Na Deogratius Temba, Shinyanga
Shirika la Wanawake katika Sheria
na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF),imefanya mafunzo ya kujenga uwezo kwa
wafanyakazi na Menejimenti ya Shirika la
RAFIKI SDO la Shinyanga, namna ya kuingiza masuala ya Kijinsia katika Programu
na muundo wa shirika kwa ujumla.
![]() |
Wafanyakazi na Menejimenti ya Shirika la RAFIKI SDO wakiwa pamoja na mwezeshaji baada ya mafunzo |
Mafunzo haya ni sehemu ya mradi
unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida) kupitia Save the
Children-Tanzania, kwa lengo la kukuza uwezo wa asasi za kiraia, kuimarisha mifumo ya kitaasisi na
kuongeza sauti za watoto kujadili, kujisimamia
na kudai haki zao za msingi,unaotekelezwa kwa ushirikiano na WILDAF, RAFIKI SDO na wadau wengine
watano.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Tangi Clement, mafunzo hayo yamewafungua
macho kujiangalia Zaidi kwa undani jinsi wanavyotekeleza masuala ya Kijinsia kama
taasisi lakini pia namna ambavyo program na miradi ya shirika inavyolenga
kutatua changamoto za kijinsia katika jamii hasa wanufaika wa miradi.
“ tunaishukuru sana WILDAF kwa
kutupatia mtaalamu wa Jinsia kutupatia elimu hii, bado sisi kama RAFIKI SDO
tunajifunza kwenye eneo la Jinsia, ni fursa muhimu sana ambayo tumeipata,
tutahakikisha tunayafanyia kazi kikami,ifu ikiwepo kupeleka elimu hii kwa
wafanyakazi ambao hawakushiriki, lakini pia wadau wetu kama Halmashauri za
wilaya tutawapa elimu hii sambamba na wanufaika wetu” alisema Tangi.
Ameongeza kwamba katika warsha
hiyo, wamekubaliana kwamba kunahitajika mapitio ya sera za ndani kama mapitio
ya mwongozo wa rasilimali watu ili kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyakazi
wenye ujauzito kupata muda wa kupumzika na iwepo sehemu maalum kwaajili hiyo.
Aidha wamependekeza kwamba,
mapitio ya sera ya Jinsia yaende sambamba na kuingiza suala la Usawa na Haki kijinsia
kwa watu wenye ulemavu na Mama aneyenyonyesha akiwa ndani shughuli za shirika
kuhudumiwa yeye na mtoto wake kikamilifu. “ Hii itahitaji mabadiliko ya kisera,
kuwasilisha kwa manajimenti na bodi ili kupata Baraka zao, lakini ni jambo
nzuri tuna Imani watatusikiliza”aliongeza.
Pia, waliweka mkakati wa kuweka
uzito katika uchechemuzi kwenye Halmashauri za wilaya ili kutenga bajeti yenye
mrengo wa Kijinsia aitakayowezesha watoto wa kike kusoma na kuwa salama ndani nan
je ya shule kama kupata mlo wa chakula cha mchana shuleni ili kupunguza utoro
na mimba za utotoni, kujenga mabweni na kuwezesha wasichana wa shule za
sekondari kupatia taulo za kike.
Naye mwezeshaji kutoka WiLDAF, Deogratius Temba, amesema kwamba, WiLDAF inamatumaini kwamba, baada ya mafunzo hayo, mabadiliko makubwa ya kitaasisi yatatokea kwani washiriki wameweka ahadi (commitiment) ya kuweka nguvu kwenye mabadiliko ya kitaasisi ili kila kitu kinachofanyika ndani ya shirika kiweze kuwa na mtazamo wa Kijinsia.
Ameongeza kwamba, mafunzo haya
yamepelekea washiriki kukubaliana kupitia upya sera ya jinsia ya Rafiki SDO ya
mwaka 2022, na Mpango Mkakati wake wa (2020-2024) ili kuweza kuzingatia usawa
wa Kijinsia na kuweka bajeti ya ndani ya Taasisi itakayotatua changamoto wa
Kijinsia.
“Sisi tuna Imani, kama
walivyosema washiriki hawa wa RAFIKI SDO, Baada yam waka mmoja tukirudi hapa
kutakuwa na mabadiliko makubwa” amesema Temba.
Kwa upande wake Programu Meneja
wa Rafiki SDO Mkoa wa Geita, Eliud Mtalemwa alisema kwamba mafunzo haya yameisaidia
taasisi kujiona vizuri Zaidi, kutambua namna inavyosimamia masuala ya Kijinsia
na mapengo yalipo kwani inahitaji kuweka
miongozo ya Kijinsia itakayowasimamia. “tumeona
kwamba, wanawake wanashiriki kwenye shughuli zetu na kwenye nafasi za maamuzi
lakini hatuna kitu kinachotuongoza na kutulazimisha kwa namba, kwamba wanawake
wawe wangapi kwenye hizo nafasi, kwa elimu tuliyopipata hapa,tumefunguka,
tutaboresha kwa kupitia upya nyenzo zetu za kiutendaji. “ alisema Mtalemwa.
No comments:
Post a Comment