Tuesday, December 19, 2023

Rushwa ya ngono tishio umilikishwaji ardhi Kibaha

 

Na Mwandishi wetu, Kibaha

Wananchi kutoka kata ya Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mji, wanaoshiriki utafiti wa kiraghibish unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wametoa malalamiko ya uwepo wa baadhi ya viongozi wa serikali za Mitaa wanaodai rushwa ya ngono kwa wanawake ili waweze kuwasaidia kupata huduma ya urasimishaji ardhi kwa bei nafuu.



Wakiwasilisha matokeo ya utafiti raghibish uliofanywa na Jamii hiyo, wakati wa mrejesho ngazi ya Halmashauri kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa “ Uimarishaji wa Sauti za wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu katika uongozi na haki ya kumiliki rasilimali” unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UNwomen), washiriki hao wapatao 30 walisema kwamba mchakato wa upimaji na umilikishaji wa ardhi katika kata hiyo yenye mitaa nane umegubikwa na vitendo vya kuomba rushwa ya pesa na rushwa ya ngono kwa wanawake

“Jamii yenye migogoro haiwezi kupata ustawi na maendeleo, tunaomba jambo hili liishe kwa kufikia mawisho.tumebaini kwamba baadhi ya viongozi wanautumia mgogoro huu kuomba rushwa ya pesa na rushwa ya ngono kwa wanawake ili wawapunguzie gharama za kulipia upimaji na urasimishaji” alisema Malaki … ambaye alikuwa msoma risala.

Washiriki hao, wakiwasilisha mapendekezo yao kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Charles Marwa, wamesema kwamba, pamoja na mapendekezo hayo, pia wameandaa mpango kazi ambao watautekeleza sambamba na viongozi wao. Kikao kazi hicho kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani hapo, pia kimehudhuria na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo pamoja na Mkuu wa dawati la Jinsia Polisi

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alistuka kusikia hivyo na kuahidi kufuatilia mara moja kwa kutuma timu kuchunguza ukweli wa jambo hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa haraka.

“jambo hili la rushwa ni bay asana, tena rushwa ya ngono, mtu anataka akunyime haki yako tu ilia pate ngono, tunataka tupate ushahidi wa kutosha wa hili, naomba mtupe ushirikiano ili tulifanyie kazi” alisema Marwa. 








No comments:

Post a Comment