TGNP yaendesha utafiti raghibish kata ya Mgagao Mwanga
- · Wanachi
Mgagao Mwanga wana na mapendekezo
Na Deogratius Koyanga
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),
umewawezesha wananchi kutoka kata ya Mgagao, Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga,
Mkoani Kilimanajro kuendesha zoezi la utafiti uraghibish ili kutokomeza vitendo
vya Ukatili wa Kijinsia na kukuza usawa wa Kijinsia.
Zoezi hilo ni sehemu ya mradi wa Kuvunja vikwazo: kuondoa na kutokomeza
Ukatili wa Kijinsia na Kukuza usawa wa Kijinsia unaotekelezwa na TGNP katika halmashauri hiyo.
Ambapo jamii imejengewa uwezo namna ya kuibua, kuchambua na kuweka mikakati ya
utatuzi wa changamoto zinazowazunguka kwa kushirikiana na viongozi katika ngazi
mbalimbali, sambamba na kuundwa kwa Kituo cha Taarifa na Maarifa katika kata
hiyo.
Miongoni mwa changamoto za ukatili wa
kijinsia zilizoibuliwa na kuwasilishwa mbele ya Mkururgnzi Mtendaji wa Wilaya
ya Mwanga, Bi. Zuhura Msangi, na wakuu wa Idara na Vitengo ni pamoja na Suala
la kushamiri kwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kama vile Ubakaji kwa wanawake
hasa wasichana, mimba za utotoni, ukeketaji wa wasichana na kuongezeka kwa
uporaji wa mali hasa mifugo.
Katika mapendekzo yao, washiriki wa
uraghibish huo, walipendekza kwamba;
Halmashauri
iweke sheria kali za vijiji na wasimamizi wa sheria (Polisi na mahakama) na
vyombo vingine zifanye kazi kwa uadilifu ili sheria itekelezeke. Halmashauri
isimamie mchakato wa uandaaji wa bajeti uwe shirikishi kuanzia ngazi za kijiji
ili tuwe na bajeti yenye mrengo wa Kijinsia itakayogusa mahitaji ya kila kundi.
Kuuhuisha
kamati za Ulinazi wa Mama na Mtoto (MTAKUWWA) katika kata na vijiji vyote,
zitambue majukumu yake na mfumo wa uwajibikaji yaani ziwe na taarifa zake za
utekelezaji.
Mwongozo
wa serikali (Feb. 2022) wa kuwarudisha wanafunzi walioacha masomo kwa sababu
mbalimbali uanze kutumika ndani ya Kata. Mratibu Elimu Kata (MEK) aanze
kuwabaini wasichana walioko mitaani na kuwarudisha shuleni kwa mujibu wa
mwongozo.
Halmashauri
isaidie usimamizi na utekelezaji wa
sheria ndogo ambazo zitathibiti watoto wa shule kuzurura hovyo siku ya Ijumaa
mnadani na katika magenge na kwenye
vibanda vya kuoneshea Video.
Sheria
kali zichukuliwe dhidi ya kutokomeza Mimba na ndoa za utotoni. Maafisa Ustawi
wa jamii na Maendeleo ya jamii washirikiane na dawati la Jinsia na
Mtoto-Polisi, kuharakisha kesi za ubakaji na wanaobainika wahukumiwe kwa mujibu
wa sheri zetu.
Halmashauri
isimamie watendaji wa Vijiji kufanya mikutano ya kisheria ya vijiji sambamba na
mikutano maalum ya kuibua na klujadili vipaumbele vya Bajeti au miradi ya
maendeleo (Mchakato wa uibuaji wa fursa na vikwazo katika maendeleo-[O&OD].
Ili kuweka kipaumbele masuala muhimu kama haya ya maji, mabweni nk.
Mradi wa
umeme wa REA wa Kijiji cha Pangaro, uweke kipaumbele kwenye shule za msingi,
zahanati ili kuboresha huduma na
kuwavutia watumishi kufanya kazi katika maeneo hayo
Kuendelea
kushirikiana kati ya jamii na serikali kutoa elimu na kuzuia vitendo vya
Ukeketaji katika jamii ya Mgagao hasa vitongoji vinavyotajwa kuwa na mila hizo.
Kwa
upande wa menejimenti ya Halmashauri, waliahidi kusimamia utekelezaji wa
mapendekezo haya, ikiwa ni pamoja na kuwezesha utekelezaji wake katika ngazi za
chini sambamba na ujenzi wa Bweni kubwa la kisasa ambalo litaanza kujengwa hivi
karibuni katika shule ya sekondari ya Mgagao.
Kuhusu suala
la maji, mwakilishi wa wakala wa Usimamizi na usambazaji wa Maji Vijijini
(RUWASA) alisema kwamba maji ya mradi wa Mwanga,Same Hedaru ayanayokatiza
katika kata hiyo ataanza kutumika katika kijiji cha Mgagao na vitongoji vyake sambamba
na shule ya sekondari Mgagao hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment