Thursday, October 27, 2022

Fahamu ukweli kuhusu Ukeketaji na Mathara yake

 **FAHAMU UKWELI KUHUSU UKEKETAJI*

📌👨‍👩‍👧‍👦ELIMIKA NA SMAUJATA🇹🇿


Ukeketaji ni kitendo Cha uondoaji wa Sehemu au sehemu yote ya Siri ya nje ya mwanamke au kuweka jeraha lingine Kwa viungo vya uzazi vya mwanamke Kwa Sababu ZISIZO za kitabibu.


Ukeketaji hauna faida Kwa wasichana na wanawake kwani hutokwa na damu nyingi na matatizo ya kukojoa na baadae uvimbe maambukizo,pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.

Zaidi wa wasichana Milioni 200 waliohai Leo wamefanyiwa ukeketaji ktk nchi 36 za Afrika Mashariki na Asia ambapo ukeketaji unafanyika Kwa kiwango Cha juu.Ukeketaji mara nyingi hufanywa Kwa watoto wadogo wa umri kati ya miaka ya uchanga na miaka 15, ukeketaji ni ukiukwaji wa haki za binaadam na Ukatili Wa wasichana na wanawake, ukeketaji hauna faida kwa wasichana na Jamii na unapingwa na Jamii na shirika la afya Duniani.


*AINA ZA UKEKETAJI*

1.Uondoaji wa Sehemu ya kinembe chote (sehemu ya nje na Inayoonekana ya kisimi,ambayo nisehemu nyeti ya sehemu ya Siri ya mwanamke)au mlango wa ngozi unaozunguka sehemu ya Siri ya mwanamke.

2.Uondoaji wa Sehemu ya kisimi au chote na labia ndogo(mkunjo ya ndani ya uke)pamoja na bila kuondolewa labia kubwa(sehemu ya nja ya ngozi ya uke)

3.Kupunguza Kwa mwanya wa Sehemu ya uke Kupitia utengenezaji wa muhuri wa kufunika sehemu hiyo(infibulation)muhuri huundwa Kwa kukata na kuweka upya labia ndogo au kubwa wakati mwingine Kwa kushona au bila kuondolewa kisimi/kinembe .

4.Inajumlisha Taratibu zingine zote zenye madhara Kwa sehemu za Siri ya mwanamke Kwa madhumuni yasiyo ya matibabu kama kutoboa,kuvuta,kuchanja,kukwarua na kuchoka sehemu za Siri.

Hauna faida yoyote Bali husababisha madhila,unadharirisha wasichana na wanawake Kwa njia nyingi.Unaharibu uke wa mwanamke na huingilia utendakazi wa asili wa MIILI ya wasichana na wanawake.huhusishwa na ongezeko la hatari ya matatizo ya kiafya hatari ni kubwa zaidi ya kutokana na aina Kali zaidi ya Ukeketaji.


*ATHARI ZA UKEKETAJI*

1.Maumivu makali.

2.kutokwa damu nyingi(kuvuja damu nyingi)

3.uvimbe wa tishu za viungo vya uzazi

4.homa Kali

5.Maambukizi ya magonjwa kama pepopunda,

6.Matatizo ya mkojo

7.Matatizo ya uponyaji wa jeraha

8.Kupata mshituko

9.kifo


*MATATIZO YA MUDA MREFU NI KAMA*

. Matatizo wakati wa haja ndogo(kukojoa Kwa uchungu na Maumivu makali,maabukizu ya magonjwa ya Njia ya mkojo)

.Magonjwa wa Sehemu za Siri kama usaha,kuwashwa,magonjwa yatokanayo na backteria,na maambukzi mengine)

.matatizo ya hedhi

.kuweka jeraha la maisha

. Matatizo ya Kushiriki Ngono(Maumivu wakati wa kujamiiana,kutokufurahia Tendo la kujamiiana,na kutokuridhika au kufika kileleni)

. Matatizo wakati wa kujifungua,kutokwa damu nyingi,kuhitaji upasuaji,kujifungua mtoto mfu na vifo vya watoto wachanga.

.Kuhitaji kufanya upasuaju baadae mfano kuziba au kupunguza uwazi wa uke

.Matatizo ya kisaikolojia msongo wa mawazo wasiwasi,kupata kiwewe baada ya kujifungua,kuweka kisasi,kutokujiamini


*NANI YUPO HATARINI*

.Wasichana wadogo kati ya umri wa utoto na ujana na mara kwa mara kwa wanawake watu wazima


*SABABU ZA KITAMADUNI NA KIJAMII*

WHO inasema Sababu zinazofanya ukeketaji ufanywe hutofautiana kutoka eneo Moja Hadi jingine na vile vile baada ya muda na ni pamoja na  Mchanganyiko wa mambo ya KITAMADUNI ktk jamii na Jamii

1.Pale ambapo ukeketaji ni utaratibu wa kijamii(kadia ya jamii)shinikizo la kijamii lakufuata kile ambacho wengine wanafanya na wamekua wakifanya pamoja na haja ya kukubalika kijamii na hofu ya kukataliwa na Jamii ni motisha kubwa ya Kuendeleza Mila hiyo.

2.mara nyingi huchuliwa kama sehemu muhimu Kulea wasichana na njia ya kumtayarisha kwa utu uzima na ndoa.Ukeketaji mara nyingi huchochewa na Imani kuhusu kile kinachochukuliwa kuwa tabia ya kujamiiana inayolenga Kuhakikisha ubikra kabla ya ndoa na uaminifu wa Ndoa.

3.Pale ambapo huaminika ukeketaji huongeza fursa ya ndoa Kuna uwezekano mkubwa wa kufanya vitendo hivyo.

4.Ukeketaji unahusisha na MAADILI ya kitamaduni,ya uke na adabu ambayo ni pamoja na Dhana kwamba wasichana ni safi na warembo baada ya kuondolewa Kwa sehemu ya mwili zinazochukuliwa kua najisi ZISIZO za kike au kiume

5.ktk.jamii nyingi ambazo ukeketaji unafanywa inachukuliwa kua ni Mila ya kitamaduni ambayo mara nyingi hutumiwa kama Hoja ya Kuendeleza Ukatili huo 


*HATUA MUHIMU*

Kwa kuzingatia kazi ya miongo iliyopita mwaka 1997 WHO ilitoa tamko la pamoja dhidi ya Mila ya Ukeketaji Kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la umoja wa mataifa la Idadi ya ary UNFPA tangu 1997 juhudi kubwa zimefanywa kukabiliana na ukeketaji Kupitia utafiti,kufanya kazi ndani ya jamii na mabadiliko ktk sera za umma.

