Tuesday, February 20, 2024

TGNP and LGTI -Hombolo conduct training on Gender to LGA Officials at Ward Level


Participants group photo 

By Deogratius Temba,Dar

Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) in collaboration with the Local Government Training Institute (LGTI) Hombolo, supported by UNWOMEN Tanzania through the Women Leadership and Economic Rights Project (WLER), have officially kicked off a four days training to Local Government officials at ward level on Gender Mainstreaming and Gender Responsive Budgeting. 

The training is being carried out in Dar es Salaam involving officials at the ward level from Lindi, Mtwara and Dar es Salaam regions.

The Women Leadership and Economic Rights Project (WLER) is currently being implemented in various regions to promote women’s participation in leadership and the right to benefit from economic opportunities.


Ms. Lilian Liundi, The Executive Director, Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) during the Opening session in Dar es salaam


Dr. Lazaro Kisumbe, Deputy Rector LGTI- Hombolo during the opening session


Speaking during the official opening, Lilian Liundi, TGNP’s Executive Director said that, this training is a great opportunity for capacity strengthening of council officials that will help them understand how to effectively engage community members in the government planning processes at ward and village levels.

“This training resulted from the realization that; LGA officials need to understand gender issues and have them prioritized at community level during planning. This together alongside collaboration with the community members themselves will help in managing the O&OD process which will consequently be beneficial to the communities they serve said Liundi

She also added that, due to their importance and the positions they have at the community level, the participants of the training have the ability to provide education in the community through township and village meetings to make women participate but also to come forward to run for leadership to increase the number of women in positions leadership and decisions at the village and local level.

On the other hand, the Deputy Rector- Adminisitration and Finance of the Local Government Training Institute (LGTI) Dr. Lazaro Kisumbe who was also the guest of honor in the official opening of the training said that, the Institute had carried out research which identified several existing gender gaps in the Local Government Authorities which hinder government efforts in planning and budgeting with a Gender perspective.

“The WLER project intends to close the existing gender gaps which is the reason why with the support from UNWOMEN Tanzania, we are collaborating with TGNP to capacitate ward level local government officials who will then go back to their duty stations to share and enlighten their respective Ward.

Development Committees on how to mainstream gender during planning processes while incorporating community priorities,” he said.

He also added that, through this training, officials will be able to identify ways that gender can be

mainstreamed at the ward level and also ensure that the concept of gender and issues related are well understood at all levels.














TGNP na Chuo cha serikali za Mitaa Hombolo waendesha mafunzo ya Jinsia


Na Deogratius Temba

Picha ya Pamoja ya washiriki mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa 'wawezeshaji ngazi ya Kata' maafisa kutoka Halmashauri mbalimbali 


Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) wameendesha mafunzo ya urasimishaji wa masuala ya Kijinsia kwa watumishi wa Halmashauri 10 katika ngazi ya Kata.

Mafunzo hayo ni sehemu a mradi unaofadhiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UNwomen) unaojulikana kama Sauti ya Wanawake, Uongozi na Haki za kiuchumi unaotekelezwa katika mikoa na Halmashauri mbalimbali kwa lengo la kuwapa wanawake nafasi ya kupaaza sauti zao, ushiriki kwenye uongozi  na haki ya kunufaika na fursa za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, amesema kwamba mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo maafisa wa Halmahauri wanaofanya kazi katika ngazi ya Kata ambako kuna wajamii ili waweze kushirikisha jamii kikamilifu katika mchakato wa kuandaa mipango ya serikali ngazi ya Kata na vijiji

“Tumeandaa mafunzo haya baada ya kutambua kwamba, wapo maafisa katika ngazi ya chini ya mamkala za serikali za Mitaa, ambao wakielewa masuala ya Kijinsia wataweza kuvipa nafasi vipaumbele vya Kijinsia katika ngazi ya Jamii, wakati wa kuibua, pia wana nafasi kubwa ya kusimamia mchakato wa O&OD ukawa shirikishi Zaidi na wenye manufaa kwa jamii” alisema Lilian

