Tuesday, November 1, 2022

KAMPENI YA KUPINGA UKEKETAJI TARIME 2022 YAPAMBA MOTO

Na Mwandishi wetu

Vituo vya Taarifa na Maarifa chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Mkoa wa Mara hivi karibuni viliamua kufanya kampeni ya kupinga ukeketaji ili kupunguza wimbi kubwa la watoto wa kike kukeketwa kama mila za kikurya zilivyo.

Baadhi ya wasichana wa Kata ya Nyakonga, Wilaya ya Tarime walioshiriki katika kampeni ya kutokomeza Ukeketaji iliyoendeshwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa, Nyakonga



Viongozi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa wakiwa na wadau wengine wakati wa Kampeni ya kuzuia Ukeketaji


Jamii hiyo ambayo imejengewa uwezo na TGNP, ilifanya tathimini na kugundua kwamba, kuna koo ambazo zinakeketa watoto wa kike kila mwaka unaogawanyika kwa mbili, na koo nyingine zinakeketa mwaka ambao haugawanyiki kwa mbili.




Hivyo katika mwaka huu ukeketaji unatarajiwa kufanyika mwezi Dec 2022 ambapo wanavituo waliamua kutoa elimu kupitia mbinu mbalimbali katika kampeni ya kupinga ukeketaji.

Vituo vya Taarifa na Maatifa vilitumia mbinu mbalimbali ili kuhakikisha wanawafikia watu wengi kadri inavyowezekana. Baadhi ya mbinu hizo ni:-

LIGI YA MPIRA WA MIGUU WA WATOTO WA KIKE

Kituo cha Taarifa na Maarifa  kata ya Nyakonga na Regicheri  walifanya bonanza fupi la ligi ya mpira wa miguu kwa watoto wa kike, ambapo ligi hiyo ilichukua  muda wa wiki moja (siku 7) ligi ilikuwa ikiambatana na elimu mbalimbali juu ya ukatili wa kijinsia ikiwemo na ukeketaji.

Washindi wa Kombe za kampeni ya kutokomeza Ukeketaji Tarime baada ya kupokea zawadi yao ya Mbuzi



 



Wanavituo walitumia mifuko ya vituo ambao inatokana na mapato mbalimbali ya miradi tuliyonayo kwenye vituo  vyetu pamoja na michango mbalimbali ya wanakituo  na  wadau mbalimbali,  zikanunuliwa zawadi mbalimbali kama vile mbuzi, kuku, soda, maji nk kwa ajili ya kutoa zawadi kwa washindi wa ligi hiyo.

 

Wazee wa mila na koo wakiwa wanasikiliza kwa makini mafundisho yaliyokuwa yakitolewa wakati wa michezo na mikutano mbalimbali ndani ya kata ya Nyakonga

 Ligi hiyo ilianza Septemba 27, 2022 na kumalizika Oktoba 04,2022 ikafanyika fainali na washindi kupewa zawadi zao.

 

Jedwali hapo chini linaonyesha  walionufaika na bonanza hili kwa kupata elimu juu ya ukeketaji.

KITUO

Watoto

wa kike

Watoto wa kiume

Watu wazima

jumla

KE

ME

NYAKONGA

314

211

43

64

632

REGICHERI

127

89

38

51

305

JUMLA

431

300

81

115

937

 

 

Kati ya  watoto wa kike waliofikiwa na elimu hii ni 431  kati yao watoto 217 wapo katika hatari kubwa ya kufanyiwa ukeketaji  Dec mwaka huu 2022.

 

MIKUTANO YA WANAUME PEKEE NA WANAWAKE  PEKEE

Ilifanyika mikutano ya wanawake pekee, hii ilisaidia kujua kwa undani kwa nini ukeketaji unaendelea katika jamii zetu, hivyo elimu ilitolewa  kwa wakina mama hao, ambapo jumla ya wanawake 82 walipata elimu hiyo.

 

Pia ilifanyika mikutano ya wakina baba ambapo wakina baba walikuwa huru kujieleza ni kwa nini ukeketaji unafanyika, wengine walijibu kuwa ni tama za baadhi ya wazazi kuwaodhesha watoto wao na kupata ng’ombe nyingi, wengine walisema ni mazoea ya mila na desturi na wengine walisema mtoto akikeketwa analeta heshima kwenye familia zao. Hivyo sisi kama wanakituo tulitoa elimu ya madhara ya ukeketaji na kuwasihi kubadili mitazamo yao ili kutengeneza jamii yenye mtazamo chanya. Jumla wa wanaume waliopata elimu hii walikuwa  64

 

KITUO

WANAUME

WANAWAKE

JUMLA

NYAKONGA

64

82

146

 

 

 

 

                  

Baada ya kampeni hii kukamilika tuliandaa mpango kazi ambao utatuongoza katika kuhakikisha elimu inawafikia watu wengi zaidi ili wanajamii waweze kubadilika na kuacha ukeketaji.

 

 CHANGAMOTO

Pamoja na jitihada zote tulizozifanya  bado tulikuwa na baadhi ya mapungufu katika kutekeleza majukumu yetu hasa upande wa kipato hakikuwa cha kutosha kuweza kufanya vitu vikubwa zaidi. Lakini pia tunaomba upande wa TGNP iweze kutupa nguvu zaidi katika kupambana na ukeketaji katika jamii zetu hasa semina/warsha/matamasha madogomadogo ya  mara kwa mara yakiwashirikisha  viongozi wa serikali, viongozi wa mila na viongozi wa dini, pia kuna baadhi ya wavituo wanaotakiwa kujengewa uwezo zaidi katika mapambano haya dhidi ya  ukeketaji.

 

No comments:

Post a Comment