Friday, December 9, 2022

DHANA MUHIMU ZA JINSIA

DHANA MUHIMU ZA JINSIA KATIKA MUKTADHA WA UONGOZI  NA USAWA WA KIJINSIA  
  Dhana Maana 

1. Jinsi Hii inahusu hali ya kibaiolojia ya mtu ambapo atajulikana kama mwanaume au mwanamke (KE and ME]. Hali hii haitofautiani kati ya tamaduni moja na nyingine. Na haibadiliki kwa namna yeyote. 

 2. Jinsia Hii inahusu tabia na kazi zinazofanywa na wanaume na wanawake kulingana na matarajio ya jamii. Tofauti na ilivyo kwa kazi za kibilojia, kazi kijinsia zinatofautiana kati ya jamii moja na nyingine. Kila jamii ina itikadi yake kuhusu jinsia, na inatoa tafsiri kuhusu kazi zipi ni za wanaume na ni zipi za wanawake, haki zao ni zipi, majukumu, pamoja na umiliki wa raslimali. Kila mwana jamii wa jamii husika atajifunza kuhusu mitazamo ya jamii yake tangu akiwa mtoto na wakati wa kupokelewa katika rika la utu uzima. 

Tofauti za kijinsia hutokea pale ambapo kazi, haki, majukumu, na raslimali hutofautishwa kati ya wanawake na wanaume. Kazi nyingine za kijinsia zina mizizi iliyojikita katika utamaduni na pengine huwa chanzo cha kunyanyua na kuwapa thamani watu katika jamii husika huku nyingine zikishusha thamani ya wengine.

 3. Uchambuzi wa kijinsia: Huu ni mchakato wa kuchambua kazi na majukumu au suala lingine lolote lile linalohusu wanawake na wanaume, wavulana na wasichana, kwa lengo la kutambua mahitaji mahususi ya wasichana na wavulana, wanawake na wanaume kwa ajili ya uandaaji na utekelezaji wa sera na programu za maendeleo. 

 4. Ubaguzi wa Kijinsia Kunyima fursa na haki au kutoa upendeleo kwa watu fulani kulingana na jinsia zao. 

 5. Usawa wa kijinsia (equality) Hii inahusu utoaji haki, heshima, na fursa sawa kwa wote bila kujali jinsia. 

 6. Fursa sawa kwa Jinsia (Equity) Hii ni kanuni ya haki sawa na utoaji wa huduma inayofanana kwa wanawake na wanume na hii hupelekea katika usawa wa kijinsia baada ya kipindi cha muda mrefu.

 7. Mtazamo potofu wa Kijinsia (Stereotype) Hii inahusu taswira potofu juu ya wanawake au wanaume ambazo hazina msingi wa kisayansi au uthibitisho wa kisayansi. Mara nyingi hutokana na imani za kitamaduni au za kidini, au maadili ya kimila. 

  10 Mwongozo wa Mafunzo Juu ya Uhamasishaji wa Wanawake kuhusu Uongozi 

 8. Uzingatiaji wa Jinsia Ni mchakato unaolenga kuhakikisha kuwa wanawake na wanaume wana haki sawa ya umiliki na usimamizi wa raslimali, manufaa ya maendeleo, na utoaji wa maamuzi katika hatua zote za shughuli za maendeleo kwa kuhakikisha kuwa mahitaji, masilahi, na vipaumbele vya wanawake na wanaume yanazingatiwa katika sera, programu na miradi yote. Hii itahitaji: a. Tathmini endelevu ya matokeo na madhara ya sheria, miradi na sera juu ya wanawake na wanaume b. Uandaaji na utekelezaji wa mikakati na shughuli ambazo zinalenga kushughulikia kwa ubora zaidi mahitaji ya wanawake na wanaume, kuboresha hali za maisha yao, na kuwezesha ushiriki wao katika shughuli za maendeleo. 

  9. Upofu wa Kijinsia Ni kushindwa kutambua kuwa mahitaji ya wanawake na wanaume yanatofautiana. Mtazamo wenye upofu wa kijinsia unachukulia kuwa suala la jinsia halina umuhimu katika miradi, programu, au sera (UNDP 2007). 

 1O. Uongozi wa kimageuzi wa kifeministi. Ni uongozi ambao msingi wake ni nadharia ya usawa wa kijinsia kuhusu haki katika jamii ambayo imeleta mabadiliko kwa mtu binafsi na kwa kundi katika kutumia nguvu yake, raslimali na ujuzi, kwa njia isiyo na ukandamizaji, kwa kupitia mifumo jumuishi na michakato ili kuhamasisha wengine – hususan wanawake na makundi mengine yaliyoko pembezoni na kuwainganisha chini ya ajenda ya pamoja ya jamii, utamaduni, mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa kwa lengo la kuleta usawa na kupata haki za binadamu kwa watu wote (Wakefield 2017). 