Mwaka huu wa 2022 WHO itazindua mwongozo wa mafunzo juu ya mawasiliano yanayomuhusu mtu binafsi PCC mbinu ya Ushauri ambayo inawahimiza watoa huduma ya Afya kupinga mitazamo Yao inayohusiana na ukeketaji na kujenga ujuzi wao wa mawasiliano Ili kutoa Ushauri nasaha wa kuzuia ukeketaji

Kuwapatia elimu watoto juu ya madhara ya Ukeketaji ktk jamii na wanawake Ili kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuzijua haki zao za msingi na kupinga Ukatili wa namna hiyo unaoendelezwa kwenye jamii ya Kiafrika.


Imeandaliwa na Mwamini Samaje

Makamu mwenyekiti idara ya Habari na mawasiliano SMAUJATA Taifa


💪🏾SMAUJATA #👨‍👩‍👧‍👦 

*KATAA UKATILI* *WEWE* *NI* *SHUJAA* *💪💪💪🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Tuunganishe nguvu kutokomeza Ubakaji

 UBAKAJI

ELIMIKA NA SMAUJATA🇹🇿💪

   Ubakaji ni Tendo la kutumia Nguvu Katika Ngono ambapo mbakaji anatumia Nguvu kutekeleza kitendo hicho. Ama ubakaji  ni Ngono isiyo ya hiari.Kama mtu hayupo hiari na analazimishwa kufanya Hivyo hii inahesabiwa kama ubakaji hata kama anaekulazimisha ni rafiki, ndugu, jirani, mume au mtu usiyefahamiana nae.

    Ingawa Kwa kawaida ubakaji unafanyika dhidi ya wanawake lakini unatokea pia dhidi ya wanaume mbali ya watoto na watu wenye Ulemavu wa akili wasio elewa kinachoendelea.

 Ubakaji unaweza kutumiwa Nguvu ya mwili lakini pia mamlaka,vitisho na nitukio baya kabisa la kikatili Kwa nafsi ya mhanga na pengine Kwa afya yake linaloweza kumuathiri maisha yake yote kama si kusababisha kifo chake hasa likifanywa na watu kadhaa Kwa pamoja.

Matukio ya namna hiyo yanazidi kutokea hata ndani ya ukoo na mengi hayaripotiwi Kwa polisi,yakiwemo yanayotokea Magerezani kati ya watu wa jinsia Ile Ile.

Kwa vyovyote mara nyingi watu wanaobaka ni watu wanaojulikana sana na mhanga.Ubakaji hautokani na tamaa.


Matendo haya hayakubaliki iwe Serikalini,Magereza,Majumbani, kwenye jamii hata vitani,sheria za kimataifa haziruhusu matendo hayo ya kinyama na kikatili Vitani.


SABABU YA UBAKAJI

1.Ushirikina 

Mara nyingi ubakaji unafanywa na mtu anaeambiwa na Waganga wa jadi Kwa lengo la Fulani,mfano Kubaka mtoto kama Njia ya kupona ukimwi,Kubaka mtu mwenye Ulemavu Kwa lengo la kupata Mali na Utajiri nk jambo ambalo si kweli na niukatili mkubwa sana.

2.Ulevi

Ulevi kupindukia hupelekea Mwanaume au mwanamke kufanya kitendo Cha ubakaji Kwa mfano baba kumbaka mtoto wake,ama mama kumbaka mtoto wake wakiume, yote hii nikutokana na kunywa pombe kupindukia na kutokujizuia mihemko iliyotokana na ulevi.

3.Mila zisizo faa

Baadhi ya makabila  huamini kua mwanamke Hana kauli mbele za wanaume jambo ambalo kumpelekea mwanamke kulazimishwa kufanya kitendo Cha Ngono bila kuridhia kwani pale ambapo mwanaume anamuhitaji kiunyumba Naye bila ya kujiandaa nakujikuta alishaingiliwa pasi na kuridhia.

4.Maadili

Mmomonyoko wa maadili Kwa baadhi ya watoto wa kike na wakiume hupelekea mbakaji kufanya vitendo vya kibakaji ambapo,

Baadhi ya watoto wa kike kuvaa nguo zisizo kua za heshima Kisha kukatiza mbele ya wanaume hupelekea wanaume kupata mihemko na kumfanyia ubakaji binti alovaa vazi ilo lisilo na maadili.Pia wanaume kuvaa Nguo zisizo faa (mlegezo)jambo ambalo hupelekea kufanyiwa ubakaji.hata hivyo uvaaji wa nguo hizo Haina maana ya Moja kwa moja kua ndio chanzo Cha kufanyiwa ubakaji.

5:Wazazi kutosimamia malezi.

Hii huchangia kiasi Kikubwa Cha mtoto kufanyiwa ubakaji kwani wazazi siku izi wamekua wakiacha watoto muda mrefu Kwa madai yakua wanatafuta ridhki bila ya Kujua huku nyuma mtoto anafanyiwa Ukatili wa ubakaji na kupelekea mtoto kupata madhara makubwa sana.


MADHARA YA UBAKAJI

1:Kifo.

Ubakaji humfanya mhanga ajiuwe kwani huathirika kisaikolojia na Kuona Kwamba Hana Tena thamani kutokana na kitendo alicho fanyiwa

2:dharau Kwa wanawake

Mwanamke aliebakwa kudharauriwa na kushushwa uthamani wake hata baadae anapoitaji kuolewa Inapelekea kuonekana kwamba Hana thamani Kwa kubakwa kwake.

3:magonjwa ya zinaa,kama ukimwi,kaswende nk kwani mhanga hupata michubuko kutokana na kuingiliwa bila ridhaa yake Kwa Nguvu.

4:mimba zisizo Tarajiwa,


NINI KIFANYIKE KUKOMESHA UBAKAJI 

1:Elimisha kizazi

Iwe Jukumu letu kuhamasisha wanawake wanaotetea haki za wanawake wa siku zijazo.pinga mitindo iliyokaririwa ya Kijinsia na maoni ya vurugu ambayo watoto kupatana nayo kwenye vyombo vya Habari,barabarani na mashuleni, watoto wako wajue kwamba familia yako ni nafasi salaama kwao kujielezea walivyo,sisitiza uamuzi wao uwafundishe umuhimu wa ridhaa ktk umri mdogo.

2:Anzisha mazungumzo na familia yako na marafiki kuhusu jinsi mnavyoweza kufanya kazi pamoja kumaliza utamaduni wa ubakaji Katika jamii zenu.

