Saturday, November 18, 2023

WiLDAF conducts Gender Equality Training for Rafiki SDO

 

By Deogratius Koyanga, Shinyanga

The Women in Law and Development in Africa (WiLDAF) has conducted capacity-building training for the staff and management of Rafiki SDO in Shinyanga on how to incorporate gender issues into the organization's programs and overall structure.



These training sessions are part of a project funded by the Swedish International Development Agency (Sida) through Save the Children-Tanzania. The project aims to enhance the capacity of civil society organizations, strengthen institutional systems, and amplify the voices of children to discuss, self-manage, and demand their fundamental rights. The project is implemented in collaboration with WiLDAF, RAFIKI SDO, and five other partners.

Speaking at the training, Acting Executive Director of RAFIKI SDO, Tangi Clement, expressed gratitude to WiLDAF for providing gender experts to impart this knowledge. She emphasized that the training has opened their eyes to how they address gender issues as an institution and how the organization's programs target gender-related challenges in the community, especially among project beneficiaries.

"We are very grateful to WiLDAF for providing us with a Gender specialist for this session. We, as RAFIKI SDO, are still learning in the area of Gender, and this is a crucial opportunity that we have received. We will ensure to implement what we have learned, including extending this knowledge to other employees who did not participate and our stakeholders such as district councils for further awareness," said Tangi.

She added that during the workshop, they agreed that there is a need for a review of internal policies and human resources guidelines to create an enabling environment for pregnant women employees to have rest periods and dedicated spaces.

Additionally, they proposed that the review of the Gender policy should align with the inclusion of Gender Equality and Justice issues for people with disabilities and breastfeeding mothers, ensuring they receive full support while engaged in the organization's activities. "This will require policy changes, submission to management and the board for their approval, but it's a positive thing, and we believe they will agree," she added.



They also outlined a strategy to prioritize advocacy in district councils to allocate a gender Responsive Budget. This would enable girls to study and stay safe both within and outside of school, providing lunch meals at schools to reduce absenteeism and early pregnancies, constructing dormitories, and facilitating secondary school girls to access sanitary towels.



WiLDAF facilitator, Deogratius Temba, expressed the organization's hope that significant institutional changes would occur after the training. He highlighted the participants' commitment to putting effort into institutional changes so that everything within the organization reflects a gender perspective.

He added that the training led participants to agree on a review of RAFIKI SDO's gender policy for 2022 and its Strategic Plan (2020-2024) to focus on gender equality and allocate an internal budget to address gender-related challenges.

Eliud Mtalemwa, the Program Manager for Rafiki SDO in the Geita region, stated that the training helped the organization see itself more positively, recognizing how it manages gender issues and identifying gaps. He stressed the need to establish gender guidelines to govern and enforce gender-related decisions within the organization. "We have observed that women participate in our activities and decision-making positions, but we lack a guiding document that obliges us by numbers, specifying how many women should be in those positions. With the knowledge we have gained here, we will improve by revisiting our operational tools," said Mtalemwa.











 

WiLDAF yafanya mafunzo ya Usawa wa Kijinsia kwa Rafiki SDO


Na Deogratius Temba, Shinyanga

Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF),imefanya mafunzo ya kujenga uwezo kwa wafanyakazi  na Menejimenti ya Shirika la RAFIKI SDO la Shinyanga, namna ya kuingiza masuala ya Kijinsia katika Programu na muundo wa shirika kwa ujumla.

Wafanyakazi na Menejimenti ya Shirika la RAFIKI SDO  wakiwa pamoja na mwezeshaji baada ya mafunzo


Mafunzo haya ni sehemu ya mradi unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida) kupitia Save the Children-Tanzania, kwa lengo la kukuza uwezo wa asasi  za kiraia, kuimarisha mifumo ya kitaasisi na kuongeza sauti za watoto kujadili, kujisimamia  na kudai haki zao za msingi,unaotekelezwa kwa ushirikiano  na WILDAF, RAFIKI SDO na wadau wengine watano.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Tangi Clement, mafunzo hayo yamewafungua macho kujiangalia Zaidi kwa undani jinsi wanavyotekeleza masuala ya Kijinsia kama taasisi lakini pia namna ambavyo program na miradi ya shirika inavyolenga kutatua changamoto za kijinsia katika jamii hasa wanufaika wa miradi.

