Friday, December 9, 2022

USHIRIKI WA JAMII KATIKA USHAWISHI NA UCHECHEMUZI KATIKA NGAZI YA SERIKALI ZA MITAA NA SERIKALI KUU

 USHIRIKI WA JAMII KATIKA USHAWISHI NA UCHECHEMUZI KATIKA NGAZI YA SERIKALI ZA MITAA NA SERIKALI KUU

WARSHA YA ASASI ZA KIRAIA ZINAZOTETEA HAKI ZA WANAWAKE NA USAWA WA KIJINSIA KWAJILI YA KUBORESHA MBINU ZA USHAWISHI A UTETEZI/UCHECHEMUZI YALIYOANDALIWA NA MTANDAO WA JINSIA TANZANIA (TGNP)

Disemba,2022

Inawasilishwa na Deogratius Temba.

Katika Hotel ya Tiffany- Dar es salaam

Mamlaka ya Wananchi katika kushiriki shughuli za maendeleo na upangaji wa Bajeti katika ngazi za jamii



Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), Mamlaka yote ya serikali na viongozi wa umma hutoka kwa wananchi. Hii ina maana kuwa wananchi ndio wenye mamlaka makubwa zaidi ambayo hutoa uhalali na mamlaka kwa serikali na vyombo vyake. Vivyo hivyo rasilimali zote za taifa na ugawaji wake kimatumizi vinakuwa chini ya mwananchi. Wananchi ndio wanaolipa kodi na kutoa michango mbalimbali inayoiwezesha serikali kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Kwa mantiki hiyo, wananchi ndio wenye maslahi na rasilimali zao, kwa mustakabali wa nchi yao.

Na hivyo, kuwa na haki yenye shauku ya kushiriki katika mchakato wa uandaaji wa bajeti na utekelezaji wake (matumizi) ni suala la msingi kwa kila mwananchi kulizingatia. Takwimu zinaonesha kuwa karibu asilimia 80 ya wananchi wote wa tanzania ni wakulima na wengi wao wakiwa wakulima na wafugaji wadogo na wa kati, ni muhimu kwa kundi hili kuzingatia mamlaka yake na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa bajeti. Kwa upande mwingine ni wajibu wa serikali kuzingatia na kuyafanyia kazi mapendekezo au vipaumbele vya kundi hili.

Umuhimu wa mamlaka za serikali za Mitaa

Kwa mujibu wa ibara ya 145 na 146 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali za Mitaa ni vyombo vya haki na vyenye mamlaka ya kushiriki na kushirikisha wananchi katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma katika sehemu zao. Serikali za Mitaa huanzishwa kwa madhumuni ya kuwahudumia wananchi na kuwapelekea madaraka kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

Majukumu ya serikali za Mitaa

       Majukumu na kazi za jumla na za lazima za Serikali za Mitaa ziko katika Sheria za Serikali za Mitaa Sura 287 na 288 Toleo la 2002 awali Sheria Na 7 na 8 za mwaka 1982.

       Katiba ya Tanzania inaelekeza kwamba Serikali za Mitaa zitakuwa na madhumuni, majukumu na kazi kuu tatu zifuatazo:

1. Kutekeleza    majukumu          ya  Serikali  za    Mitaa    katika    maeneo               ya mamlaka zao;

Majukumu ya serikali za Mitaa

       Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na usalama wa wananchi; na

       Kuimarisha demokrasia katika maeneo yake na kuitumia katika kuongeza kasi ya maendeleo ya watu (kwa kufanya vikao vya mashauriano)

       Hivyo majukumu ya Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri, Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji wote, msingi wake mkuu ni maelekezo hayo ya Katiba  na  Sheria  za  Serikali  za  Mitaa  pamoja  na  miongozo  na nyaraka mbalimbali zilizotolewa/zitakazotolewa na Serikali kwa mujibu wa Sheria.

Upangaji mipango katika Mamlaka za serikali za Mitaa

       Upangaji Mipango na Bajeti katika ngazi za msingi za MSM una anzia katika ngazi za Vitongoji/Vijiji au Mitaa ambapo Jamii inashiriki kufanya uchambuzi wa matatizo  na mahitaji halisi.

       Kabla ya upangaji wa mipango ya jamii, vijiji/mitaa vinapaswa kutambua jitihada za jamii zilizopo katika maeneo yao.