3:Usifurahie ubakaji

Ubakaji sio jambo la kuchekesha ,utani hivyo Jitahidi kutoharirisha unyanyasaji wa kijinsia hivyo kua ngumu Kwa waathirika kusema wakati idhini Yao inakiukwa.utani unaohalalisha dhuluma ya Kijinsia Haikubaliki kashifu.

 4:Ubakaji unaoendelezwa na kutokuwepo au ukosefu wa utekelezaji wa sheria zinazoshughulikia Ukatili dhidi ya wanawake na sheria za kibaguzi ya umiliki Mali,ndoa,talaka na utunzaji wa watoto.

5.Wazazi tutenge muda wa kuwalea watoto wetu kwani Kwa kufanya Ivyo tutakua nao karibu na kuweza kuwapa elimu zaidi kwani mwalimu wakwanza Kwa mtoto nimzazi hivyo tupate muda wa kukaa na watoto wetu 

 

KWA MSAADA ZAIDI YA WAHANGA WA UKATILI

Piga simu namba 116 Bure 

Toa taarifa kwa Maafisa Ustawi,Dawati la jinsia, police,ofisi za Serikali ya mtaa,

Toa taarifa kwa Mashujaa wa maendeleo SMAUJATA

Mhanga akimbizwe hospital mara moja kwa ajili ya matibabu na Vipimo.


Imetayarishwa na

Mwamini Samaje

Idara ya Habari mawasiliano na Hamasa SMAUJATA Taifa



KATAA UKATILI WEWE NI SHUJAA💪🇹🇿

TGNP yapongeza Kikosi kazi cha Rais Samia

 TGNP yapongeza Kikosi kazi cha Rais Samia

Na Mwandishi wetu, Dar

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), imepongeza Kikosi kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mapendekezo yaliyotolewa, kwa lengo la kuboresha demokrasia ya vyama vingi nchini.

Bi. Lilian Liundi, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP


Taarifa iliyitolewa Jijini Dar es salaam, na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi imeeleza kwamba:-  “…Kikosi kazi hiki kupitia Mwenyekiti wake, Prof. Rwekaza Mukandala, kimeweza kukabidhi taarifa yake kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yenye mapendekezo 18, ikiwemo mapendekezo yenye lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake na makundi yaliyo pembezoni katika uongozi na siasa. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na

       I.            Pendekezo la. 5: Katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi walau wajumbe wawili wawe wanawake, na sifa za kuwa Mwenyekiti, Makamu au Mjumbe ziainishwe.

    II.            Pendekezo la 11: Sharti la uwepo wa Sera ya Jinsia kwenye Chama cha Siasa na ujumuishi wa makundi maalumu. Utararibu wa Viti maalumu uendelee ila sheria ziboreshwe na kuweka ukomo wa miaka 10 na pia, ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi usipungue asilimia 40.

 III.            Pendekezo na. 12: sheria zinazo kwamisha ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye siasa ziangaliwe upya

 IV.            Pendekezo na. 13: juhudi za ushirikishwaji wa vijana kwenye siasa ziongezwe

Ni matumaini yetu kuwa mapendekezo haya yatachukuliwa na kutekelezwa kwa haraka ili kuweza kufikia malengo ya kuwa na demokrasia ya vyama vingi jumuishi na itakayoleta tija katika maendeleo ya taifa letu.

Kipekee, tunatoa pongezi pia kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa kwa kuwa sehemu ya mchakato huu kwenye kikosi kazi na kuweza kubeba na kuhakikisha ajenda ya masuala ya jinsia yanajitokeza katika mapendekezo hayo.

Ikumbukwe kuwa, mnamo mwezi Februari mwaka huu, chini ya mradi wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi unaotekelezwa na TGNP kwa kushirikiana na WiLDAF, tuliweza kufanya kikao cha mashuriano na Baraza la Vyama vya Siasa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Kikosi Kazi hiki cha Kuratibu maoni ya wadau kwa lengo la kuangalia mapengo ya kijinsia ndani ya vyama vya siasa na kukubaliana namna bora ya kuziba mapengo hayo ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi ndani na nje ya vyama vya siasa.  Miongoni mwa mapendekezo yaliyotoka katika kikao chicho cha mashauriano ni pamoja na uwepo wa Sera ya Jinsia katika vyama vya siasa.


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, akipokea taarifa ya mapendekezo ya kikosi kazi kutoka kwa Mwenyekiti wake, Prof. Rwekaza Mkandala, Ikulu Jijini Dar es salaam

TGNP tunaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Baraza la Vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili katika kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo hayo yaliyotolewa na kikosi kazi na kuhakikisha kuwa kwa pamoja tunaweka misingi imara ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi wa siasa na ngazi za maamuzi.   Tunatambua mchango wa Kikosi Kazi, Baraza la vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika kuleta mabadiliko na usawa wa kijinsia nchini.

 

Mhe. Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa na wajumbe wa Kikosi kazi Ikulu Dar es saalam

Tuesday, October 18, 2022

Mambo ya kuzingatia kabla na wakati wa kuandika wosia

 Mambo ya kuzingatia kabla na wakati wa kuandika wosia

Hapo awali nilikuwa nikiamini kuacha wosia ni uchuro yaani kujitakia au kujitabiria kifo chako mwenyewe. Hii ilipelekea nikaogopa mnoo inapotokea nikisikia habari zinazohusu masuala ya wosia. Hali kadhalika ninaamini pia wapo watu wengi wanaoogopa kuacha wosia kwa dhana hii hii kwamba ni uchuro wa kujitabiria kifo.

Wengine nao huamini ya kwamba wosia unaachwa na watu wasomi au wazee au wanaume au wanaokaribia kufa au wenye uwezo mkubwa kwenye kumiliki mali kama vile nyumba, viwanja, hisa kwenye makampuni au pesa katika akaunti za Benki na kadhalika.

Yote hayo yatajibiwa na makala hii hatua kwa hatua ambapo nitaangazia kwa ufasaha ni nini maana ya wosia kwa jicho la kisheria zaidi, aina zake, sifa, pamoja pia na faida. Tutaweza pia kuangalia japo kwa uchache wosia unatakiwa uweje.

Nini basi maana ya wosia?

Wosia ni tamko lenye nguvu kisheria ambapo mtoa wosia anakusudia ni namna gani mali yake au zake zitasimamiwa baada ya kifo chake. Katika wosia mtoa wosia anaweza kuelezea ni kwa namna gani mali yake au zake zitagawanywa kwa warithi wake, kiwango ambacho watagawiwa, orodha ya mali anazomiliki, orodha ya wadai na wadaiwa, namna gani atazikwa na kadhalika.