“ tunaishukuru sana WILDAF kwa kutupatia mtaalamu wa Jinsia kutupatia elimu hii, bado sisi kama RAFIKI SDO tunajifunza kwenye eneo la Jinsia, ni fursa muhimu sana ambayo tumeipata, tutahakikisha tunayafanyia kazi kikami,ifu ikiwepo kupeleka elimu hii kwa wafanyakazi ambao hawakushiriki, lakini pia wadau wetu kama Halmashauri za wilaya tutawapa elimu hii sambamba na wanufaika wetu” alisema Tangi.




Ameongeza kwamba katika warsha hiyo, wamekubaliana kwamba kunahitajika mapitio ya sera za ndani kama mapitio ya mwongozo wa rasilimali watu ili kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyakazi wenye ujauzito kupata muda wa kupumzika na iwepo sehemu maalum kwaajili hiyo.



Aidha wamependekeza kwamba, mapitio ya sera ya Jinsia yaende sambamba na kuingiza suala la Usawa na Haki kijinsia kwa watu wenye ulemavu na Mama aneyenyonyesha akiwa ndani shughuli za shirika kuhudumiwa yeye na mtoto wake kikamilifu. “ Hii itahitaji mabadiliko ya kisera, kuwasilisha kwa manajimenti na bodi ili kupata Baraka zao, lakini ni jambo nzuri tuna Imani watatusikiliza”aliongeza.

Pia, waliweka mkakati wa kuweka uzito katika uchechemuzi kwenye Halmashauri za wilaya ili kutenga bajeti yenye mrengo wa Kijinsia aitakayowezesha watoto wa kike kusoma na kuwa salama ndani nan je ya shule kama kupata mlo wa chakula cha mchana shuleni ili kupunguza utoro na mimba za utotoni, kujenga mabweni na kuwezesha wasichana wa shule za sekondari kupatia taulo za kike.



Naye mwezeshaji kutoka WiLDAF, Deogratius Temba, amesema kwamba, WiLDAF inamatumaini kwamba, baada ya mafunzo hayo, mabadiliko makubwa ya kitaasisi yatatokea kwani washiriki wameweka ahadi (commitiment) ya kuweka nguvu kwenye mabadiliko ya kitaasisi ili  kila kitu kinachofanyika ndani ya shirika kiweze kuwa na mtazamo wa Kijinsia.

Ameongeza kwamba, mafunzo haya yamepelekea washiriki kukubaliana kupitia upya sera ya jinsia ya Rafiki SDO ya mwaka 2022, na Mpango Mkakati wake wa (2020-2024) ili kuweza kuzingatia usawa wa Kijinsia na kuweka bajeti ya ndani ya Taasisi itakayotatua changamoto wa Kijinsia.

“Sisi tuna Imani, kama walivyosema washiriki hawa wa RAFIKI SDO, Baada yam waka mmoja tukirudi hapa kutakuwa na mabadiliko makubwa” amesema Temba.

Kwa upande wake Programu Meneja wa Rafiki SDO Mkoa wa Geita, Eliud Mtalemwa alisema kwamba mafunzo haya yameisaidia taasisi kujiona vizuri Zaidi, kutambua namna inavyosimamia masuala ya Kijinsia na mapengo yalipo kwani  inahitaji kuweka miongozo ya Kijinsia itakayowasimamia.  “tumeona kwamba, wanawake wanashiriki kwenye shughuli zetu na kwenye nafasi za maamuzi lakini hatuna kitu kinachotuongoza na kutulazimisha kwa namba, kwamba wanawake wawe wangapi kwenye hizo nafasi, kwa elimu tuliyopipata hapa,tumefunguka, tutaboresha kwa kupitia upya nyenzo zetu za kiutendaji. “ alisema Mtalemwa.