 11. Ukatili wa Kijinsia Ukatili wa kijinsia ni ukatili dhidi ya wanaume kutokana na mwanamke kuwa na nafasi ya chini kaitka jamii. Hii inajumuisha tendo au tishio lolote, linalofanywa na mwanaume au taasisi iliyotawaliwa zaidi na wanaume, anbalo litasababisha madhara ya kimwili, kingono, au kisaikolojia kwa mwanamke au msichana kutokana na jinsia yake ya kike. Katika tamaduni nyingi, imani za kimila zinahalalisha na hivyo kuendeleza ukatili dhidi ya wanawake. Ukatili wa kingono ni pamoja na ukatili wa juu ya mwili, wa kijinsia, wa kisaikolojia mfano ni ukatili wa majumbani, unyanyasaji wa kingono kama vile ubakaji na unyanyasaji wa kingono wa watoto unaofanywa na wanafamilia, mimba za kulazimishwa, utumwa wa kingono, vitendo vya kimila vinavyowadhuru wanawake kama vile mauaji ya kimila, kuchomwa moto au kumwagiwa tindikali, ukeketaji wa sehemu za siri za wanawake, unyanyasaji unaohusiana na mahari, unyanyasaji katika maeneo ya vita kama vile mauaji, unyasaji wa kihisia kama vile kulazimishwa na matumizi ya lugha ya kashfa. Usafirishaji haramu wa wanawake na wasichana kwa ajili ya biashara ya ngono, ndoa za kulazimishwa, unyanyasaji wa kijinsia na vitisho mahali pa kazi nayo ni nyongeza za mifano ya ukatili dhidi ya wanawake. Unyanyasaji wa kijinsia hutokea katika maeneo ya ‘umma’ na ‘binafsi’. Ukatili huu hautokei katika familia na jamii pekee lakini mara nyingine huendekezwa na taifa kwa kupitia sera zake au vitendo vya vyombo vya serikali kama vile jeshi la polisi, mamlaka za kijeshi au uhamiaji. Ukatili wa kijinsia hutokea katika kila jamii katika matabaka yote ya jamii huku wanawake wakiwa wapo katika hatari zaidi ya kuathiriwa na wanaume wanaowafahamu. 

 12 Mgawanyo wa majukumu kijinsia (gender roles) Ni kugawana majukumu kulingana na jinsi au jamii husika. Ni muhimu kuzingatia kwamba yapo majukumu mahususi kwa wanawake kutokana na maumbile mfano kubeba ujauzito, kujifungua, kuingia hedhi, na kunyonyesha ilihali jukumu la wanaume kijinsi ni kutunga mimba. Mahitaji haya yanamfanya mwanamke uhitaji rasilimali zaidi za kibajeti kuliko mwanaume. Majukumu mengine yote kando ya haya tunayaita majukumu ya kijinsia ambayo hujengwa na jamii husika 

 13. Mahitaji ya kimkakati kijinsia (Gender strategic needs) Ni mahitaji yanayowezesha safari ya maendeleo ambayo kila mtu anatakiwa kuyapata katika jamii ili kumkwamua kiuchumi au kijamii. Mfano elimu kuhakikisha kila shule ina mabweni ya wasichana, fursa za mikopo eg 4.4.2, CHF, ufikiaji wa rasilimali nk 

 14 Mfumo Dume au Mfumo Kandamizi (Patriarchy) Huu ni mfumo, hauna sura ya kike wala ya Kiume. Ni mfumo wa kuhodhi madaraka, maamuzi na umiliki wa rasilimali. Kwa vile wanaouhodhi mara nyingi ni wanaumme, basi ni Mfumo wa maisha unaopendelea wanaume katika ngazi zote kuanzia kaya, jamii, taifa hadi kimataifa. Mfumo huu unaelekeza umiliki wa rasilimali, maamuzi na majukumu ya kazi. Katika ngazi zote mfumo huu unawapendelea wanaume hasa wazee na kutoa nafasi, miliki kidogo sana kwa wanawake na vijana. Mfumo unaendelezwa na sera, sheria na mikakati mbalimbali ya maendeleo. Umejikita katika nyanja zote za maisha kupitia malezi na makuzi, elimu, mila na desturi

No comments:

Post a Comment