 Hiyo ni baadhi tu ya orodha ya mambo yanayotakiwa yawepo katika wosia na ni vyema kila jambo ambalo ni muhimu kuandikwa katika wosia ili kuondoa utata. Ikumbukwe kuwa mwacha wosia hatakuwa hai ili aweze kuulizwa kuhusiana na wosia wake wakati utakapoanza kutumika hivyo basi ni vyema uandikwe kwa lugha iliyo wazi na yenye kueleweka vizuri. Utata wowote utakaojitokeza unaweza kupelekea wosia kubatilishwa na wosia huo utakuwa batili automatiki.

Ikumbukwe ya kuwa kutokuacha wosia au kuacha wosia wenye dosari itapelekea mali utakazoacha kugawanywa kwa utaratibu wa wasioacha wosia. Utaratibu huu unaweza ukawa sio rafiki sana kwani wakati mwingine unaweza kwenda kinyume kabisa na matakwa ya mtoa wosia.

Aina za wosia

Wosia wa mdomo

Huu ni wosia unaotolewa kwa maneno ya mdomo yaani ‘Oral will’. Japokuwa aina hii ya wosia ni ngumu wakati mwingine kuthibitishwa  lakini sharia inautambua kuwa ni wosia kama vile ulivyo ule wa maandishi. Kwa mfano, Local Customary Law (Declaration) (No. 4) Order, 1963 inataka wosia huu ni lazima utolewe wakiwepo mashahidi wanne (4) yaani wawili wawe ni ndugu na wawili wasiokuwa ndugu. Mke au wake za marehemu, kama anaye au anao, ni lazima awe nyongeza  ya mashahidi hao. Kigezo hiki kisipofuatwa basi wosia huo utabatilishwa kweupee.

Wosia wa maandishi

Huu ni wosia unaotolewa kwa njia ya maandishi. Wakati mwingine unajulikana kama wosia rasmi. Lengo lake ni sawa tu kama lilivyo la wosia wa mdomo kama nilivyoeleza hapo juu. Umakini wa hali ya juu sana unatakiwa uzingatiwe katika kuandika wosia huu.

Ni lazima ‘legal formality’ yaani matakwa ya kisheria yafuatwe wosia wa aina hii unaopoandikwa. Baadhi ya matakwa hayo ni kama vile ni lazima uwe kwa maandishi na kusainiwa na mtoa wosia huo mbele ya mashahidi, ushuhudiwe angalau na mashahidi wawili na ni vizuri mmoja kati yao akawa ni nduguye mtoa wosia; mashahidi hao wanaweza kuzidi wawili ila tu wasipungue.

Wosia wa maandishi unaweza ukabatilisha wosia uliotolewa awali kwa mdomo, isipokuwa wosia wa mdomo hauwezi kubatilisha ule wa maandishi.  Na anayeweza kufanya hivyo ni mtoa wosia peke yake na si mtu mwingine.

Wosia uliotolewa na watu wawili kwa lengo la pamoja

Huu unaitwa kwa lugha ya kitaalamu ‘a mutual will’. Wosia huu unatolewa na watu wawili wenye malengo ya pamoja kama nilivyodokeza hapo juu kwa maana ya kwamba wote wanakubaliana jambo au mambo yanayofanana.

Wosia huu unapendelewa sana na walio katika mahusiano ya kimapenzi kama vile wanandoa. Kwa mfano kwenye wosia huu wanaweza wakakubaliana katika wosia huo ya kwamba yeyote atakayetangulia kufariki kati yao basi mali zitaenda kwa yule aliyebakia hai, kama vile mume akitangulia kufariki basi mali walizonazo zitamilikiwa na mke na kinyume chake, halafu wanaweza pia kukubalia namna gani watoto wao watapata urithi baada ya wote kufariki.

Hii ijulikane ya kwamba makubaliano haya kama yalikwisha kuwekwa hakuna namna yanaweza kubadilishwa kama mmoja wapo wa watoa wosia huo kashafariki.

Wosia wa masharti fulani

Unaweza ukauitwa ‘Conditional will’ ambapo masharti fulani aliyoyaweka mtoa wosia na ni lazima yatimizwe kwanza ndipo tunaweza kusema wosia una nguvu kisheria. Msharti haya yanatakiwa yawe ni yale yanayotekelezeka.

Kwa mfano mtoa wosia anaweza kusema nyumba hii apewe Comfort pindi atakapooa au atakapoweza kupata Shahada yake ya kwanza ya Sheria, hivyo basi ikiwa mtoa wosia huo amefariki  nyumba hiyo haitokwenda kwa Comfort mpaka atakapokuwa ameoa au kupata Shahada yake ya kwanza ya Sheria.

Mambo ya msingi yanayotakiwa kuzingatiwa wakati wa kuandaa wosia

Wosia ni lazima uwe na mambo yafuatayo vinginevyo inaweza kupelekea ukabatilishwa na mpango wa kugawanya mali bila wosia ukachukua nafasi. Mambo hayo ni kama vile:

1. Mtoa wosia ni lazima kisheria awe na uwezo wa kuacha wosia. Hapa nina maana ya kwamba sharia inahitaji mtu anayetoa wosia awe na umri wa miaka isiyopungua kumi na minane (18). Pia anatakiwa awe na akili timamu wakati wa kuacha wosia huo. Hali kadhalika mtu mwenye matatizo ya akili anaweza kuandika wosia pindi tatizo hilo limemwondoka kwa mfano endapo atakuwa anasumbuliwa na tatizo la ukichaa wa muda ‘temporary insanity’. Mtu akiwa na akili timamu na akaandika wosia lakini baadae akapata ukichaa wosia ule hautokuwa batili kwani wakati anauandika alikuwa na utimamu wa akili.

2. Mtoa wosia ni lazima afahamu yale yaliyoandikwa katika wosia. Kwa mfano mwacha wosia kaandikiwa wosia eidha na wakili au mtu yeyote ni lazima afahamu yale yaliyoandikwa ndani kabla hajaweka saini.

3. Wosia ni lazima utaje majina ya mtoa wosia.

4. Wosia unatakiwa utaje atakaye simamia mirathi.

5. Wosia ni lazima uwe na tarehe ya siku wosia huo ulipoandaliwa.

6. Wosia ni lazima utaje aina na kiwango cha thamani ya mali zinazotolewa katika wosia. Kama kuna kitu kinamilikiwa na watu wawili au zaidi basi ni sharti hilo libainishwe katika wosia.

7. Wosia unatakiwa utaje idadi ya warithi na wanufaika wa mirathi hiyo.

8. Wosia unatakiwa utilie maanani vipi itakapotokea mrithi au warithi na mnufaika au wanufaika watakapofariki kabla ya mtoa wosia.