Monday, November 13, 2023

WILDAF Conducts Gender Mainstreaming Training for Forum CC Staff

By- Our Reporter in Dodoma

The Women in Law & Development in Africa (WILDAF) conducted a capacity-building training for the staff of the Climate Change Forum (Forum CC) to integrate gender issues into the organization's programs and structures. 


Participants in a group photo after the day one session


 This training is part of a broader project funded by the Sida through Save the Children aimed at strengthening organizational capacity, enhancing institutional structures, and amplifying the voices of children to discuss, advocate for, and assert their fundamental rights, particularly in the realm of climate change. The joint initiative is being implemented by WILDAF, Forum CC and 5 other consortium partners.  



During the training conducted by WiLDAF, Forum CC Executive Director, Sarah Ngoy, highlighted the significance of the workshop in the context of a gender gap identified within the organization during a capacity assessment conducted in 2022. She emphasized the need for capacity-building among staff to ensure gender responsiveness in programs and advocated for systemic changes to address gender equality issues comprehensively.

Deogratius Temba, a facilitator from WiLDAF


Ngoy expressed gratitude for the insights gained through the training and outlined specific areas for improvement. These include making budgets gender-responsive, increasing training for staff, allocating a budget for sanitary pads for female employees, providing a resting room for pregnant mothers, and revising financial guidelines to cover costs for assistants to breastfeeding women and assistants of people with disabilities.

Post-training, the organization plans to conduct a thorough review of internal policies and guidelines, including the human resources policy, to align them with the organization's gender policy. Ngoy announced the development of a gender implementation plan scheduled to commence in 2024.

Deogratius Temba, the facilitator from WILDAF, expressed optimism regarding the potential for significant institutional changes following the training. He highlighted the participants' commitment to contributing to institutional change, ensuring that all activities within the organization become gender-responsive.








WiLDAF yafanya mafunzo ya Usawa wa Kijinsia kwa Forum CC

Na Deogratius Temba, Dodoma

 Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF),imefanya mafunzo ya kujenga uwezo kwa wafanyakazi wa Jukwaa la Mabadiliko ya tabia nchi (Forum CC), ili kuweza kuingiza masuala ya Kijinsia katika Programu na muundo wa shirika kwa ujumla.
Washiriki wa Mafunzo ya Jinsia, ambao ni wafanyakazi wa FORUM CC wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo, na Mwezeshaji kutoka WiLDAF, Deogratius Temba

Mafunzo hayo, ambayo ni sehemu ya mradi wa kukuza uwezo wa asasi za kiraia, kuimarisha mifumo ya kitaasisi na kuongeza sauti za watoto kujadili, kujisimamia na kudai haki zao za msingi hasa katika eneo la Mabadiliko ya tabia nchi, unaotekelezwa na WILDAF na Forum CC.
Majadiliano wakati wa warsha ya Jinsia iliyowezeshwa na WiLDAF  
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Forum CC, Sarah Ngoy, amesema kwamba, mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo, ambapo mwaka jana 2022, taasisi hiyo ilifanya zoezi la kupima uwezo wake katika masuala ya Kijinsia na kuonekana kwamba kuna pengo kwenye eneo la usawa wa Kijinsia ndani ya taasisi.
Mwezeshaji akisisitiza Jambo wakati wa warsha ya Uingizwaji wa masuala ya Kijinsia kwenye Taasisi, iliyofanywa na WiLDAF kwa Forum CC

“warsha hii kwa wafanyakazi wetu imekuja kwa wakati muafaka, mwaka jana tulipofanya zoezi la kujipima kama taasisi tuliona hili pengo la kijinsia ndani ya shirika, tukagundua kwamba pamoja na kuhitaji kujenga uwezo kwa wafanyakazi wetu kwenye masuala ya Kijinsia, ili kuzifanya program zetu ziwe na mtazamo wa Kijinsia, pia tulihitaji mabadiliko ya kimfumo, sambamba na kuongeza uelewa na maarifa ya masuala ya kijinsia kwa timu yetu yote”alisema Sarah na kuongeza: “Warsha hii imetufungua macho sana, kumbe bado tuna pengo la masuala ya kijinsia, kumbe tunahitaji kufanya mabadiliko na maboresho ya bajeti zetu ziweze kuwa na mtazamo wa kijinsia, kupitia mafunzo haya tumegundua kwamba tunatakiwa kuongeza mafunzo kwa wafanyakazi, kuweka bajeti kwaajili ya taulo za kike kwa wafanyakazi, kuweka chumba cha kupumzika mama wajawazito wanapokuwa ndani ya shirika letu, na pia kubadilisha mwongozo wa fedha ili kuruhusu kuwalipia gharama wasaidizi wa wanawake wanaonyonyesha na wasindikizaji wa watu wenye ulemavu” alisema Sarah.
Wafanyakazi wa Forum CC wakifuatilia warsha

Ameongeza kwamba, mara baada ya mafunzo hayo, taasisi hiyo itakaa na kupitia upya sera za ndani ya shirika na miongozo mbalimbali ukiwemo ule wa rasilimali watu ili uweze kuendana na sera ya Jinsia ya Taasisi sambamba na kuwa na mpango wa utekelezaji wa masuala ya Kijinsia kwa taasisi utakaoanza kutekelezwa mwaka 2024. Naye mwezeshaji kutoka WiLDAF, Deogratius Temba, amesema kwamba, WiLDAF
Mwezeshaji, Deogratius Temba, akisisitiza mabadiliko ya Kitaasisi kwa mtazamo wa Kijinsia, wakati wa mafunzo ya Jinsia kwa wafanyakazi wa Forum CC

inamatumaini kwamba, baada ya mafunzo hayo, mabadiliko makubwa ya kitaasisi yatatokea kwani washiriki wameweka ahadi (commitiment) ya kuweka nguvu kwenye mabadiliko ya kitaasisi ili kila kitu kinachofanyika ndani ya shirika kiweze kuwa na mtazamo wa Kijinsia.


Tuesday, November 7, 2023

Miaka 30 ya TGNP: Tanzania kinara utekelezaji wa maazimio ya Beijing

 

na Deogratius Temba

Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini, Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka,  amesema T
anzania inaongoza katika kutekeleza maazimio ya Mkutano wa nne wa wanawake duniani uliofanyika Beijing Nchini china mwaka 1995.

Mgeni wa Heshima katika tamasha la Jinsia la 15, Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini, Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka



Akizungumza wakati wa sherehe za ufunguzi wa Tamasha la Jinsia la 15,  na miaka 30 ya ya Mtandao wa Jinsia Tanznaia (TGNP), Mhe. Phunzile ambaye amekuwa pia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linaloshughulikia masuala la Wanawake (UNwomen),  ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema kwamba, Mkutano wa Bijing uliofanyika miaka 28 uliweka maazimio ambayo Tanzania imeendelea kufanya vizuri kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na nchi nyingine.



“Kwa uelewa wangu wa kufanya kazi katika ngazi ya kimataifa, ninaweza kuona mchango wa TGNP katika kujenga uwezo kwa wanawake wa Tanzania kufanya uchambuzi wa masuala ya Kijinsia, ni nchi ya Kolombia na Tanzania pekee ambazo wanawake wamejenga uwezo kwa kiasi kikubwa wa kiuchamnganuzi na kiuchambuzi kuhusu masuala ya Kijinsia.” Alisema na Kuongeza kwamba



