Friday, December 9, 2022

Mashirika yanayotetea Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia kupambana na Ukatili wa Kijinsia

Mashirika yanayotetea Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia kupambana na Ukatili wa Kijinsia Na Deogratius Temba Mashirika yanayotetea Haki za wanawake na Usawa wa Kijinsia nchini yamekubaliana kwa pamoja kushirikiana katika ngazi ya wilaya kuzuia vitendo vya Ukatili wa Kijinsia unaotokana na uwepo wa mila na desturi kandamizi na zilizopitwa na wakati ili kulinda utu na hadhi ya mtoto wa kike Wakizungumza wakati wa kuweka maazimio ya kuhitimisha mafunzo ya siku nne ya kujenga uwezo juu ya Ushawishi na Utetezi yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), walikubaliana kwamba, watahakikisha katika ngazi ya wilaya wanaendeleza na kuimarisha nguvu ya pamoja na TAPO la harakati za utetezi wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia ili kutokomeza vitendo vya Ukatili, udhalilishaji.
Aidha katika mafunzo hayo, wamekubaliana pia, kwenda kujenga uwezo kwa jamii kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uandaaji wa Bajeti katika ngazi ya jamii, hasa mchakato wa O&OD, ili kuweza kushawishi bajeti za serikali za Mitaa zizingatie mahitaji ya kijinsia. Awali washiriki hao, walipitishwa lkatika mzunguko wa Bajeti na fursa zilizopo kwa CSOs/ WROs kuibua masuala ya kijinsia ngazi ya jamii na kuyafanyia ushawishi na uchechemuzi ili yaingizwe kwenye bajeti za Halmashauri.
Malengo ya mafunzo haya ni; Kubainisha umuhimu wa asasi kujihusisha na michakato sera na bajeti ya kijinsia katika muktadha wa Tanzania, Kuhamasisha ujenzi wa nguvu za pamoja na mbinu za kimkakati katika kushawishi uingizwaji wa masuala ya jinsia katika bajeti.
Washiriki walikubaliana kwamba; kuna haja ya washiriki wote kwenda kutoa elimu au kufanya mrejesho kwa ofisi zao kili kurejesha elimu ya usawa wa kijinsia na kuzifanya taasisi ziwe na mrengo wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment