Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeandaa mafunzo ya kuimarisha uwezo
wa ushawishi na uchechemuzi kwa mashirika yanayotetea haki za mwanamke na
usawa wa kijinsia yaliyoanza leo
Desemba 06 hadi 09, 2022 yakiwa na lengo la kuongeza uelewa wa dhana ya
kijinsia, kuongeza ujuzi wa washiriki wa ushawishi na
uchechemuzi wa masuala ya kijinsi, kutambua fursa zilizopo kwa ajili ya kuwezesha
uchechemuzi ngazi ya Serikali pamoja na
kuandaa mikakati na mipango kwa ajili ya kujega sauti na utendaji wa pamoja
na katika ushawishi na uchechemuzi wa masuala
ya kijinsia.
Akizungumza Mwezesha wa Mafunzo hayo Mary Nsemwa amesema washiriki wa
mafunzo haya ni wadau mbalimbali kutoka Taasisi mbalimbali zunazoshughulikia
masuala kijinsia pamoja na haki za wanawake
hivyo wamekutanishwa hapa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ili kuwaongezea
uelewa kuhusu masuala ya kijinsia ili
waweze kuongeza ushawishi zaidi kwenye jamii.
Amesema Suala la ukatili wa kijinsia linatokea kwasababu nyingi lakini ukiangalia
nyuma ya hili ni kuwa ukatili wa kijinisa umebeba nguvu na mfumo duni kwasababu
anayefanya ukatili anajiona yeye ndo
mwenye nguvu kuliko anayemfanyia ukatili mfano ukatili wa mwanaume kwa
mwanamke hii ni kutokana na Mwanume kujiona
yeye ana nguvu na hata jamii pia inamuona ni mtu wa tofauti au mwanamke kwa mtoto
kwasababu yeye anauwezo wa
kufanya chochote kwa mtoto wake.
pia amesema wadau hawa wakijengewa uwezo na kujenga sauti ya pamoja ya kukemea
masuala yote ya ukatili wa kijinsia watakwenda kujenga msingi mzuri hasa kutengeneza
vuguvugu na nguvu zaidi kwenye suala
la kupunguza ukatili wa kijinisia maana zikiachwa ziendelee zitakuja kuleta madhara
makubwa baadae kwenye jamii na
hasa zitamuumiza sana Mama na mtoto.
Naye mnufauka wa mafunzo Selina Lyapinda ameushukuru Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP
) kwa kuweza kuwapa mafunzo hayo kwani yatawaongezea uelewa kwenye masuala
ya kijinsia na kupambana na masuala haya kwenye jamii ambayo yamekidhiri.
\Mwezesha wa Mafunzo Mary Nsemwa akiwasilisha mada iliyokuwa inahusu dhana
za Jinsia na maana yake katika muktadha wa sasa wakati wa mafunzo ya
kuimarisha uwezo wa ushawishi na uchechemuzi kwa mashirika yanayotetea
haki za mwanamke na usawa wa kijinsia yaliyoanza leo Desemba 06 hadi 09, 2022
yakiwa na lengo la kuongeza uelewa wa dhana ya kijinsia yaliyoandaliwa na Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu kuongeza
ujuzi wa washiriki wa ushawishi na uchechemuzi wa masuala ya kijinsi na kijinsia
wa mafunzo ya kuimarisha uwezo wa ushawishi na uchechemuzi kwa mashirika
yanayotetea haki za mwanamke na usawa wa kijinsia yaliyoanza leo
Desemba 06 hadi 09, 2022 yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)
yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakichangia mada zinazohusu namna ya kuongeza
kuongeza ujuzi wa washiriki wa ushawishi na uchechemuzi wa masuala ya
kijinsi na namna ya kuongeza uelewa wa dhana ya kijinsia kwa mashirika
yanayotetea haki za mwanamke na usawa wa kijinsia wakati wa mafunzo
yalioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) yaliyoanza leo Desemba
06 hadi 09, 2022.
Baadhi ya washiriki wakijadiliana kwenye makundi ili kuongeza kuongeza ujuzi
wa washiriki wa ushawishi na uchechemuzi wa masuala ya kijinsi na namna ya
kuongeza uelewa wa dhana ya kijinsia kwa mashirika yanayotetea haki za
mwanamke na usawa wa kijinsia wakati wa mafunzo yalioandaliwa na Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP) yaliyoanza leo Desemba 06 hadi 09, 2022.
No comments:
Post a Comment