Monday, November 13, 2023

WiLDAF yafanya mafunzo ya Usawa wa Kijinsia kwa Forum CC

Na Deogratius Temba, Dodoma

 Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF),imefanya mafunzo ya kujenga uwezo kwa wafanyakazi wa Jukwaa la Mabadiliko ya tabia nchi (Forum CC), ili kuweza kuingiza masuala ya Kijinsia katika Programu na muundo wa shirika kwa ujumla.
Washiriki wa Mafunzo ya Jinsia, ambao ni wafanyakazi wa FORUM CC wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo, na Mwezeshaji kutoka WiLDAF, Deogratius Temba

Mafunzo hayo, ambayo ni sehemu ya mradi wa kukuza uwezo wa asasi za kiraia, kuimarisha mifumo ya kitaasisi na kuongeza sauti za watoto kujadili, kujisimamia na kudai haki zao za msingi hasa katika eneo la Mabadiliko ya tabia nchi, unaotekelezwa na WILDAF na Forum CC.
Majadiliano wakati wa warsha ya Jinsia iliyowezeshwa na WiLDAF  
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Forum CC, Sarah Ngoy, amesema kwamba, mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo, ambapo mwaka jana 2022, taasisi hiyo ilifanya zoezi la kupima uwezo wake katika masuala ya Kijinsia na kuonekana kwamba kuna pengo kwenye eneo la usawa wa Kijinsia ndani ya taasisi.
Mwezeshaji akisisitiza Jambo wakati wa warsha ya Uingizwaji wa masuala ya Kijinsia kwenye Taasisi, iliyofanywa na WiLDAF kwa Forum CC

“warsha hii kwa wafanyakazi wetu imekuja kwa wakati muafaka, mwaka jana tulipofanya zoezi la kujipima kama taasisi tuliona hili pengo la kijinsia ndani ya shirika, tukagundua kwamba pamoja na kuhitaji kujenga uwezo kwa wafanyakazi wetu kwenye masuala ya Kijinsia, ili kuzifanya program zetu ziwe na mtazamo wa Kijinsia, pia tulihitaji mabadiliko ya kimfumo, sambamba na kuongeza uelewa na maarifa ya masuala ya kijinsia kwa timu yetu yote”alisema Sarah na kuongeza: “Warsha hii imetufungua macho sana, kumbe bado tuna pengo la masuala ya kijinsia, kumbe tunahitaji kufanya mabadiliko na maboresho ya bajeti zetu ziweze kuwa na mtazamo wa kijinsia, kupitia mafunzo haya tumegundua kwamba tunatakiwa kuongeza mafunzo kwa wafanyakazi, kuweka bajeti kwaajili ya taulo za kike kwa wafanyakazi, kuweka chumba cha kupumzika mama wajawazito wanapokuwa ndani ya shirika letu, na pia kubadilisha mwongozo wa fedha ili kuruhusu kuwalipia gharama wasaidizi wa wanawake wanaonyonyesha na wasindikizaji wa watu wenye ulemavu” alisema Sarah.
Wafanyakazi wa Forum CC wakifuatilia warsha

Ameongeza kwamba, mara baada ya mafunzo hayo, taasisi hiyo itakaa na kupitia upya sera za ndani ya shirika na miongozo mbalimbali ukiwemo ule wa rasilimali watu ili uweze kuendana na sera ya Jinsia ya Taasisi sambamba na kuwa na mpango wa utekelezaji wa masuala ya Kijinsia kwa taasisi utakaoanza kutekelezwa mwaka 2024. Naye mwezeshaji kutoka WiLDAF, Deogratius Temba, amesema kwamba, WiLDAF
Mwezeshaji, Deogratius Temba, akisisitiza mabadiliko ya Kitaasisi kwa mtazamo wa Kijinsia, wakati wa mafunzo ya Jinsia kwa wafanyakazi wa Forum CC

inamatumaini kwamba, baada ya mafunzo hayo, mabadiliko makubwa ya kitaasisi yatatokea kwani washiriki wameweka ahadi (commitiment) ya kuweka nguvu kwenye mabadiliko ya kitaasisi ili kila kitu kinachofanyika ndani ya shirika kiweze kuwa na mtazamo wa Kijinsia.


No comments:

Post a Comment