9. Wosia unatakiwa utilie maanani ndoa inayoweza kufungwa baada ya wosia kuandaliwa. Ndoa itakayofungwa baada ya wosia kuandikwa inaweza kuathiri wosia huo.

10.         Wosia ni lazima usainiwe na mtoa wosia mbele ya mashahidi.

11.         Wosia ni lazima uthibitishwe na mashahidi.

12.         Mtoa wosia ni lazima aonyeshe ya kuwa ameandika wosia huo akiwa na akili timama pia bila kushurutishwa.

13.         Lazima katika wosia kuwe na kipengele kinachoonyesha ya kuwa mtoa wosia akibatilisha wosia wowote alioutoa awali.

14.         Endapo mtu ambaye kwa kawaida alitakiwa kupewa sehemu ya mirathi lakini hakutajwa katika wosia basi ni vyema sababu zikatolewa.

15.         Endapo mambo haya yatazingatiwa itapunguza kwa kiasi kikubwa matatizo yanayoweza kutokea baadae mtoa wosia atakapokuwa amekwisha fariki, mfano, wosia huo kukataliwa au kubatilishwa kwa kutokufuata taratibu kama nilivyokwisha kuelezea kwa uchache hapo awali.

Muhimu: Ifahamike ya kwamba hakuna fomula maalumu ya kuandika wosia lakini endapo utazingatia mambo niliyoyataja hapo juu basi wosia wako utakuwa una nguvu kama wosia mwingine wowote.

Faida za kuacha wosia

·         Humsaidia mtoa wosia kupanga ni namna gani mali yake itakavyosimamiwa baada yakufariki kwake. Endapo atafanya hivyo basi itamzuia mtu asiyehusika kuingilia mali zake pindi atakapofariki.

·         Kuepuka mali alizoacha kugawanywa kwa utaratibu wa asiyeacha wosia. Upoutaratibu ambapo mtu asiyeacha wosia mali zake kugawanywa kinyume cha matakwa yake kama nilivyoeleza hapo awali hivyo basi ili kuepusha jambo kama hili kutokea ni vyema kabisa ukajiwekea utaratibu wako ambao utaheshimiwa na kila mtu.

·         Kuepusha watu wadanganyifu wenye nia ya kutaka kunufaika na mali alizokuwa amechuma marehemu.

·         Wosia utamwezesha mtoa wosia kumweka mtu mwaminifu atakayesimamia mali zake baada ya yeye kufariki. Pia utamsaidia kuandaa walezi wa mtoto au watoto wake. Jaribu kufikiri mazingira ambayo baba mwenye mtoto au watoto kafariki na pengine mkewe nae kafariki au hawaishi wote na pengine mtoa wosia huyo ndugu zake wa kuzaliwa walimtangulia auhana kabisa, katika mazingira haya marehemu asipoandaa utaratibu mzuri wa kusimamia mirathi basi mali na watoto alioacha watakuwa katika mazingira magumu sana. Wosia tu ndio utakaookoa hilo lisitokee.

·         Wosia utasaidia kufahamu mali za marehemu na nani apewe nini na kipi.

·         Wosia pia utaweza kueleza utaratibu wa namna mtoa wosia atakavyozikwa. Hapa ataweza kuelezea azikweje, wapi na kwa gharama zipi kutoka wapi. Unaweza hata kuamua uchomwe moto badala ya kufukiwa na waliobakia watahakikisha hilo linatokea.

Je ni wakati gani sahihi kwa mtu kuandika wosia?

Lengo kuu la wosia ni kutaka mambo fulani fulani yafanyike pindi mtu atakapokuwa umefariki. Tusikariri ya kuwa ni lazima tuwe na vitu vingi ndio tuweze kuacha wosia kwani unaweza hata kuacha wosia kuutoa mwili wako pindi utakapofariki utumike katika kufanyia majaribio kwa wanafunzi wa udaktari katika chuo cha udaktari cha Muhimbili.

Ukizingatia vigezo vingine kama vile umri na kadhalika, mtu yeyote anaweza kuacha wosia. Hata kama unayo mali yenye thamani ndogo bado ni muhimu kwa wewe kuacha wosia kama nilivyoweza kuelezea hapo juu.

Unaweza ukaacha wosia kwenye mambo mengine ukiacha mali na vitu kama nilivyokwisha kudokeza hapo juu. Hivyo basi wosia unaweza kuachwa wakati wowote mtu anapokuwa hai na sio kusubiria mtu yupo mahututi ndio anatoa wosia.

Ni nani anapaswa kuandika wosia?

Mtu yeyote, awe mwanaume au mwanamke, kijana au mzee, mwenye mali nyingi au chache, mwenye umri wa miaka kumi na minane (18) na kuendelea akiwa na akili timamu wakati wa kuacha wosia basi anakidhi vigezo vya kuacha wosia.

Muhimu

Ni muhimu pia kufahamu ya kuwa wosia unakusudiwa kuwa na nguvu pale mtoa wosia huo atakapofariki. Watu wafahamu wosia ni tamko au karatasi tu kama aliyeandika wosia huo bado yupo hai. Itambulike pia mali zitakazopatikana baada ya wosia kuachwa zinaweza kuwa sehemu ya wosia bila hata kuorodheshwa katika wosia huo.

Lakini pia wosia wa mwanzo unaweza kufutwa au kubadilishwa na wosia mwingine. Hii inaweza kutokea hata kama kuna kipengele katika wosia kinachosema wosia huo hautabadilishwa kamwe. Jambo hili linaweza kufanywa na aliyetoa wosia kipindi cha uhai wake na sio mtu mwingine yeyote.

Mwisho naendelea kukusisitiza ndugu msomaji wangu usikose mwendelezo wa Makala hizi. Endelea kuutembelea ukurasa huu ili kujipatia makala mbali mbali kuhusiana na sheria. Kumbuka ‘learning is a process’ kwa maana ya kwamba kujifunza ni mchakato hivyo usichoke kujifunza. MAKALA HII NI KWA MUJIBU WA: https://ijuesheriatz.wordpress.com/2017/09/04/mambo-ya-kuzingatia-kabla-na-wakati-wa-kuandika-wosia/

ANDIKA WOSIA KUILINDA FAMILIA DHIDI YA MIGOGORO YA MIRATHI

ANDIKA WOSIA KUILINDA FAMILIA DHIDI YA  MIGOGORO YA MIRATHI

Kwa mujibu wa wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ni muhimu kuandika wasio ili kuepusha jamii kuingia kwenye migogoro ya mirathi mara mtu anapofariki.

