Tuesday, December 19, 2023

Rushwa ya ngono tishio umilikishwaji ardhi Kibaha

 

Na Mwandishi wetu, Kibaha

Wananchi kutoka kata ya Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mji, wanaoshiriki utafiti wa kiraghibish unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wametoa malalamiko ya uwepo wa baadhi ya viongozi wa serikali za Mitaa wanaodai rushwa ya ngono kwa wanawake ili waweze kuwasaidia kupata huduma ya urasimishaji ardhi kwa bei nafuu.



Wakiwasilisha matokeo ya utafiti raghibish uliofanywa na Jamii hiyo, wakati wa mrejesho ngazi ya Halmashauri kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa “ Uimarishaji wa Sauti za wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu katika uongozi na haki ya kumiliki rasilimali” unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UNwomen), washiriki hao wapatao 30 walisema kwamba mchakato wa upimaji na umilikishaji wa ardhi katika kata hiyo yenye mitaa nane umegubikwa na vitendo vya kuomba rushwa ya pesa na rushwa ya ngono kwa wanawake

“Jamii yenye migogoro haiwezi kupata ustawi na maendeleo, tunaomba jambo hili liishe kwa kufikia mawisho.tumebaini kwamba baadhi ya viongozi wanautumia mgogoro huu kuomba rushwa ya pesa na rushwa ya ngono kwa wanawake ili wawapunguzie gharama za kulipia upimaji na urasimishaji” alisema Malaki … ambaye alikuwa msoma risala.

Washiriki hao, wakiwasilisha mapendekezo yao kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Charles Marwa, wamesema kwamba, pamoja na mapendekezo hayo, pia wameandaa mpango kazi ambao watautekeleza sambamba na viongozi wao. Kikao kazi hicho kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani hapo, pia kimehudhuria na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo pamoja na Mkuu wa dawati la Jinsia Polisi

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alistuka kusikia hivyo na kuahidi kufuatilia mara moja kwa kutuma timu kuchunguza ukweli wa jambo hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa haraka.

“jambo hili la rushwa ni bay asana, tena rushwa ya ngono, mtu anataka akunyime haki yako tu ilia pate ngono, tunataka tupate ushahidi wa kutosha wa hili, naomba mtupe ushirikiano ili tulifanyie kazi” alisema Marwa. 








Haya hapa mapendekezo 11 ya wakazi wa Kibaha kwa Halmashauri


Na Deogratius Temba, Kibaha

Wananchi kutoka kata ya Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mji, wanaoshiriki utafiti wa kiraghibish unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wametoa mapendekezo yao 11, yanayotokana na changamoto zilizoibuliwa wakati wa zoezi hilo lililoanza mapema mwezi huu

Picha ya pamoja ya washiriki wa kikao kazi cha mrejesho wa utafiti raghibish ngazi ya  Halmashauri, uliofanywa na TGNP , katika Halmashauri ya Kibaha Mji

Kikao kazi hicho cha mrejesho ngazi ya Halmashauri ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa “ Uimarishaji wa Sauti za wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu katika uongozi na haki ya kumiliki rasilimali” unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UNwomen).

Washiriki hao, wakiwasilisha mapendekezo yao kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Charles Marwa, wamesema kwamba, pamoja na mapendekezo hayo, pia wameandaa mpango kazi ambao watautekeleza sambamba na viongozi wao. Kikao kazi hicho kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani hapo, pia kimehudhuria na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo.

“Kutokana na hayo hapo juu, kutokana na changamoto kubwa zilizoibuliwa ambazo ni Uongozi usiowajibika na usiozingatia uwakilishi wa Kijinsia, Mila na desturi kandamizi, umiliki wa ardhi na rasilimali nyingine na Ukatili wa kijinsia hasa mimba za utotoni.  Biashara haramu ya ngono inachochea mmomonyoko wa maadili,  na kuongeza matukio ya Ubakaji kwa wanawake hasa wasichana, kuongezeka kwa uporaji na migogoro mikubwa ya ndoa ambayo inaadhiri kwa kiasi kikubwa watoto” amesema mwasilishaji wa mapendekezo hayo”alisema mwasilishaji. 

 

Tunapendekeza yafuatayo kwa ujumla wake yafanyiwe kazi.

 

  1. Kutokana na suala la uongozi usiowajibika kuibuka, na kukosekana kwa uwakilishi wa Kijinsia katika uongozi, na kupelekea kukosekana kwa sauti za wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu kwenye maamuzi. Elimu ya usawa wa kijinsia itolewe kwa viongozi walioko madarakani, viongozi wa vyama vya siasa kuanzia ngazi za chini hadi wilaya.
  2. Viongozi walioko madarakani katika mitaa, wajengewe uwezo ili kujua mipaka ya kiutendaji, uwajibikaji, uandaaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia vipaumbele vyenye mtazamo wa Kijinsia, ushiriki wa wananchi kwenye mchakato wa O&OD
  3. Halmashauri isimamie mchakato wa uandaaji wa bajeti uwe shirikishi kuanzia ngazi za mitaa ili kuwepo kwa bajeti yenye mrengo wa Kijinsia itakayogusa mahitaji ya kila kundi na kuwezesha wanawake kumiliki rasilima.
  4. Halmashauri kwa kushirikiana na TARURA izipe kipaumbele barabara zinazounganisha Kata ya Pangani na Mji wa Kibaha ili kurahisisha usafiri na kupunguza kiwango cha umasikini kwa jamii  na kupunguza vifo vya mama na mtoto.
  5. Mwaka wa fedha 2024/25, Halmashauri itenge bajeti kwenye mapato yake ya ndani, kwaajili ya kugharamikia urasimishaji wa ardhi na mipango miji ili kupunguza mzigo wa gharama kubwa za upimaji kwa wananchi hasa wanawake na watu wenye ulemavu, lakini pia fedha hizo zitarudi kupitia kodi itakayolipwa baada ya kumilikishwa.
  6. Kuhuisha kamati za Ulinzi wa Mama na Mtoto (MTAKUWWA) katika kata na Mitaa yote, zitambue majukumu yake na mfumo wa uwajibikaji yaani ziwe na taarifa zake za utekelezaji.
  7. Bado tuna kundi la wanawake wasiojua kusoma na kuandika katika kata ya pangani.Tunashauri kuondoa tatizo hili  mwongozo wa kuwarudisha  wanafunzi walioacha masomo kwa sababu mbalimbali uanze kutumika ndani ya Kata ya Pangani. Mratibu Elimu Kata (MEK) aanze kuwabaini wasichana walioko mitaani na kuwarudisha shuleni kwa mujibu wa mwongozo au waraka wa Elimu namba 1 wa mwaka 2022.
  8. Halmashauri isaidie usimamizi  na utekelezaji wa sheria ndogo ambazo zitathibiti watoto wa shule kuzurura hovyo mitaani, kila shule itoe huduma ya chakula kwa wanafunzi, watoto kutokushiriki ngoma na mikesha ya usiku ya ngoma, kufunga sehemu zote zenye ‘ubanda’ panapofanyika biashara haramu ya ngono na mabanda mengine ya kuonyesha video yadhibitiewe watoto wasiingie.  
  9. Sheria kali zichukuliwe dhidi ya kutokomeza Mimba na ndoa za utotoni. Maafisa Ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii washirikiane na dawati la Jinsia na Mtoto-Polisi, kuharakisha kesi za ubakaji na wanaobainika wahukumiwe kwa mujibu wa sheri zetu.
  10. Kutenga bajeti kwaajili ya kupeleka maji kwa mitaa sita (6) kati ya Minane (8), ya Kata ya Pangani ambayo haina maji kabisa, hii inapelekea kuongezeka kwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia
  11. Katika uibuaji, kulijitokeza tatizo la kukidhiri kwa rushwa ya pesa na rushwa ya ngono ili kupata huduma, hasa urasimishaji wa ardhi. Tunashauri, viongozi wa serikali za Mitaa wajengewe uwezo ili wazingatie uadilifu, maadili ya uongozi na utawala bora.











 

Monday, December 18, 2023

Traditional dances contribute to teenage pregnancy in Kibaha


By  Deogratius Koyanga, Kibaha

The existence of traditional dances that young girls play in the Pwani region has contributed to the existence of early marriage and pregnancy and has prevented girls from reaching their goals, including becoming leaders in the community.


Pangani Ward in Kibaha Town Council leaders and Participatory Action Research (PAR) 
participants, during the ward-level feedback 


Speaking during a ward-level feedback session on the participatory action research (PAR) conducted by Tanzania Gender Networking Programme (TGNP), for ward leaders at Pangani ward, Kibaha Town Council, in Pwani Region, the ward councillor, Augustino Mdachi, said that teenage pregnancy is caused to a large extent by the presence of customs and traditions that lead to children being exposed to risky environments.