Aidha ameongeza kwamba, washiriki wa mafunzo hayo kutokana na umuhimu wao na nafasi walizo nazo katika ngazi ya jamii, wanauwezo wa kutoa elimu katika jamii kupitia mikutano ya vitongoji na vijiji ili kuwafanya wanawake washiriki  lakini pia kujitokeza kugombea uongozi ili kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi ngazi ya Kijij na mtaa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian liundi, akizungumza na washiriki wa mafunzo 


Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa, ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Chuo, Utawala na Fedha, Dkt Lazaro Kisumbe,  Alisema kwamba, Chuo hicho kilifanya utafiti na kubaini kwamba kuna mapungufu  ya Kijinsia katika mamlaka za serikaali za Mitaa, ambayo yanakwamisha jitihada za serikali katika kupanga mipango na bajeti yenye mtazamo wa Jinsia. 

“ Mradi huu, unalenga kuondoa hili pengo la Kijinsia katika jamii,  ndio maaana kwa kushirikiana na Shirika la UNWomen na  TGNP tunalenga kujenga uwezo kwa wataalamu hawa ngazi ya kata, ili wanaaporudi wakatoe elimu hiyo kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) namna ya kuzungatia usawa wa Kijinsia wakati wa kuandaa mipango lakini pia kuweka nguvu kwenye vipaumbele vya Jamii” alisema.


Naibu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) Hombolo, anayesimamia Utawala, Mipango na Fedha, Dkt. Lazaro Kisumbe, akizungumza na washiriki wakati wa ufunguzi


Alisema kwamba, kupitia mafunzo hayo, wataalamu hao ngazi ya Kata, watawezesha kutambua mbinu za kwenda kukondoisha masuala ya Kijinsia katika ngazi ya Kata, na kuhaikisha wanawezesha masuala ya Kijinsia kueleweka katika ngazo zote.











Friday, January 26, 2024

Transforming Lives: The Success Story of Msimbati Peace Club

  


By Dr Fatma Waziri


In the coastal of Mtwara region, Msimbati Bay, the Msimbati Peace Club has emerged as a ray of positive change through their innovative peace dividend project.

The transformative initiative is part of the Dumisha Amani Project, which has now successfully concluded its first phase of implementation.  The project has been implemented jointly by Global Peace Tanzania and the Prime Minister’s office funded by UNDP in Tanzania. 

Focused on the sustainable livelihood of the community while promoting peace, the club members have effectively engaged in the buying and selling of fresh fish and sardines from the Indian Ocean . The proactive approach, marked by aggressive market strategies and branding initiatives, sets them apart as they proudly bring their sardines and fish, dried by the warm embrace of sunlight, to the market.

The club is formed by nine members of which 5 are women and 4 are men. Among the 3 peace clubs involved in the fish project, the youth of Msimbati Dumisha Amani  Peace club have demonstrated exceptional dedication and effort, showcasing a remarkable journey from despair to hope. They also, exemplify a spirit of resilience and determination in reinforcing their role as leaders in promoting peace and sustainable development.

Their journey is among powerful testimony to the success of the DumishaAmani project in the three region of Lindi, Mtwara, and Ruvuma. These young individuals are not only securing a sustainable livelihood but also leaving an indelible mark on their community, proving that peace, innovation, and economic progress go hand in hand.

"We are grateful to the support we have received from UNDP through GPF Tanzania, our business is thriving both in Msimbati and beyond. We are receiving numerous orders from Tandahimba, Nanyamba, and Mtwara, as well as Songea, and Newala. We make sure to safely deliver our goods to our customers," shares the Msimbati Peace Club, chairperson Juma Kambanga

"So far, within just two months, we have made a profit from our business. With this profit, we have initiated new ventures for sustainability and growth. We have established a small fresh vegetable shop (gege) selling tomatoes, potatoes, onions, okra, and ginger in bulk, selling them at our shop in Msimbati," he added.