O&OD

       O&OD- Opportunity and Obstacles in Development (mchakato wa kuibua fursa na vikwazo katika maendeleo, ni mfumo unaosimamiwa na serikalini kupitia Ofisi ya Rais- Tamisemi, ambao unalenga kuwapa wanajamii nafasi ya kushiriki kikamilifu katika kuibua changamoto zao na kuweka vipaumbele vya kutekeleza kutokana na uwezo wao na pia uwezo wa serikali kwa wakati huo.

       Ni mpango unaolenga kuondoa dhana ya utegemezi kwa serikali, ambapo kupitia fursa ya kushiriki vikao vya kuibua, kupanga na kutekeleza, wananchi wanaweza kuwa na umiliki wa miradi inayotekelezwa kwenye eneo lao. Ni Mpango shirikishi unaoleta maendeleo ya haraka.

CHIMBUKO LA O&OD

       Ili kutekeleza adhima ya Ugatauji wa madaraka(D by D)  kikamilifu, Ofisi ya Rais- Tamisemi ilianzisha mfumo wa upangaji wa Mipango Shirikishi Jamii wa Fursa na Vikwazo katika maendeleo (Opportunities & Obstacles in  Development- O&OD) wa mwaka 2001

       Mfumo huu ulisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba mipango ya Maendeleo  inahusisha mahitaji  halisi ya jamii  katika ngazi ya msingi (kata, Mitaa na Vitongoji)

Changamoto za mfumo wa O&OD wa awali

       Ushiriki hafifu wa jamii- huu mfumo awali ulijikta katika uibuaji wa vipaumbele vya jamii kwa kutegemea serikali itekeleze vipaumbele hivyo. Hivyo kutokana na ufinyu wa bajeti, jamii ikakosa hamasa ya kuendelea kushiriki katika mchakato huu

       Jamii kukosa Moyo wa Umiliki wa Miradi: licha ya kushiriki katika mchakato wa kupibua na kupanga vipaumbele, umiliki wa mpango wa bajeti ulibaki mikononi mwa halmashauri na kazi ya jamii iliishia kuibua vipaumbele tu

       Utegemezi wa jamii kwa serikali: Mchakato wa Uibuaji wa vipaumbele vya miradi ya maendeleo ulifanya jamii kuamini kwamba baada ya kuibua miradi yao ya maendeleo serikali itatekeleza. Hali hii liifanya jamii kuachana masuala yote ya msingi kwa serikali hata yale yaliyo ndani ya uwezo wao

MFUMO WA O&OD ULIOBORESHWA

       Katika kutatua changamotozilizoainishwa hapo juu: na kuliwezesha taifa kufikia maendeleo endelevu, serikali imefanya maboresho katika mfumo huu kwa kuishirikisha jamii katika hatua za awali za kuibua, kupanga na kuonesha jitihada zao.

       Msingi mkuu wea mfumo wa O&OD ulioboreshwa  umejikita katika dhana ya kwamba wananchi ndio wahusika wakuu wa shughuli z maendeleo bila ya kuisubiria serikali ifanye kwaajili yao.

       Katika mfumo wa O&OD  ulioboreshwa wanajamii watapanga  mipango yao kulingana na mahitaji halisi, uwezo wa kitaasisi,  na rasilimali walizo nazo kwa kushirikiana na MSM

UMUHIMU WA MFUMO WA O&OD ULIOBORESHWA

       Kujenga uwezo wa jamii

       Uendelevu wa Miradi

       Kupungua kwa gharama za Utekelezaji wa Miradi

       Kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina ya jamii na serikali

       Utawala Bora katika ngazi ya msingi

       Maendeleo ya Kiuchumi katika ngazi za Msingi

 

MCHAKATO WA KUANDAA BAJETI NA KUINGIZA MASUALA YA KIJINSIA

DATE/ MONTHS

SHUGHULI INAYOFANYIKA WAKATI HUU

TAASISI HUSIKA

FURSA ILIYOPO KUTOKA KWA WADAU

JULAI O1-JUNI 3O

Huu ni mwaka wa utekelezaji wa Bajeti ya  Mwaka wa fedha ambao umeanzia Julai 1, na utathimini na ufuatiliaji

Wadau wote wa maendeleo, serikali na jamii

Ni kipindi cha kusambaza machapisho, tafiti, chambuzi  za Bajeti kwa mrengo wa kijinsia. Na kufuatilia utekelezaji wake

 

Agosti - Septemba

Maandalizi ya Bajeti ya mwaka mwingine wa fedha. Halmashauri zinawasilisha mwongozo wa mchakato wa kukusanya maoni ya vipaumbele vya Miradi kwa serikali za Mitaa/Vijiji/Kata.