“Mkutano wa Beijing uliipa Tanzania heshima kubwa Zaidi, ukizingatia kwamba uliongeozwa na Mtanzania ambaye aliweka historia ambayo haitasahaulika duniani kwakuwa mkutano ule ulizaaa maazimio amzito kabisa ambayo yamesababisha mageuzi wa kimifumo, kisera na kisheria katika mtataifa mbalimbali lakini pia maazimio yale yamepelekea kuongeza vuguvugu la harakati hizi kuanzia ngazi ya jamii hadi kitaifa, na sasa kuna misamiati mingi ya kukomboa wanawake…”



Aliongeza kwamba, dunia itaendelea kuikumbuka Tanzania kwa kile kilichotokea Beijing, chini ya uongozi wa Balozi Getrude Mongela, ambapo hata hivyo nchi inaongoza kwa kuwa na sera zenye mtazamo wa Kijinsia ikiwepo mabadiliko ya kisheria na kimwongozo.

Kwa  upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa UNWomen Tanzania,  akitoa salaam, alisema kwamba Changamoto za mapengo ya usawa wa Kijinsia bado zipo, ikiwepo Ukatili wa Kijinsia, lakini  kunahitajika nguvu ya mapoja na mshikamano wa mashirika mbalimbali ili kutokomeza kabisa vitendo vya Ukatili wa Kiinsia.



“tusipofanya jitihada za ziada, itachukua Zaidi ya miaka 300 kufikia usawa wa Kijinsia, tunahitaji kujipanga, kushikamana, kuwahusisha wanawake na wanaume kwa umoja wao ili kuzuia mabaya yote ambayo wanawake na watoto wa kike na kiume wanatendewa” alisema Odan.



Awali alitoa hotuba yake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi alisema kwamnba, Tamasha linatoa fursa ya wana jamii hususan wanawake kushirikishana uzoefu, kujadili, kujifunza, kujenga ajenda ya pamoja kuhusu usawa wa jinsia na maendeleo hususani ya namna ya kupanga mikakati ya pamoja ili kusonga mbele kwa pamoja.



“Tunaposheherekea mafanikio ya harakati zetu kwa miaka 30 ya uwepo wa TGNP, hatuna budi kuipongeza serikali kwa kukubali maoni na mapendekezo kadhaa mbayo tumekuwa tukipelekea na haya ndio yamesababisha Tanzania kuonekana kwamba imetekeleza kwa kiasi kikubwa maazimio ya Beijing…” alisema Lilian.  



Friday, October 27, 2023

Viti Maalum vifutwe- Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi


Na Deogratius Temba

 

Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uongozi na Uchaguzi, ambao wamekuwa wakidai na kushawishi mabadiliko ya kisera, kisheria na kimuundo ili kutoa nafasi sawa kwa wanawake kushiriki kwenye nafasi za uongozi katika nyanja mbalimbali wametoa msimamo wao juu ya uwepo wa Viti Maalum katika nafasi za uongozi wa kisiasa.

Wawakilishi wa Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uongozi na Uchaguzi, wakiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam, wakati akiwa Makamu wa Rais. (Picha na Maktaba yetu)


Mara baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuteua Kikosi Kazi cha kukusanya maoni na kuyachakata juu ya namna ya kukuza Demokrasiasa nchini, Kikosi kazi ilichofanya kazi chini ya Uenyekiti wa Prof. Rwekaza Mkandala,  pamoja na kwamba Mtandao waliwasilisha maoni yao kwa kikosi kazi, moja ya pendekezo lao kama msimamo ni kuhusu muundo wa Viti maalum vya Ubunge, udiwani na Halmashauri za Vijiji na Kamati za Mitaa unaotumika hivi sasa.

Wanamtandao wa Wanawake, Katiba, Uongozi na Uchaguzi ni muunganiko wa asasi za kiraia zaidi ya 200 ulioanzishwa mwaka 2011, ulishauri kwamba mfumo wa Viti Maalum uliopo sasa ufutwe katika ngazi zote za uongozi.  Kwa mantiki hiyo, kusiwepo na Viti Maalum vya wanawake.