Suala la mirathi, linahitaji, uelewa wa jamii nzima kwa mapana yake. Jamii ielewe kwamba mirathi sio uchiro, mirathi ni kitu muhimu kw amustakabali wa familia zetu.

TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA
Taratibu za kuandika wosia zinatofautiana kulingana na sheria ya mirathi inayotumika.

1. WOSIA WA MAANDISHI

  • Wosia huu unashuhudiwa na watu wawili pale ambapo mtoa wosia anajua kusoma au kuandika. Shuhuda mmoja lazima awe ndugu wa karibu wa mtoa wosia  na mwingine ambaye sio ndugu wa karibu.Wosia na unatakiwa uwe na tarehe, uandikwe kwa karamu ya wino au upigwe chapa na uwe na saini ya mtoa wosia na saini za mashuhuda ambapo wote wanatakiwa kutia saini zao kwa wakati mmoja.
  • Mtoa wosia asiye jua kusoma ua kuandika awe na mashuhuda wa nne wanao jua kusoma na kuandika,muhusia huyo aweke alama ya kidole gumba cha mkono wake wa  kulia,mashuhuda  hao wote washuhudie na waweke saini zao kwenye Wosia kwa wakati mmoja.

2. WOSIA WA MDOMO/MATAMSHI

  • Wosia huu unashuhudiwa na mashuhuda  wasiopungua wa nne wawili  kati yao ndugu wa mtoa wosia na wawili waliobaki wasio ndugu wa mtoa wosia.Wosia huu utolewa na mtu asiye jua kusoma na kuandika.

TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA KATIKA SHERIA ZA MIRATHI

  • Wosia katika Sheria za kimila,zipo katika jedwali la 3 la Sheria ya (The Local Customary Law (Declaration|) No. 4 Order,1963.
  • Wosia katika Sheria za kiserikali,zipo katika sheria iliyorithiwa kutoka kwa Waingereza ya(The Indian Succession Act ),iliyopitishwa huko India mwaka 1865.
  • Hauna tofauti kubwa na wosia wa kimila isipokuwa wosia huu unatakiwa uwe katika maandishi.Vipengele vyote vya wosia wa maandishi vinatumika.
  • Mtoa wosia anaweza kufuta au kuongeza maneno mengine kwa kuandika maandishi mengine ambayo yatatakiwa kuzingatia masharti ya uandikaji wosia.
  • Wosia katika Sheria za kiislamu, mtoa wosia anaruhusiwa kuuusia 1/3 ya mali yake 2/3 lazima irithiwe na warithi halali.

UMUHIMU WA KUANDIKA WOSIA

  • Unaweka mambo bayana kuondoa utata kwa familia na jamaa zako.
  • Unamchagua msimamizi wa mirathi unayemtaka wewe.
  • Unatoa maelezo ya wapi mwili wako uhifadhiwe, taratibu zitakazotumika kuuzika mwili wako na jinsi gani mali yako igawanywe kama upendavyo wewe na kwa mujibu wa Sheria.

MASHARTI YA WOSIA

  • Mtoa wosia lazima awe na akili timamu.
  • Awe ametimiza miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
  • Uonyeshe tarehe,mwezi na mwaka ulioandikwa.
  • Uonyeshe majina ya warithi.
  • Mtoa wosia ahusishe mali zake binafsi na si za mtu mwingine.
  • Wosia ni siri wanufaika hawatakiwi kuujua.
  • Ushuhudiwe na mashaidi wawili,  kwa  mtoa wosia anaye jua kusoma na kuandika na kwa yule asiye jua kusoma ua kuandika mashuhuda wake lazima wawe wanne na wajue kusoma na kuandika.
  • Mtoa wosia lazima aweke saini yake,na kama hajui kusoma na kuandiaka aweke alama ya dole gumba la mkono wa kulia.

 

Monday, October 17, 2022

Mambo muhimu kwa vyombo vya habari kukabiliana na Ukatili

 

Mambo muhimu kwa vyombo vya habari kukabiliana na Ukatili

Na Mwandishi Wetu.

SERA ya Jinsia ya vyomvo vya habari ya mwaka 2019, inavitaka vyombo vyote vya habari kuzingatia yafuatayo ili kuepuka kuwa sababu au chanzo cha ukatili wa kijinsia.  Vyombo vya habari vitaepuka kuunga mkono chuki au kushadidia ukatili wa kijinsia. Vitapaswa kuepuka mambo yafuatayo:

 Kutangaza au kuchapisha kwa kinagaubaga habari za ubakaji au ukatili wa kingono kwa namna ambayo itafanya waathirika watambulike;

Kushadidia picha chafu na za ukatili dhidi ya wanawake na watoto;

Kuwadunisha wanawake kwa kuwabainisha kama viumbe dhalili wanaostahili kufanyiwa ukatili, labda tu pale ambapo ukatili ni sehemu ya habari inayosimuliwa;

Kuwadunisha ama kuwatumia vibaya wanawake kwa kuwaonyesha kama viumbe dhalili wasio na uwezo wa kufanya lolote mbele ya ukatili na unyanyasaji;

Kuwadunisha au kuwatumia vibaya wanawake na kuhujumu nafasi chanya waliyo nayo, na umuhimu wao katika jamii;

Kushadidia unyanyasaji wa mawazo[1]mgando juu ya jinsia, na

Kuchapisha habari ambazo zinaweza kuibua vurugu na chuki kutokana na uwasilishaji mbaya wa masuala ya jinsia au kutukuza ukatili dhidi ya wanawake

Wakuu wa nchi wanawake ni 13 pekee duniani

 

Wakuu wa nchi wanawake ni 13 pekee duniani

Na Deogratius Temba

Kwa mujibu wa Tovuti ya UNWOMEN.

Kati ya nchi 193 ambazo ni Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa, ni wanawake 28 pekee wanaohudumu kama Wakuu wa Nchi au Serikali waliochaguliwa. Bado kuna safari ndefu linapokuja suala la uwiano wa wanawake katika ngazi nyingine za uongozi wa kisiasa.

Hadi sasa, wanawake ni asilimia 21 ya mawaziri duniani, asilimia 26 ya wabunge wa Mabunge ya kitaifa, na asilimia 34 ya viti vya serikali za mitaa waliochaguliwa.


Ushiriki sawa wa wanawake na uongozi katika maisha ya kisiasa na ya umma ni muhimu ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030. Hata hivyo, data zinaonyesha kuwa wanawake hawana uwakilishi mdogo katika ngazi zote za kufanya maamuzi duniani kote, na kwamba kufikia usawa wa kijinsia katika maisha ya kisiasa ni mbali.

