na Deogratius Temba
Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika
ya Kusini, Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka, amesema T
anzania inaongoza katika kutekeleza
maazimio ya Mkutano wa nne wa wanawake duniani uliofanyika Beijing Nchini china
mwaka 1995.
![]() |
Mgeni wa Heshima katika tamasha la Jinsia la 15, Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini, Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka |
Akizungumza wakati wa sherehe za
ufunguzi wa Tamasha la Jinsia la 15, na miaka
30 ya ya Mtandao wa Jinsia Tanznaia (TGNP), Mhe. Phunzile ambaye amekuwa pia
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linaloshughulikia masuala la Wanawake (UNwomen), ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema kwamba,
Mkutano wa Bijing uliofanyika miaka 28 uliweka maazimio ambayo Tanzania
imeendelea kufanya vizuri kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na nchi nyingine.
“Kwa uelewa wangu wa kufanya kazi
katika ngazi ya kimataifa, ninaweza kuona mchango wa TGNP katika kujenga uwezo
kwa wanawake wa Tanzania kufanya uchambuzi wa masuala ya Kijinsia, ni nchi ya
Kolombia na Tanzania pekee ambazo wanawake wamejenga uwezo kwa kiasi kikubwa wa
kiuchamnganuzi na kiuchambuzi kuhusu masuala ya Kijinsia.” Alisema na Kuongeza
kwamba
“Mkutano wa Beijing uliipa
Tanzania heshima kubwa Zaidi, ukizingatia kwamba uliongeozwa na Mtanzania
ambaye aliweka historia ambayo haitasahaulika duniani kwakuwa mkutano ule
ulizaaa maazimio amzito kabisa ambayo yamesababisha mageuzi wa kimifumo, kisera
na kisheria katika mtataifa mbalimbali lakini pia maazimio yale yamepelekea kuongeza
vuguvugu la harakati hizi kuanzia ngazi ya jamii hadi kitaifa, na sasa kuna
misamiati mingi ya kukomboa wanawake…”
Aliongeza kwamba, dunia
itaendelea kuikumbuka Tanzania kwa kile kilichotokea Beijing, chini ya uongozi
wa Balozi Getrude Mongela, ambapo hata hivyo nchi inaongoza kwa kuwa na sera
zenye mtazamo wa Kijinsia ikiwepo mabadiliko ya kisheria na kimwongozo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa UNWomen
Tanzania, akitoa salaam, alisema kwamba Changamoto
za mapengo ya usawa wa Kijinsia bado zipo, ikiwepo Ukatili wa Kijinsia,
lakini kunahitajika nguvu ya mapoja na
mshikamano wa mashirika mbalimbali ili kutokomeza kabisa vitendo vya Ukatili wa
Kiinsia.
“tusipofanya jitihada za ziada, itachukua
Zaidi ya miaka 300 kufikia usawa wa Kijinsia, tunahitaji kujipanga,
kushikamana, kuwahusisha wanawake na wanaume kwa umoja wao ili kuzuia mabaya
yote ambayo wanawake na watoto wa kike na kiume wanatendewa” alisema Odan.
Awali alitoa hotuba yake
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi alisema kwamnba, Tamasha linatoa
fursa ya wana jamii hususan wanawake kushirikishana uzoefu, kujadili,
kujifunza, kujenga ajenda ya pamoja kuhusu usawa wa jinsia na maendeleo
hususani ya namna ya kupanga mikakati ya pamoja ili kusonga mbele kwa pamoja.
“Tunaposheherekea mafanikio ya
harakati zetu kwa miaka 30 ya uwepo wa TGNP, hatuna budi kuipongeza serikali
kwa kukubali maoni na mapendekezo kadhaa mbayo tumekuwa tukipelekea na haya
ndio yamesababisha Tanzania kuonekana kwamba imetekeleza kwa kiasi kikubwa
maazimio ya Beijing…” alisema Lilian.
No comments:
Post a Comment