Katika Mapendekezo ya Mtandao, wanasema kwamba: “ Licha ya kwamba, wadau walishauri kuondolewa kwa mfumo wa Viti Maalum, Kikosi Kazi kiliamua Mfumo wa Viti Maalum uendelee bila kutoa sababu za msingi za kuendeleza huu mfumo” inaeleza sehemu ya Taarifa ya Mapendekezo ya Mtandao wa wanawake na Katiba na kuongeza kuwa:

“Kikosi Kazi kilipendekeza kwamba, Wabunge wa Viti Maalum waitwe Wabunge wa Taifa na Madiwani waitwe Madiwani wa Wilaya. Vile vile Kikosi Kazi kilipendekeza Sheria ya Mfuko wa Uchaguzi ibadilishwe ili Wabunge wa Viti Maalum wafaidike nao kama Wabunge walioteuliwa kwa kupitia majimbo ya Uchaguzi. Na kwamba kuweko kwa mwongozo wa kisheria wa uteuzi wa wagombea na uchaguzi wa viongozi ndani ya Vyama vya Siasa ikiwemo wabunge wa Viti Maalum ili kusaidai uteuzi na uchaguzi wa haki na huru” pendekezo hili la Kikosi kazi, Mtandao unalikataa.

Mtandao wa wanawake na Katiba hawakubaliani pia  na maoni ya Kikosi kazi kwamba;  mfumo wa viti maalum uliopo sasa uendelee kutumika kama njia ya kupata uzoefu na kisha kupisha wanawake wengine wenye nia ya kuongeza uzoefu na ujuzi wa masuala ya siasa,

“ Kwetu sisi Wanamtandao wa Wanawake, Katiba, Uongozi na Uchaguzi, tunaona pendekezo la kuendeleza Viti Maalum ambavyo sisi kama wadau tunaoathirika na mfumo huu uliopo ambao tunaona umejaa ubaguzi na udhalilishaji wa Kijinsia, tunashauri ubadilishwe au kuondolewa kabisa” inasema sehemu ya Mapandekezo ya Mtandao.

 

Lakini pia, wanamtandao wa wanawake Katiba, Uongozi na Uchaguzi, wanasema kwamba,  kuendeleza mfumo wa Viti Maalum wa sasa ni kuijengea jamii Imani kwamba, wanawake bado hawana uwezo, uzoefu, wala ujuzi wa masuala ya siasa, na kwamba  wengi ikiwa ni pamoja na hao walioko kwenye uwanda wa siasa tayari, kwamba wanahitaji takriban miaka kumi ya kujenga uwezo huo ili kuwapisha wengine wanaowania kuingia kwenye uwanda wa siasa.

 

Ni muhimu kujenga fikra chanya kuhusu uwezo wa wanawake, na pia kutokuwaunganisha kwenye kapu moja na Makundi Maalum. Wanawake sio wote ni makundi maalum kwa sababu hata wanaume baadhi yao wapo kwenye kundi maalum.

 

Tafsiri ya Mtandao wa wanawake, Katiba Uongozi na Uchaguzi juu ya kuendeleza mfumo wa Viti Maalum, ni la kuturudisha nyuma, na kupuuza hazina ya ujuzi, uwezo  ulioko miongoni wa wanawake wengi kwenye masuala ya siasa na uongozi.

 

Nchi yetu inatakiwa kuweka mazingira salama, wezeshi na kuondoa vikwazo kwenye michakato ya uchaguzi ili kuwapa nafasi wanawake washindane na wanaume. Tunapoelekea kwenye chaguzi za serikali za Mitaa mwaka 2024, ni muhimu kuanza kujiandaa kuweka mifumo rafiki ya uchaguzi kwa wanawake ili wagombee na wanaume, na wapigiwe kura ambazo sio za huruma au za kupewa kwa sababu wao ni wanawake.