Wanawake katika nafasi za serikali

Kufikia tarehe 19 Septemba 2022, kuna nchi 28 ambapo wanawake 30 wanahudumu kama Wakuu wa Nchi na/au Serikali. Kwa kiwango cha sasa, usawa wa kijinsia katika nyadhifa za juu zaidi za mamlaka hautafikiwa kwa miaka 130 nyingine.

Nchi 13 pekee zina Mkuu wa Nchi mwanamke, na nchi 15 zina Mkuu wa Serikali mwanamke.

Asilimia 21 pekee ya mawaziri wa serikali walikuwa wanawake, huku nchi 14 pekee zikiwa zimefikia asilimia 50 au zaidi ya wanawake katika makabati. Kwa ongezeko la kila mwaka la asilimia 0.52 pekee, usawa wa kijinsia katika nyadhifa za mawaziri hautapatikana kabla ya 2077.

Nyadhifa tano zinazoshikiliwa zaidi na mawaziri wanawake ni: Familia/watoto/vijana/wazee/walemavu; ikifuatiwa na mambo ya Kijamii; Mazingira/maliasili/nishati; Mafunzo ya ajira/kazi/ufundi, na masuala ya Wanawake/usawa wa kijinsia.

Wanawake katika mabunge ya kitaifa

Ni asilimia 26 pekee ya wabunge wote wa kitaifa ni wanawake, kutoka asilimia 11 mwaka 1995.

Ni nchi tano pekee ndizo zenye asilimia 50 au zaidi ya wanawake bungeni katika nyumba za pekee au za chini: Rwanda (asilimia 61), Cuba (asilimia 53), Nicaragua (asilimia 51), Mexico (asilimia 50) na Umoja wa Kiarabu. Emirates (asilimia 50).  Nchi nyingine 27 zimefikia au kuzidi asilimia 40, zikiwemo nchi 15 za Ulaya, tano Amerika Kusini na Karibea, tano barani Afrika, moja Asia na moja katika Pasifiki. Zaidi ya theluthi mbili ya nchi hizi zimetumia upendeleo wa kijinsia—ama upendeleo wa wagombea waliopitishwa kisheria au viti vilivyotengwa—nafasi ya kufungua kwa ushiriki wa kisiasa wa wanawake katika mabunge ya kitaifa.

Ulimwenguni, kuna Majimbo 24 ambapo wanawake wanachangia chini ya asilimia 10 ya wabunge katika nyumba moja au chini, ikiwa ni pamoja na vyumba vitatu vya single/chini visivyo na wanawake kabisa. Kwa kiwango cha sasa cha maendeleo, usawa wa kijinsia katika vyombo vya sheria vya kitaifa hautafikiwa kabla ya 2063. Katika Amerika ya Kusini na Karibiani, na Ulaya na Amerika Kaskazini, wanawake wanashikilia zaidi ya asilimia 30 ya viti vya ubunge. Wanawake ni asilimia 26 ya wabunge katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Katika Asia ya Mashariki na Kusini-mashariki mwa Asia, kuna asilimia 22 ya wabunge wanawake ikifuatiwa na Afrika Kaskazini na Asia Magharibi yenye asilimia 21 ya wanawake katika mabunge ya kitaifa. Kuna chini ya asilimia 20 ya Wabunge wanawake katika Asia ya Kati na Kusini mwa Asia na Oceania.

Wanawake katika serikali za mitaa

• Takwimu kutoka nchi 136 zinaonyesha kuwa wanawake wanajumuisha karibu milioni 3 (asilimia 34) ya wajumbe waliochaguliwa katika vyombo vya mashauri vya mitaa. Ni nchi mbili pekee zimefikia asilimia 50, na nchi nyingine 20 zina zaidi ya asilimia 40 ya wanawake katika serikali za mitaa.

• Tofauti za kimaeneo pia zimebainishwa kwa uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya mashauri vya ndani, kufikia Januari 2022: Asia ya Kati na Kusini, asilimia 41; Ulaya na Amerika Kaskazini, asilimia 36; Oceania, asilimia 32; Asia ya Mashariki na Kusini-Mashariki, asilimia 28; Amerika ya Kusini na Karibiani, asilimia 25; Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, asilimia 25; Asia ya Magharibi na Afrika Kaskazini, asilimia 18.

Saturday, October 8, 2022

Sheria zitumike kuzuia mila na desturi kandamizi- DC Mpogolo

kuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akifunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini.
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akizungumza wakati akifunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo amefunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro huku akihimiza kila mmoja kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kusisitiza Mila na desturi ziendelee kuwepo lakini sheria itawale.


Mpogolo amesema Dhamira ya serikali ni kuhakikisha mila na desturi kandamizi zinafutwa hivyo ni wajibu wa kila mwanachi anakuwa mstari wa mbele kutokomeza ukatili wa kijinsia.

“Mila na desturi ziwepo lakini sheria itawale, ukiacha mila na desturi zitawale lazima kuna kundi la watu litakandamizwa. Kuna watu wanatumia mila na desturi kuharibu sheria hivyo kuathiri sheria kuchukua mkondo wake. Hongereni sana TGNP Warsha hizi, matamasha haya yanasaidia sana huku pembezoni”,amesema Mpogolo.


“Nawaahidi serikali itakwenda kusimamia yale yote tuliyokubaliana kwenye tamasha la jinsia ikiwemo kutokomeza mila kandamizi. Changamoto kubwa ni mila na sheria zetu, hakuna mtu yeyote atakayeweza bila sisi wenyewe kuamua kuziweka pembeni mila kandamizi zinamkandamiza mwanamke”,ameongeza.
Mkuu wa wilaya ya Same Mhe. Edward Mpogolo akisalimiana na washiriki wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini.

Aidha amewahamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya serikali za mitaa na kuingia kwenye vyombo vya maamuzi.

“Kina mama mna nguvu, sasa hivi hakuna mama wa nyumbani Mama zangu , dada zangu tunaishi kule mtaani tuna nafasi ya kugombea kwenye serikali za mitaaa, kule ndiko kaya zinakopatikana na ndiko kuna vyanzo vya ukandamizaji. Huko ndiko wajane waliko, huku kwenye ofisi zetu wanaokuja ofisini ni wajane wanalalamika ardhi zao kudhulumiwa. Haki ya umiliki wa ardhi imekuwa changamoto kwa wajane, watoto wa kike hawapewi haki lazima haya tuyaondoe”,amesema Mpogolo.