The councillor also said that another reason is the walking distance to secondary school education, as girls have to walk long distances from the Vikawe streets to Kidimu Secondary School, which is located in the ward headquarters.


Participants presented the key issues through the ward map. 


The participatory action research, which involves community-based research, was conducted by the Tanzania Gender Network (TGNP), as part of the implementation of the project to empower the voices of women, girls and people with disabilities in leadership and the right to own resources, funded by UNWomen in the council.

TGNP and UNWomen are working with the Kibaha Town Council to build capacity for the community to change attitudes, customs and traditions that contribute to women, girls and people with disabilities being unable to participate in leadership and decision-making positions at various levels and to look at the challenges that contribute to this group not owning resources.



"The distance problem is the source of these childhood pregnancies, which contribute to a large extent to girls losing their dream of getting an education and becoming tomorrow's leaders. For example, girls who walk the entire distance from Vikawe to Kidimu are a major problem and can lead to pregnancy. We are continuing with the process, we have already started the process of getting another secondary school in Vikawe to solve this problem."

 

Findings presented through the Poem 

The PAR participants also proposed that if parents protect their daughters by preventing them from participating in traditional dances, and ensuring that only those who have reached the age of adolescence and adulthood are involved in traditional dances like ‘Unyago’, the problem of teenage pregnancy will end. They also proposed that girls who are involved in  ‘unyago’ dances should not be released from inside with their chests exposed, as this humiliates them and makes them lose the courage to be leaders or to stand in front of people.

Cartoons and pictures were used to provoke debate among the Participants


The Vikawe Street chairperson, Anas Bwanari, said that teenage pregnancy is a major problem in his street, and the reasons he sees are due to marital conflicts, the existence of divorce, where children are raised by one parent or by foster parents who also abused them sexually.

"….. sexual violence prevents women from achieving their goals, including owning resources, benefiting from existing resources and becoming good leaders of tomorrow. We recommend the existence of self-awareness education for the entire community, to eliminate the problem of teenage pregnancy, but also to reduce sexual violence against women."

Earlier, giving details about the feedback exercise that took place, the PAR facilitator from TGNP, Deogratius Temba, said that after leading the community to conduct participatory action research, various issues have been identified and ranked in priorities, where the issue of irresponsible leadership, teenage pregnancy and oppressive customs and traditions were seen as the reason why women, girls and people with disabilities are unable to participate fully in leadership and decision-making positions and also in resource ownership.

Participatory action research  (PAR), conducted by TGNP aims to build communities from an gender analytical perspective by identifying opportunities and challenges that surround them, analyzing the obvious causes, and the root causes of the problem, and setting up action plans to implement or make recommendations for solving the problem.

It is a concept used to change communities from a perspective of relying on the government to do everything and making communities propose their solutions using the resources surrounding them in collaboration with leaders. It also removes conflicts between communities and their leaders.

Drama 






















Ngoma, unyago zachangia mimba za utotoni Kibaha

Na Mwandishi wetu 

Uwepo wa ngoma za jadi wanazochezwa wasichana wadogo kwa jamii ya Mkoa wa Pwani kumechangia uwepo wa ndoa na mimba za utotoni na kusababisha wasichana kuhsindwa kufikia ndoo zao ikiwepo kuwa viongozi katika jamii.
Picha ya pamoja kati ya Viongozi wa Kata na washiriki wa Uraghibish, baada ya mrejesho wa Kata na kusikia mtazamo wa viongozi kutokana na amsuala yaliyoibuliwa

Akizungumza wakati wa zoezi la mrejesho wa uraghibishi (PAR), kwa viongozi wa Kata ya Pangani, Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoani Pwani, Diwani wa kata hiyo, Augustino Mdachi, Alisema kwamba Mimba za utotoni zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa mila na desturi zinazopelekea watoto wa kike kuingizwa kwenye mazingira ya vishawishi na hatarishi. Aidha, Diwani huyo amesema pia, sababu nyingine ni umbali wa kupata elimu ya sekondari kwani wanafunzi wanatembea umbali mrefu kutoka mitaa ya Vikawe Bondeni na Vikawe shule kwenda shule ya sekondari Kidimu iliyoko makao makuu ya Kata.