Looking forward, they envision themselves self-sufficient in five years, "expanding our business, opening markets, and setting up stands in places like Mtwara town, Songea, and Nachingwea. Additionally, on a personal and family development level, we plan to purchase a large piece of land in Msimbati, divide it among ourselves, and name it the 'Msimbati Peace Club Land,'" Said Kambanga

The ambitions and determination to success colours their story whilst illustrating how Dumisha Amani project has significantly instilled a sense of purpose and unity among the youth of southern region boarding Mozambique which are prone to VE. They serve as living proof that when given the right tools and opportunities, the youth can lead the way towards positive transformation. 






Saturday, January 13, 2024

‘KALAMU’ YA KIBOSHO ILIVYOZALISHA WASOMI NA MAPROFESA

 

'Kalamu' ikiwa nchini wakati mwandishi akiendelea na mazungumzo na mfanyabiashara huyo




Na Deogratius Temba, 

KALAMU sio kitu kipya kwa watu wote, unaposikia neno ‘Kalamu’ kinachokujia kichwani ni ile inayotumika kuandikia kwenye karatasi au sehemu nyingine.

Huko Kibosho Moshi,mkoani Kilimanjaro, wanawake wafanyabiashara wadogo wa ndizi mbivu, wanaotokea maeneo ya Kibosho Kirima , kwao kalamu ni  aina ya Kibox ambacho hutumika kubeba ndizi mbivu, kilichotengenezwa kwa ustadi mkubwa na fundi seremala kwaajili ya kumwezesha kujitwisha kichwani na kusafiri nachO hadi Moshi mjini kwaajili ya kuuza ndizi. Kalamu hutumika kutunza usalama wa mikungu ya ndizi siziharibike.

Mwandishi akiinyanyua 'Kalamu'tayari kwaajili ya kumtwisha ili aendelee na mizunguko 


Hivi karibuni, wakati wa mapumziko ya sikukuu za Noeli (Krismas), nikakutana na Mama anayeitwa Maria Modest, ambaye ni mwenyeji wa Kibosho - Kirima masoka ambaye anaitumia ‘kalamu’ kuuzia ndizi zake.

Nilimuuliza, ni kwanini hii inaitwa ‘kalamu’? akasema “kwani hujui? Hii ilitumika tangu zamani sana, Bibi zetu ndio walikibatiza hiki kibox jina hilo” akasema Maria akifikiri kwamba mwandishi ni mgeni sana eneo hilo.

Mwandishi akimtwisha mfanyabiashara huyo 'kalamu'


Mwandishi: kwanini hao kina Bibi wa zamani, wajasiriamali walikiita jina hilo? Maria akajibu:  “ahaaaa, sasa ni kuambie, hao kina Bibi, walitusimulia kwamba walikiita hivyo kwa sababu walifanya biashara hii ya ndizi kwa kubeba kichwani na wakafanikiwa kuwasomesha watoto wao hadi wakafika vyuo vikuu”

Mwandishi:  ehheee! Hadi Vyuo vikuu kabisa? Ada inapatikana kwa hii biashara?

Maria: “ mhhhh, yaani mwanangu nikuambie, hata mimi ni shahidi, nimesomesha watoto wangu shule nzuri, wapo wawili, mmoja ameshamaliza Chuo Kikuu, na sasa amepata kazi, huyo mdogo wake yupo Chuo kikuu kingine, ninalipa ada shilingi 1,600,000 kwa biashara yangu hii, na mimi nina pata mahitaji yangu yote na matibabu” anaeleza maria kwa kujiamini.

Lakini maria anaeleza kwamba, wanawake wengi  hapo awali hawakuamini kwamba biashara ile ya kubeba ndizi kichwani itawakomboa, lakini kwa kuona wanawake wa Kibosho –Kirima Boro waliofanikiwa waliamua kuiga na sehemu nyingine.

