbadala.


Mgeni rasmi, Kaimu Mkuu wa Wilaya katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo


Ameongeza kuwa wananchi wa nchi ya Tanzania hatuna sehemu nyingine tutakayoishi Kwa amani kama Tanzania, hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuijenga, kuilinda na kuitunza amani yetu.

Amelipongeza shirika Hilo Kwa kutoa mafunzo haya katika Wilaya ya Nyasa Kwa kuwa Wilaya hii inapakana na Nchi ya Msumbiji na Malawi hivyo ni elimu Muhimu.



Kwa upande wake Joseph Malekela, Afisa kutoka Global Peace Foundation, akizungumza kwaniaba ya  Mkurugenzi Mkaazi wa Global Peace Fouandation , Bi. Martha Nghambi alisema kwamba Mradi huo  unatekelezwa katika mikoa mitatu ya Kusini mwa nchi ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma chini ya ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), na kutekelezwa na wadau wenza ambao ni Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana, Kazi na watu wenye Ulemavu),  Chama cha Skauti Tanzania (TSA),  Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), na Shirika la Global Religions for Children Foundation (GRCF).

No comments:

Post a Comment