NAFASI YA MWANAUME KATIKA KULEA WATOTO NJITI
·
Malezi ya Kangaroo yanahitaji wanaume
kushiriki
·
Baadhi ya wanaume hulazimika kufunga
biashara, kulea
·
Likizo ya uzazi kwa wanaume
yashauriwa
Deogratius Temba, Mwandishi wa makala hii akizungumza na Ndugu Mohamed, wakati wa mahojiano maalum |
Na Deogratius Temba
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ipo katika
mchakato wa kufanya marakebisho kwenye sheria kuu ya Ajira na mahusiano Kazini, sura ya 366, ambapo moja
ya kifungu cha sheria hiyo kinachofanyiwa marakabisho ni pamoja na kuongezwa
kwa muda wa likizo kwa wanawake wanaojifungua watoto njiti.
Kifungu kinaeleza kwamba Mama aliyezaa motot njiti ataendelea
kuwa likizo yenye malipo hadi zitimie wiki ya 36 ya ujauzito na baadaye
aendelee na likizo yake ya uzazi kama kawaida.
Katika mswada huo, marakabisho yanafanyika kwenye sheria ya
msingi ya awali kwamba: Kifungu cha 33 cha muswada kinaeleza kwamba “ Sheria inarekebishwa katika kifungu cha 33
kwa- (a) kuongeza mara moja baada ya kifungu kidogo (7) yafuatayo: "(8)
Mfanyakazi anayezaa mtoto kabla ya muda wake ana haki ya likizo ya uzazi
iliyolipwa kuanzia tarehe ya kujifungua hadi kukamilika kwa wiki thelathini na
sita za ujauzito na hadi kipindi cha likizo ya uzazi kilichotolewa chini ya
kifungu kidogo (6) katika mzunguko wa likizo.";
Inaelezwa kwamba, lengo la marekebisho haya ya sheria, sio
upendeleo tu kwa wanawake, bali inalenga kulinda ustawi wa afya za watoto
wanaozaliwa kabla ya wakati na kuhitaji muda wa kutosha wa aungalizi wa mama na
Baba. Mtandao wa Haki ya Afya ya Uzazi
(SRHR), unaoratibiwa na Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT-T) wanapendekeza kuwepo
kwa likizo ya kutosha ili kuhakikisha kwamba wanawake na wanaume wanapata
nafasi ya kumlea mtoto njiti bila tatizo.
Mtandao wa Haki ya Afya ya Uzazi, wakiongozwa na shirika la
Doris Moleli Foundation, Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), chini ya usimamizi wa WFT-T wanasema kwamba,
ili kuongeza tija katika uzalishaji mali nchini na kujenga taifa la wetu wenye
afya njema na nguvu kazi ya baadaye ni lazima kulinda afya na ukuaji wa watoto
njiti.
“Kifungu kina tija kwa wafanyakazi waliojifungua kabla ya
muda ili kuruhusu mzazi kuhudumia mtoto kwa ukaribu ili atengemee isipokua siku
zilizotajwa hapo ziongezeke kutoka wiki 36 mpaka wiki 40 kwa sababu za Kiafya
hasa makuzi ya mtoto” linasema moja ya pendekezo la Mtandao huo kwa kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii waliowasilisha kuhusu muswada huo. Mtandao wa SHRSR, TUCTA na wengine
wanapendekeza kwamba likizo ya malipo ya
wiki za kabla ya kujifungua ambazo mama angekuwa hajajifungua ziongezeke hadi
wiki 40 kwasababu wanawake wengi hujifungua kati ya wiki ya 36 hadi 40 na ndipo
ianze likizo rasmi ya uzazi.
Likizo inayopendekezwa ni kwa wanawake (Mama anayejifungua)
na mume wake kwasababu za msingi ambazo ni kwamba, mtoto njiti anahitaji malezi
ya pande zote na pia Mama aliyejifungua anahitaji usaidizi wa mwenza wake
wakati huu.
Kwa mujibu wa sheria kuu ya ajira na mahusiano kazini nchini
Tanzania, sura ya 366, vifungu 33 na 34
vinavyozungumzia likizo za watumishi, hakuna kabisa suala la likizo ya mama
anayejifungua mtoto njiti, lakini kutokana na marekebisho haya yam waka 2025,
kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa imegusia suala la mtoto njiti kwenye sheria.
Kifungu cha 34 cha sheria n ahata kwenye muswada, hakielezi kuhusu likizo ya uzazi kwa wanaume
ambao wenza wao wanajifungua watoto njiti, hii inamkosesha baba nafasi ya
kushiriki katika kumhudumia mtoto wake au
kumsaidia mwenza wake jukumu ya akulea.
Jambo la msingi la la kiafya kwa mtoto aliyezaliwa Njiti, ni
kutunzwa kwa mfumo wa Kangaroo, ambao unamuhitaji mama kumweka mtoto kifuani
muda wote ilia pate joto la mwili badala ya kutumia mashine ambazo ni gharama
kubwa katika hospitali. Mama anayejifungua mtoto njiti anaweza kuruhusiwa kutoka
hospitalini mapema na akakaa nyumbani na mtoto wake endapo atakuwa na usaidizi
wa Baba wa mtoto katika kumsaidia kumweka mtoto kifuani (Kangaroo).
Utaratibu wa Kangaroo ulipendekezwa kwa mara ya kwanza mwaka
wa 1978 na madaktari wa watoto wawili katika kitengo cha uzazi katika Hospitali
ya San Juan de Dio huko Bogotá, Colombia. Leo hata Shirika la Afya Duniani
(WHO) linasema njia hii ni bora zaidi.
