Na Deogratius Temba, Dodoma
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), imependekeza jeshi la
Polisi Tanzania kutojihusisha na shughuli za kusimamia masuala ya ulinzi na
usalama wakati wa uchaguzi badala yake kuundwe kikosi maalum cha cha uchaguzi
chini ya Tume ya taifa ya Uchaguzi kitakachohudumu wakati wa mchakato wa uchaguzi pekee.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha maoni na mapendekezo ya
maboresho ya miswaa mitatu (3), ambayo ni Mswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi wa mwaka 2023, Mswada wa sheria ya Uchaguzi wa Madiwani, wabunge na
Rais wa mwaka 2023 na mswada wa marekebisho ya sheria ya mambo ya Vyama vya
siasa ya mwaka 2019, ambao umewasilishwa Bungeni Oktoba 10,2023.
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi, akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Bonephas Butondo, katika viwanja vya Bunge |
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, amesema kwama,
ni vizuri Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC), ikaunda kikosi maalum cha kusimamia
masuala ya usalama na ulinzi wakati wa uchaguzi, ambapo wahusika watajengewa
uwezo namna ya kulinda usalama wa raia wote bila kusababisha changamto za
uvunjivu wa Amani.
“.. Masuala ya ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi ni
lazima yajitokeze bayana katika sheria hii ili kudhibiti vitendo vya uvunjivu
wa Amani, Tunapendekeza kifungu kipya
cha 69 (1) kutakuwa na kikosi maalum cha Polisi watakaofanya kazi ya
kulinda Amani na Utulivu wakati wote wa uchaguzi, kifungu cha 169 (2) Tume
iwapatie mafunzo polisi wote wa kikosi cha Uchaguzi kuhusu masuala ya
mchakato wa uchaguzi ikiwepo
unyanyasanji na udhalilishaji wa kijinsia” alisema Lilian
Pia, TGNP imependekeza kwamba, kuwepo kwa kifungu kipya cha
169 (3) kitakachosomeka kwamba, Polisi wa kikosi cha uchaguzi watakula kiapo
cha uaminifu, na uadilifu mbele ya Hakimu wa mahakama ya mwanzo kabla ya kuanza
majukumu ya kulinda usalama kwenye uchaguzi,
Pendekezo lingine ni kwamba kuwepo na kifungu cha 169 (4)
ambapo Kikosi cha Polisi cha Uchaguzi kitaundwa kwa misingi ya uwiano wa
Kijinsi yaani wanawake na wanaume hasa vijana wa kike na kiume.
No comments:
Post a Comment