Thursday, May 4, 2023

TAKUKURU mkoa wa Singida tokomezeni rushwa ya ngono- RC Serukamba

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba,ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani kwa kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kuhakikisha rushwa ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia inatokomezwa katika mkoa huu.
Akizungumza leo Mei Mosi wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi kimkoa zilizofanyika Manispaa ya Singida, amesema tatizo la rushwa ya ngono ni lazima likomeshwe kwenye Mkoa wa Singida. Serukamba amewagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ambao bado hawajawalipa posho watendaji wa kata kuwalipa ndani ya miezi mitatu na kutoa taarifa kwake. "Nichukue nafasi hii kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuwapandisha madaraja watumishi waliokuwa wanastahili hali ambayo imeleta motisha na tija katika utendaji kazi kwa watumishi ," amesema Serukamba.

No comments:

Post a Comment