 

MAANDALIZI YA MWONGOZO WA BAJETI NGAZI YA TAIFA

Halmashauri, WDC/ Vijiji/Mitaa

 

 

Kamati ya Bajeti, DPPs, Makatibu wakuu, kamishina wa bajeti

-Mafunzo kwa CMT, Mafunzo kwa WDC, WEOs,VEOs, na waheshimiwa madiwani juu ya uandaaji wa Bajeti

 

 

 

Kukutana na DPPs na kamati ya Bajeti ngazi ya Taifa, OR-TAMISEMI, na wadau wengine wa bajeti. Mashirika ya kijamii yanafursa kubwa kujenga mahusiano na serikali katika eneo hili

Oktoba

Vikao vya robo ya pili ya Mwaka vinafanyika kupitisha maoni ya wananchi kuhusu miradi ya vipaumbele/ Kila Kijiji kinafanya mikutano hii muhimu.

VEOs/Wenyeviti wa Vijiji na wananchi wote

Kutumia fursa hii kuwawezesh ili wawe na jicho la kijinsia wakati wa kuibua, wananchi/ vikundi vilivyofanyiwa  mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia

Novemba- Disemba

Mipango ya Mitaa/Vijiji iliyopangwa kwa kutumia mchakato shirikishi wa kuibua fursa na vikwanzo (O&OD) wakisaidiwa na watendaji wa Halmashauri- vinatumwa Halmashauri kwa kupitiwa.

WDC/WEO

Mafunzo kwa madiwani ili kuwanadaa kupokea mipango ya halmshauri, CMT ki- halmashauri wanaweza kujengewa uwezo wakati huu kwa kunagalia chambuzi za bajeti za nyuma kwa mrengo wa kijinsia, mapungufu yake

Disemba

WDC zinakaa kupitisha  na kuziunganisha Mipango ya Bajeti kutoka kwenye vijiji /Mitaa yote ya Kata na kuiwasilisha Halmashauri

WDC/WEO

Jamii iwezeshwe  kuwa na agenda na mapendekezo yao ya bajeti  na yawasilishwe kwenye Kata. CSOs zijitahidi kushiriki vikao vya WDC, kama hawaalikwi wanapaswa kuulizia kwa WEO

Januari

Mipango ya Kata, inapitiwa na Halmashauri, na kuunganishwa pamoja ili kuwa na Bajeti moja ya Halmashauri

CMTs na kamati ya Bajeti ya Halmashauri

Mafunzi kwa CMT wakiwa pamoja, kuangalia masuala waliyoyazingatia katika bajeti zao.

Februari

Majukwaa ya Kiushauri yanakutana kupitia Bajeti ya Halmashauri (DCC/RCC) na Baraza la Madiwani kwaajili ya kupitisha Bajeti ya Halmashauri

DCC/RCC/Kamati za kudumu za Madiwani, wadau wengine

Asasi za Kiraia ni wajumbe wa Kikao hiki. Wanapswa kushiriki, wakiwa na agenda na waishauri serikali kuzingatia usawa wa Kijinsia katika bajeti

Februari

Mapitio na Marekebisho ya Bajeti za Halmashauri iliyopitishwa na Full Council, DCC, RCC

OR- TAMISEMI- idara ya bajeti za serikali za Mitaa

Kuendelea kufanya kazi na idara ya bajeti za serikali za Mitaa

Machi

Mapitio ya Bajeti za Halmashauri , kuingiza Takwimu, na kuchapisha vitabu vya bajeti (kamati ndogo ya Bajeti ya serikali kuu inakaa)

Wizara ya Fedha, Utumishi, OR-TAMISEMI,

Kuendeela kuziandaa Kamati za Bunge juu ya masuala ya msingi ya kijinsia ili wakipokea Bajeti wawe na jicho la kijinsia

Aprili- Juni

Mjadala wa kina juu ya Bajeti zote za sekta na Bajeti ya Jumla kwenyekamati za Bunge na Bunge linapitisha Bajeti husika

Bunge na wataaluamu kutoka wizara zote za kisekta

Kushiriki na kufuatilia mijadala na kuweka ushauri Zaidi wa kitaalamu

MASWALI YA VIKUNDI

No comments:

Post a Comment