Anaeleza kwamba, wakiwa wanashangaa wale wanaotokea maeneo ya Boro wanavyofanikiwa, wale wanaotokea maeneo ya Kirima Masoka, walikuja kuiga biashara hiyo na sasa wamefanikiwa sana.

“Mimi ninazaliwa kule Boro, lakini nimeolewa Masoka, kule Boro biashara hii ipo sana, wanawake karibia wote wenye afya nzuri wanafanya biashara hizi, upatikanaji wa ndizi mbichi kwaajili ya kufundika ni wa shida, lakini huku masoka ndizi zipo maana awali hakukuwa na ushindani mkubwa wa wanawake anaozifundika” anasema Maria.

Jitihada za wanawake wengi kufanya biashara kwa lengo la kujikombia kiuchumi zinafanikiwa kwa jinsi wao wenyewe wanavyoweka mtazamo chanya juu ya kile wanachokifanya wakiamini kwamba kitaleta tija. Suala muhimu ni serikali kuweka mifumo rafiki ya kuwawezesha kufanya biashara na kukutana na wateja wao bila kusukumwa, kunyang’anywa biashara zao na mgambo, au maafisa wengine.

Thursday, January 11, 2024

TGNP yapendekeza Jeshi la Polisi kutojihusisha na uchaguzi

 

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi, akiwasilisha mapendekezo ya Miswada ya sheria kwa mtazamo wa Kijinsia mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Dodoma

Na Deogratius Temba, Dodoma

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), imependekeza jeshi la Polisi Tanzania kutojihusisha na shughuli za kusimamia masuala ya ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi badala yake kuundwe kikosi maalum cha cha uchaguzi chini ya Tume ya taifa ya Uchaguzi kitakachohudumu  wakati wa mchakato wa uchaguzi pekee.

Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Bi. Gemma Akilimali akiteta jambo na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, katika viwanja vya Bunge muda mfupi baada ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Sheria na Katiba


Akizungumza wakati wa kuwasilisha maoni na mapendekezo ya maboresho ya miswaa mitatu (3), ambayo ni Mswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa mwaka 2023, Mswada wa sheria ya Uchaguzi wa Madiwani, wabunge na Rais wa mwaka 2023 na mswada wa marekebisho ya sheria ya mambo ya Vyama vya siasa ya mwaka 2019, ambao umewasilishwa Bungeni Oktoba 10,2023.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi, akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Bonephas Butondo, katika viwanja vya Bunge


Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, amesema kwama, ni vizuri Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC), ikaunda kikosi maalum cha kusimamia masuala ya usalama na ulinzi wakati wa uchaguzi, ambapo wahusika watajengewa uwezo namna ya kulinda usalama wa raia wote bila kusababisha changamto za uvunjivu wa Amani.



“.. Masuala ya ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi ni lazima yajitokeze bayana katika sheria hii ili kudhibiti vitendo vya uvunjivu wa Amani, Tunapendekeza kifungu kipya  cha 69 (1) kutakuwa na kikosi maalum cha Polisi watakaofanya kazi ya kulinda Amani na Utulivu wakati wote wa uchaguzi, kifungu cha 169 (2) Tume iwapatie mafunzo polisi wote wa kikosi cha Uchaguzi kuhusu masuala ya mchakato  wa uchaguzi ikiwepo unyanyasanji na udhalilishaji wa kijinsia” alisema Lilian




Pia, TGNP imependekeza kwamba, kuwepo kwa kifungu kipya cha 169 (3) kitakachosomeka kwamba, Polisi wa kikosi cha uchaguzi watakula kiapo cha uaminifu, na uadilifu mbele ya Hakimu wa mahakama ya mwanzo kabla ya kuanza majukumu ya kulinda usalama kwenye uchaguzi,

Pendekezo lingine ni kwamba kuwepo na kifungu cha 169 (4) ambapo Kikosi cha Polisi cha Uchaguzi kitaundwa kwa misingi ya uwiano wa Kijinsi yaani wanawake na wanaume hasa vijana wa kike na kiume.



