Friday, May 26, 2023

Wazee wataka utamaduni wa asili 'Vikome' urudi usukumani

Wazee wataka utamaduni wa asili ‘vikome’ usukumani urudi

 Na Mwandishi Wetu, Msalala

 Wanaume kutoka kata za Lunguya na Shilela, Halmashauri ya wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, wameitaka jamii kurudisha utamaduni wa asili wa kukaa na familia maarufu kama vikome ili kurudisha maadili ambayo yameporomoka.
Wakizungumza katika mdahalo wa wanaume uliolenga kujenga mjadala juu ya nafasi ya wanaume katika kuzuia vitendo vya Ukatili wa Kijinsia na kuacha mila na destri kandamizi ulioendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), walisema kwamba, mila hiyo ya asili ni muhimu sana ikarudi kwani ilisaidia sana kujenga jamii kuanzia ngazi ya familia. 

 Amesema kwamba kuna umuhimu mkubwa kwa jamii kurudisha utamaduni wa asili wa kufanya vikao vya familia (vikome) kati ya Baba na watoto ili kujenga maadili mema, na kukemea tabia chafu ikiwa ni pamoja na kujenga uwajibikaji katika familia. “turudishe utamaduni wa asili, vikao vyetu vya Baba wa familia na watoto vilikuwa na maana sana wakati ule, tumekimbilia tamaduni za nje, umesahau mamabo yetu. Vikome vilisaidia sana kujenga maadili. Wazee w a leo, wamekuwa hivyo kwa sababu ya vikao vya familia (vikome) siku hizi hakuna” alisema Mchungaji Joseph Mwamashimba.

 Mwezeshaji wa Midahalo huo kutoa TGNP, Deogratius Temba, alisema kwamba, mdahalo huo ni sehemu ya mradi unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa mataifa la idadi ya watu (UNFPA), na Shirika la Msaada wa Korea (KOICA), ambao unalenga kubadilisha mitazamo, mila na destru kandamizi zinazochangia Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto.

No comments:

Post a Comment