“Nilichokiona ni namna gani TGNP ina ushirikiano na wadau mbalimbali, mmealika wageni kutoka ngazi ya kitongoji hadi mkoa. Tunawahakikishia wanawake kuwa nafasi za kuingia vyombo vya maamuzi lakini msikengeuke, kuna baadhi wakiingia huko wanakengeuka, msimamie vizuri ili kulinda haki za wanawake, msitumie msumeno kukata vibaya mnapoingia kwenye vyombo vya maamuzi",amesema.
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo.

Mpogolo ameipongeza TGNP na wadau wake kwa kulifanikisha Tamasha hili la kanda ya Kaskazini ambapo washiriki wamepata fursa ya kujadili kwa kina, na kubadilishana uzoefu kupitia mada mbalimbali zilizofanyika katika jopo na warsha mbalimbali ambazo zilijikita katika kuangalia masuala ya fursa za kilimo, uimarishaji wa huduma za kijamii, uongozi shirikishi na mila kandamizi. Mada zote hizi ziliongozwa na mada kuu ya Tamasha hili Jinsia isemayo, “Haki za Kiuchumi:Rasilimali ziwanufaishe wananchi waliopo pembezoni kwa Maisha endelevu”.


“Nimearifiwa pia mijadala hiyo ilitoa mapendekezo na maazimio mbalimbali yenye mrengo wa kusaidia Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Same katika kutekeleza na kusimamia masuala nyeti ili kufikia Haki za Kiuchumi hususan kwa makundi yaliyo pembezoni, pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazokwamisha ufikiwaji wa fursa kwa makundi hayo”,amesema Mpogolo.

“Nimefarijika zaidi baada ya kuarifiwa ya kwamba washiriki wote waliofika hapa, zaidi ya 500 wameweka azma ya kwamba kila mmoja kuwafikia angalau wanajamii watano (5) na kuwahamasisha kujiunga kwenye harakati za kuwainua wanawake na makundi ya pembezoni katika kutambua, kufikia na kutumia fursa za kiuchumi ili kuleta maendeleo katika ngazi ya kaya, Kijiji, Halmashauri na hatimaye kitaifa. Huu ndio unapaswa kuwa msingi wa kujenga uchumi wetu na kudumisha mshikamano baina ya makundi mbalimbali kwenye jamii. Huu ndio Uzalendo na ndio njia sahihi inayostahiki kuunga mkono jitihada za Serrikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kufika usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu”,amesema Mpogolo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi ameyataja baadhi ya maazimio yaliyofikiwa kwenye Tamasha hilo ni pamoja na Wajumbe wa Kamati za Vijiji kuweka hamasa na kutumia fursa mbalimbali za kujiongezea uwezo na uelewa kuhusu elimu ya afya ya uzazi ili kuwa mstari wa mbale katika kusimamia kwa ufanisi wa utoaji huduma hizo.

“Maazimio mengine ni Serikali za Vijiji kwa kupitia Utaratibu uliowekwa na TAMISEMI wa Fursa na Vikwazo vya Maendeleo (yaani O&0D) kutambua na kuweka kuwa kipaumbele upatikanaji wa vifaa tiba na idadi ya kutosha ya watoa huduma kwenye zahanati na vituo vya afya na Kuchagiza mapitio na marekebisho ya sheria (Uchaguzi Serikali za Mitaa) na Kanuni ili kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake na makundi mengine kujumuishwa na kushiriki kikamilifu kugombea nafasi za uongozi na vyombo va maamuzi katika ngazi mbalimbali”,amesema Liundi.


“Pia Kuboresha mfumo na utaratibu wa utoaji wa mikopo ya Halmashauri na mafunzo ya uendeshaji miradi/biashara na utunzaji wa fedha kwa wanawake, vijana na makundi mengine ili kupunguza urasimu na kuwezesha upatikanaji rahisi wa taarifa kuhusu fursa kwa makundi hayo na Kuhamasisha vikundi vya kijamii (wanawake, wanaume, vijana, wazee, watu wenye ulemavu) na Viongozi wa mila na dini ili kuwa mstari wa mbele kutoa elimu na kuongeza uelewa kwenye jamii kuhusu haki za wajane kurithi na kukemea ukatili na dhuluma za ndoa za utotoni na ukeketaji”,ameongeza.


Maazimio mengine ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya, hususani, maafisa biashara kwa kushirikiana na sekta binafsi na taasisi zisizo za kiserikali kuwapatia taarifa (kupitia teknolojia ya simu) na kuwajengea uwezo wanawake na makundi mengine ya pembezoni wanaoshiriki katika kilimo kutambua na kufikia masoko na kunufaika na bei nzuri kwa mazao yao.

Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali amesema sheria ndiyo msumari wa kumaliza matukio ya ukatili huku akihamasisha wanawake wasiachwe nyuma kwenye masuala ya maendeleo.

Mwakilishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Bi. Bahati Majwala amewahamasisha kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa kwenye halmashauri, kwenye wizara, benki ya biashara Tanzania akibainisha kuwa Serikali inaendelea kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali kuhusu elimu ya vifungashio na namna ya kuandaa bidhaa na kuhamasisha wanawake kujiunga kwenye vikundi.


Naye Mratibu wa Jinsia OR-TAMISEMI, Linus Kahendaguze amesema Mikopo inayotolewa na halmashauri imeboreshwa sasa inafanyika kidigitali na imeendelea kuwanufaisha wananchi na serikali imeendelea kutoa fedha nyingi mfano Mwaka 2021 ilitoa shilingi Bilioni 62 ambapo asilimia kubwa ya wanufaika ni wanawake.

“Rais Samia ni kinara wa masuala ya kijinsia ndiyo maana ameendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake ikiwemo fursa za mikopo,kilimo. Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kila anazuia ukatili wa kijinsia. Tunatakiwa kuishi katika mazingira ya amani, tutoea taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia”,amesema.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akizungumza wakati akifunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akizungumza wakati akifunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akizungumza wakati akifunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi  akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi  akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi  akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
Rose Ngunangwa akiwasilisha taarifa ya mambo yaliyojiri kwa niaba ya TGNP wakati wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
Mratibu wa Jinsia OR-TAMISEMI, Linus Kahendaguze akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) 

Mwakilishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Bi. Bahati Majwala akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) 
Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Watoto na Vijana KKKT Dayosisi ya Pare na Compassion Tanzania akizungumza kwa niaba ya washiriki wa Tamasha wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Annastazia Tutuba akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) 
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea

Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea

Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akiagana na washiriki wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akiagana na washiriki wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akiagana na washiriki wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) baada ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same