Ili kushughulikia usawa wa kijinsia katika uongozi, serikali ilifanya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka za Serikali za Wilaya (1982) na marekebisho Na.4 ya mwaka 2000 katika kifungu cha 35 ili kuanzisha jitihada za makusudi za kuongeza uwakilishi wa wanawake katika serikali za mitaa ambapo wanawake wanapaswa kufikia theluthi moja ya wajumbe wa mabaraza.

 

Katika ngazi ya kijiji, wanawake wanapaswa kuwa asilimia 25 ya wajumbe wa Halmashauri ya kijiji ambayo kwa kawaida ina wajumbe 15 hadi 25. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa asilimia 30 ya viti maalum kwa wanawake Bungeni na asilimia 33.3 ya viti maalum katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Ingawa mafanikio makubwa yamepatikana, Serikali bado haijafikia lengo la Umoja wa Afrika la usawa wa kijinsia wa 50/50.

Tuesday, October 24, 2023

AZAKI zajadili Tekonolojia na Usawa wa Kijinsia


Na deogratius Temba, Arusha

ASASI za zimejadili namna ambavyo ni vigumu kutenganisha mabadiliko ya Sayansi na Tekonolojia na Usawa wa Kijinsia kwa maendeleo endelevu.




Akizungumza, wakati wa ufunguzi wa Wiki ya AZAKI nchini inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimatifa (AICC) Jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Asasi za Kiraia (FCS), Francis Kiwanga alisema kwamba jamii haiwezi kukwepa kwenda sambamba na mabdiliko ya sayansi na Teknolojia ikiwepo kulinda na kuheshimu haki za Binadamu na usawa wa kijinsia.  



“mwaka huu tunakutana hapa, Zaidi ya AZAKI 500, mijadala yetu yote itajikita katika kujadili, Tekonolojia na Jamii, wapi tumetoka, Tulipo, na tunapokwenda. Tusigope, mabadiliko ni makubwa sana, kasi ya mabadiliko haikwepeki” alisema Kiwanga na Kuongeza:

“Miaka ya 2000, watu waliogopa sana, walifikiri, ujio wa komputa utafuta ajira zote, makatibu muhutasi walifikiri hawatakuwepo tena na wataondoka, lakini hadi leo wao..”




Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ni moja ya wadau wanaoshiriki Mkutano huo,pia ni wajumbe wa Kamati ya Maandalizi, na watatoa mada  na kujenga mjadala juu ya Ubunifu wa Kiteknolojia kama chachu ya Usawa wa Kijinsia.



Katika warsha hiyo ya TGNP pia watakuwepo wadau muhimu ambao ni Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT) ambao wanafunzi wa kike watapata nafasi ya kuonesha mashine walizotengeneza zinazolenga kupunguza gharama za matibabu kwa jamii 

TGNP,DIT waendesha majadala wa Usawa wa Kijinsia katika Tekonolojia

Na Mwandishi Wetu, Arusha #CSOWEEK2023 

 Wadau wamatakiwa kondoa hofu na mabadiliko ya Sayansi na kiteknolojia katika utendaji wa shughuli za kila siku ili kupunguza gharama za uendeshaji na uzalishaji.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Ushawishi na Utetezi (TGNP), Florah Ndaba, akitoa maelezo wakati wanafunzi wa Chuo cha DIT wakielezea Mashine za kusaidia kupumua walizotengeneza. 