Mohamed Saleh, ni Mume wa Dada Saada Nassor Mohamed, wakazi
wa Dar es salaam nchini Tanzania ambaye amezaa watoto wawili (2) kabla ya muda (njiti), Mohamed analeza jinsi
avyowajibika kumsaidia mke wake katika malezi ya mtoto njiti ili kukoa maisha
ya mtoto lakini pia kupunguza gharama ambazo
zingelipwa hosipitalini.
“tulipitia kwenye kipindi kigumu kwa babu tulipata mtoto
njiti,gharama za Hopsitali zilikuwa kubwa, matunzo ya mtoto wodini ni Zaidi ya
shilingi 200,000 kwa siku, lakini
tulishauriwa kuondoka Hospitalini na tukatumia mfumo huu wa kangaroo, ambapo
Mimi kama (Baba) nililazimika kusaidia mke wangu kumweka mtoto kifuani ilia
pate joto”
Wakati mke wangu anajifungua hawa watoto Njiti, hasa huyu wa
mwisho, nilitoa muda wangu mwingi, ilinilazimu kufunga biashara ili nikae
nyumbani kumsaidia mke wangu kumtunza mtoto. Wakati tunaruhusiwa kutoka
Hospitalini tulipewa masharti endapo tunataka mtoto apone, basi, asishikwe na
mtu mwingine yeyote isipiokuwa mimi na Mama. Niliamua, ili mtoto apone na
kukua, ni lazima nitumie muda huo kumlinda na kumtunza kwa kuzingatia masharti
ya kulea mtoto njiti” anasema Mohamed
“ mfumo wa Malezi ya Kangaroo, una gharama kubwa,
nililazimika kuacha kazi kwa miezi 4, nikafunga biashara zangu ili nipate muda
wa kumlea mtoto apate joto na kukua”
anaongeza Mohamed.
Mohamed anawaasa wanaume wote kuwa karibu na wenza wao hasa
wakati wa ujauzito, kuhakikisha malezi ya mimba ni ya wote, lakini pia wanawake
wanapo zaa watoto njiti wasitengwe au kufanyiwa ukatili au kutelekezwa. “Nafasi
ya Baba ni muhimu sana ili kuwa na mtoto mzuri mwenye afya njema. Mwanaume
akishiriki kumtunza mtoto ataokoa gharama za matibabu, kwasababu mtoto
hatapatwa na maambukizi” anaongeza Muhamed
Kwa upande wa Bi. Saada Nassor Mohamed, akizungumzia mchango
wa Mume wake wakati alipojifungua mtoto
njiti anasema “ nilipojifungua mtoto njiti, kwanza sikuamini, nilipoona mtoto
hana hata umbo nzuri, nilistuka sana,
nikamwambia daktari kwamba amenibadilishia mtoto, nilimuita mume wangu na
kumweleza. Lakini alipofika alinitia moyo, alikaa na Daktari wakaelewana
wakaniweka vizuri. Mume wangu tangu siku hiyo hakuniacha mbali, aliacha
shughuli zake, akaanza kunisaidia katika malenzi ya Kangaroo, Nimeona mchango
mkubwa sana wa Mume wangu” anasema Bi. Saada.
Kwa upande wake Mkurugrenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake
(WFT-T) Tanzania, Bi. Rose Marandu, anasema kwamba changamoto ya uzazi wa kabla
au kuzaa mtoto njiti ni kubwa, na linahitaji kuwekewa kipaumbele na serikali
katika kutenga rasilimali fedha ili kuboresha huduma za afya, kuweka fedha
kwaajili ya kuboresha huduma kwenye zahanati na vituo vya afya vijijini ili
kuwezesha wanawake masikini wa vijijini kutokuhangaika kusaifiri mbali kufuata
huduma katika hospitali kubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Doris Moleli, Foundation,
Bi. Doris Moleli anasema kwamba, yeye alizaliwa mtoto njiti na kwa jinsi
alivyoona changamoto wanazokumbana nazo wanawake wanaozaa watoto njiti, ameamua
kujikita katika kupigania haki na kuteteza huduma za afya hasa kwa uzazi wa
watoto njiti ziboreshwe.
Sizya Puya ni Mama wa watoto Njiti, ambapo kila uzazi
aliopitia alipata mtoto njiti, na ameweza kulea
vizuri kwa kuzingatia masharti ya kulea na watoto wake wana afya njema
na wanaendeela na masomo.
Sizya anaeleza kwamba, nafasi ya Mzazi wa kiume ni muhimu
sana, kwa kuzingatia mahitaji ya kumelea mtoto njiti ni makubwa. “kuna suala la
rasilimali fedha, inahitaji fedha kuanzia nyumbani kuboresha mazingira na usafi
wa kila kitu, lakini gharama za matibabu, dawa, sindano, usafiri wa kwenda
hospitalini na kurudi, lakini pia usaidizi wa nyumbani hasa mama anapokuwa
anashinda ya kiafya kama maumivu ya mgongo, Baba atahitajika kumsaidia kumbeba
mtoto” anaeleza Sizya.
Doris anasema kwamba “…Imetokea mara kadhaa wanawake wana acha
kazi au kuachishwa kutokana na uzazi, mwaka 2017 tulianzisha hii agenda ya
kuomba serikali iongeze siku za uzazi kwa mama anayejifungua mtoto njiti,
mwaka 2018 tulishawishi wizara iongeze
siku za likizo ya uzazi kwa wanaume,
lakini haikufanikiwa. Mwaka 2019, tuliamua kuunganisha nguvu kwa kiasi kikubwa
na wadau wengine wengi Zaidi. Baadaye
WFT-T ilitusaidia kuunganisha nguvu na kuunda Mtandao wa SRHR ambapo tulipata nafasi ya kuwa na sauti ya pamoja katika
kupigania haki za wanawake na sasa tumefikia mafanikio ya kupata kifungu cha
sheria.
No comments:
Post a Comment