Saturday, December 30, 2023

Kondoa DC yapongezwa kuzingatia bajeti yenye mtazamo wa Kijinsia


Na Mwandishi Wetu, Kondoa


Halmashauri ya wilaya ya kondoa, mkoani Dodoma, kwa mwaka wa fedha 2023/2024, imeandaa bajeti yenye mtazamo wa Kijinsia kwa kujenga miundombinu ya vyoo vya shule vyenye kukidhi mahitaji ya wasichana wanapokuwa kwenye hedhi.

Washiriki wa Uchambuzi wa Bajeti kwa mtazamo wa Kijinsia wakiwa katika Picha ya Pamoja na wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Kondoa


Hayo yalibainishwa na Afisa Mipango wa Halmashauri, Joshua Mnyang’ali, alipokuwa akijibu taarifa ya uchambuzi wa Bajeti ya Halmashauri kwa mtazamo wa Kijinsia iliyofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Vituo vya Taarifa na Maarifa Kata ya Haubi.

“Choo tulichojenga shule ya Msingi Mwisanga na shule mpya ya sekondari ya Ntomoko, vina vyumba maalumu ya kujisitiri wasichana wanapokuwa kwenye hedhi, kichomea taka kwaajili ya kuteketeza taulo za kike ambazo zimetumika. Pia katika vyoo tunavojenga sasa, tunaweka sehemu ya haja ndogo kwa wavulana, lengo ni kupunguza msongamano kwenye vyoo, ili wanafunzi wafurahie kuwepo shuleni. Kwa kufanya hivyo tunapunguza pia utoro na kuongeza ufaulu” alisema Mnang’ali.

Aidha  naye mganga mkuu wa halmashauri, Dkt Nelson Kimolo,  amesema kwamba, Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, imedhamiria kupunguza kabisa au ikiwezekana kutokomeza vifo vya mama na mtoto, kwa kutenga bajeti Zaidi ya shilingi Milioni 44 kwaajili ya kuwalipa madereva wa ngazi ya jamii watakaotumika kuwasafirisha Mama wajawazito kutoka zahanati kwenda Hospitali kubwa ili kurahisisha mfumo wa rufaa.

“Huu ni mradi unaojulikana kama M-MAMA ambao umeleta mabadiliko makubwa, unasaidia sana kuondoa tatizo la usafiri, magari tuliyo nayo ya kubeba wagonjwa hayatoshelezi, tumeona afadhal kuwa na utaratibu huu mpya wa kuingia mikataba na madereva waliko kwenye jamii, wahudumu wa Hospitali wawasilane nao muda wowote ili kuhakikisha Mama mjamzito anapata huduma ya haraka na kukokoa maisha yake” alisema Dkt.Kimolo

Awali akiwasilisha mapendekezo ya Jumla mwezeshaji wa Uchambuzi wa Bajaeti kutoka TGNP, Deogratius Temba, alisema kwamba, pamoja na halmashauri kuwa na vyanzo vichache vya mapato ya ndani, bado wamejitahidi kuangalia eneo la afya na elimu.

Temba, ameongeza kwamba, bado kuna mapengo ya kijinsia kwenye Bajeti ya Halmashauri hasa katka eneo la ustawi wa Jamii ambapo Bajeti ya kuzuia na kutokomeza Ukatili wa Kijinsia imetengwa kidogo, sambamba na Idara ya Maendeleo ya Jamii inayotakiwa kuwajibika katika uhamasishaji wa jamii kushiriki katika shughuli na maendeleo kutengewa fedha kidogo sana.

“eneo la Ukatili wa Kijinsia, ni muhimu kuliangalia,tukiwekeza kwenye miundombinu ya elimu, alafu tusipoweka mikakati ya kuwalinda watoto wa kike na kiume wasifanyiwe ukatili wa Kijinsia na udhalilishaji wakingono, hatutapata matokeo mazuri”alisema Temba.