Hayo yameibuka kwenye mjadala ulioendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika, uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafssi, serikalini, wanazuoni na asasi za kiraia, katika wiki ya AZAKI #WIKIYAAZAKI2023 inayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) Jijini Arusha, ambapo pamoja na mengine, ujumbe mkuu ulikuwa ni ubunifu na Teknolojia kama chachu ya usawa wa Kijinsia.
Mwezeshaji kutoka TGNP akitoa maelezo ya awali juu ya ubunifu wa wasichana katika Sayansi na Tekonolojia ili kutatua changamoto za Jamii

Akizungumza wakati wa jopo, Kaimu Mkuu wa Idara ya Ushawishi na Utetezi, TGNP Florah Ndaba alisema kwamba, Jamii haipaswi kuogopa wala kuwa na hofu juu ya ukoaji wa teknolojia badly ni kuangalia, teknolojia isitumike bibaya kuongeza Ukatili na udhalilishaji wa Kijinsia au kuongeza tofauti za kiuchumi kati ya wanawake na wanaume.

 “Teknolojia, inapunguza gharama za utendeshaji na uzalishaji, Ndio maana TGNP tuliingia makubaliano ya DIT kusaidiana katika kuendeleza kuhakikisha jitihada za ubinifu wa kisayansi zinazofanywa na DIT zinazingatia usawa wa Kijinsia lakini pia wasichana wanaochagua fani za sayansi na tknolojia wanapata nafasi na kulelewa vipaji vyao hadi waingie kwenye soko la ajira” alisema Flora Naye Mwanajopo mtaalamu na Mchambuzi wa Masuala ya Kijinsia Deogratius Temba, alisema kwamba, kukosekana kw a usawa wa Kijinsia katika teknolojia kunaikosesha nchi fedha nyingi ambazo zingepatikana kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji.
Wana jopo mara baada ya Mjadala Wanafunzi wa Chuo cha DIT na Mkufunzi wao na Timu kutoka TGNP

 “ Utafiti uliofanywa na UNwomen kwa nchi 51 mwaka 2022, umeeleza kwamba, nchi za uchumi wa chini na Kati ambazo hakuna usawa wa Kijinsia katika Teknolojia zinapoteza Dola za Kimarekani Trilion 1 kila mwaka, na ifikapo mwaka 2025, zitapoteza Zaidi ya dola za kimarekani Trilion 1.5. Ukiangalia hii ni kwamba, Usawa wa Kijinsia kwenye eneo la Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati hauepukiki” alisema Temba.


 Aidha, akizungumza Mkufunzi kutoka Taasisi ya Tekonolojia Dar es salaam, (DIT), Nizentha Kimario, alisema kwamba DIT imekuwa na mtazamo wa Kijinsia, mahusiano yake na TGNP yamesaidia pia kujenga uelewa wa masuala ya Kijinsia na kubadili mitazamo hasi juu ya uwezo wa wasichana katika fani za sayansi na Teknolojia, lakini pia kwamba wanafunzi wanaona umuhimu wa kwenda kwenye jamii kuangalia changamoto na mahitaji yao kabla ya kuanza kufanya ubunifu. 





 “utaona kwamba, mashine nyingi za kibunifu tumebuni kutokana na mahitaji ya jamii. Wanafunzi wetu baada ya kuona kuna changamoto ya gharama kubwa ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo ndio walikuja na mashine hii hapa, lakini pia kuna gharama kubwa kwenye kutunza na kuwawekea dawa watoto wenye changamoto ya kupumua hasa arthima, ndio maana vijana wetu tena wasichana wamebuni hii mashine..” alisema Kimario. Sambamba na mijadala huo, wanafunzi kutika Chuo cha DIT walionesha mashine mbalimbali ambazo zimebuniwa na wanafunzi, na Pikipiki ya magurudumu matatu (Bajaji) yenye uwezo wa kubeba abiria saba (7) na Dereva ambayo inatumia nishati ya Betri la kuchaji. Wiki ya AZAKI 2023 inayoratibiwa na Mfuko wa Asasi za Kiraia (FCS), imeanza Oktiba 23 hadi 27 2023 jijini Arusha ikiwa imewahusisha wakurugenzi, wafanyakazi na wadau mbalimbali wa asasi za kiraia Zaidi ya 500, wadau wa maendeleo, wataalamu kutoka serikalini na wanajamii ambao wananufaika na rasilimali na kazi za AZAKI.