washiriki wakiwa katika kujadili picha chokozi za katuni


 Uraghibish huo ambao unahusisha utafiti shirikishi wa jamii, umefanywa na shirika lisilo la kiserikali la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa kuwezesha sauti za wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu, katika uongozi na haki ya kumiliki rasilimali, unaofadhiliwa na shirika laUmoja wa Mataifa linaloshughuikia masuala ya wanawake (UNWomen) katika halmashauri hiyo. TGNP na UNwomen wanashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, kujenga uwezo kwa jamii, kujitambua, kubadilisha mitazamo, mila na desturi ambazo zinachangia wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu, kushindwa kushiriki kwenye nafasi za uongozi na maamuzi katika ngazi mbalimbali na kuangalia vikwazo vinavyochangia kundi hilo kutokumiliki rasilimali. 

washiriki wakiwasilisha ramani ya Kata, kuonesha fursa na changamoto na maeneo hatarishi kwa jamii


 “Tatizo la Umbali ni chanzo cha hizi mimba za utoto ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa wasichana kupoteza ndoto yao ya kupata elimu na kuja kuwa viongozi wa kesho. Mfano wasichana wanaotembea umbali wote kutoka Vikawe hadi Kidimu ni tatizo kubwa na linaweza kusababisba mimba. Tunaendelea na utaratibu,tumeshaanza mchakato wa kupata shule nyingine ya sekondari Vikawe ili kuondoa tatizo hilo” Aidha, washiriki wa Utafiti huo walipendekeza kwamba, endapo wazazi watawalinda watoto wa kike, kwa kuzuia ushiriki wao kwenye ngoma za unyago, na kuhakikisha wanaochezwa unyago ni wale waliofikia umri wa ujana na utu uzima, tatizo la mimba za utotoni litakoma. 
washiriki wakiigiza kuonesha jinsi ndoa za utotoni zinavyojitokeza kwenye kata hiyo kutokana na ngoma za unyago wanazo chezwa wasichana wadogo



Pia walipendekaza kuzuia wasichana wanaochezwa ngoma za unyago kutokutolewa ndani wakiwa kifua wazi kwani inawadhalilisha na kuwakosesha ujasiri wa kuwa viongozi au kusimama mbele za watu.f Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Vikawe Anas Bwanari, alisema kwamba kwenye mtaa wake mimba za utotoni ni tatizo kubwa ambapo sababia anazo ziona yeye ni kutokana ana migogoro ya ndoa, uwepo wa talaka, ambapo watoto wanalellewa na mzazi mmoja au kulelewa na wazazi wa kufikia ambao pia huwafanyia vitendo vya Ukatili wa KIjinsia. “vitendo vya Ukatili wa Kijinsia vinasababisha wanawake kushindwa kufikia malengo yao, ikiwepo kumiliki rasilimali, kunufaika na rasilimali zilizopo na kuwa viongozi wazuri wa kesho. Tunashauri uwepo wa elimu yakujitambua kwa jamii nzima, ili kuondoa tatizo la mimba za utotoni, lakini pia kupunguza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake”alisema Awali akitoa maelezo juu ya zoezi hilo lilofanyika, Mwezshaji wa uraghibish kutoka TGNP, Deogratius Temba, alisema kwamba, baada ya kuwaongoza wanajamii kufanya uraghibish masuala mbalimbali yameibuliwa na kupangwa katika vipaumbele, ambapo suala la Uongozi usiowajibika, Mimba za utotoni na mila na desturi kandamizi yalionekana ni sababu ya wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu kushindwa kushiriki kikamilifu kwenye nafasi za uongozi na maamuzi na pia katika umiliki wa rasilimali. Uraghibishi unaofanywa na TGNP, unalenga kuijenga jamii, katika mtzamo wa kiuchambuzi kwa kuibua fursa na changamoto zinazowazunguka, kuchambua sababu za wazi, za kina kiini cha tatizo, na kuweka mikakai ya kutekeleza au kutoa mapendekezo ya utatuzi wa tatizo. Ni dhana inayotumika kuibadilisha jamii kutoka katika mtazamo wa kuitegemea serikali kufanya kila kitu, na kuifanya jamii kupendekeza njia zao za utatuzi kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka kwa kushirikiana na viongozi. Na pia inaondoa migogoro kati ya jamii na viongozi wao.