Pia, aneo linguine lenye mapungufu ambalo Halmashauri imeshauriwa kuboresha na kuongeza msisistizo kwa viongozi wa vijiji na kata kuwashirikisha wananchi kwenye mchakato wa kuandaa bajeti ili waweze kuibua fursa na vikwazo katika maendeleo (O&OD) ili waweze kushiriki vizuri katika kuisimamia na kuitekeleza miradi ya maendeleo.

Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2023/24 imepanga kutumia kiasi cha shs.milion 440 kuboresha vyanzo vya maji, sh. Million 3, kujenga vichomea taka katika zahanati, sh. Million 23 kujenga mashimo ya taka mbichi (placenta pit) katika zahanati na vituo vya afya, ambapo Kituo cha afya mnenia kimetengewa bajeti ya sh. Million 35 kwaajili ya kujenga kichomea taka  na vyoo.

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), inatekeleza miradi mbalimbali katika halmashauri ya Kondoa, inayolenga kujenga uwezo wa kwa jamii kupitia Kituo cha taarifa na Maarifa, kupata uwezo wa kuchambua masuala ya Kijinsia na kushawishi kuingzwa kwa masuala ya Kijinsia katika sera, mipango na miongozo. Sambamba na kuwajengea uwezo viongozi mbalimbali wa Halmashauri kuhusu masuala ya Usawa wa Kijinsia na Uongozi bora na ushiriki wa wanawake katika uongozi. 









Tuesday, December 19, 2023

Rushwa ya ngono tishio umilikishwaji ardhi Kibaha

 

Na Mwandishi wetu, Kibaha

Wananchi kutoka kata ya Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mji, wanaoshiriki utafiti wa kiraghibish unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wametoa malalamiko ya uwepo wa baadhi ya viongozi wa serikali za Mitaa wanaodai rushwa ya ngono kwa wanawake ili waweze kuwasaidia kupata huduma ya urasimishaji ardhi kwa bei nafuu.



Wakiwasilisha matokeo ya utafiti raghibish uliofanywa na Jamii hiyo, wakati wa mrejesho ngazi ya Halmashauri kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa “ Uimarishaji wa Sauti za wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu katika uongozi na haki ya kumiliki rasilimali” unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UNwomen), washiriki hao wapatao 30 walisema kwamba mchakato wa upimaji na umilikishaji wa ardhi katika kata hiyo yenye mitaa nane umegubikwa na vitendo vya kuomba rushwa ya pesa na rushwa ya ngono kwa wanawake

“Jamii yenye migogoro haiwezi kupata ustawi na maendeleo, tunaomba jambo hili liishe kwa kufikia mawisho.tumebaini kwamba baadhi ya viongozi wanautumia mgogoro huu kuomba rushwa ya pesa na rushwa ya ngono kwa wanawake ili wawapunguzie gharama za kulipia upimaji na urasimishaji” alisema Malaki … ambaye alikuwa msoma risala.

Washiriki hao, wakiwasilisha mapendekezo yao kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Charles Marwa, wamesema kwamba, pamoja na mapendekezo hayo, pia wameandaa mpango kazi ambao watautekeleza sambamba na viongozi wao. Kikao kazi hicho kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani hapo, pia kimehudhuria na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo pamoja na Mkuu wa dawati la Jinsia Polisi

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alistuka kusikia hivyo na kuahidi kufuatilia mara moja kwa kutuma timu kuchunguza ukweli wa jambo hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa haraka.

“jambo hili la rushwa ni bay asana, tena rushwa ya ngono, mtu anataka akunyime haki yako tu ilia pate ngono, tunataka tupate ushahidi wa kutosha wa hili, naomba mtupe ushirikiano ili tulifanyie kazi” alisema Marwa.